Kunambi: Suala la utoaji haki linahitaji umakini

beth

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
3,877
6,326
Mbunge Godwin Kunambi amesema jambo la utoaji wa Haki ni gumu na linahitaji umakini mkubwa kwenye maamuzi

Ameeleza hayo Bungeni ambapo amegusia Sheria za utakatishaji Fedha na Uhujumu Uchumi akisema zilitungwa kwa nia njema, lakini changamoto iliyopo sasa ni utekelezaji wake

Ameeleza, "Kuna adhabu ukipewa na kosa umetenda hata usiposema nafsi yako itasema kweli nilikosea. Lakini ukionewa nafsi ina masikitiko na manung'uniko, Mungu anasikia"

Amesisitiza suala la umakini Ofisi ya DPP akisema Watanzania wanalalamika. Ametoa rai kwa Waziri kufuatilia jambo hilo akisema, "Kama ikisadikika Wananchi ni kweli wana makosa Sheria ichukie mkondo wake"
 
DPP ni wa ukanda ule , sasa hajui amsikilize nani kwa sasa. Na alikuwa TRA wakati ule .
 
Back
Top Bottom