Kuna watu wanatumiwa kuchafua na kuharibu nchi.....

kwa-muda

JF-Expert Member
Sep 5, 2018
1,176
2,000
Hii kauli ndiyo imeshika kasi awamu hii kwa yoyote ambaye atakuwa na mtazamo tofauti na wenye chama basi atakuwa anatumiwa na wananchi wengi wameaminishwa hivyo.
Jambo ambalo limenistajaabisha zaidi ni kusikia wafanya biashara wa korosho wanatumiwa na vyama pinzani eti wameweka mgomo kununua korosho wanatumiwa.
Hivi kwa akili ya kawaida kuna mfanya biashara anaweza acha biashara yake inayo muingizia faida kisa ameambiwa afanye hivyo na chama pinzani? Numbers never lie, ukiona wafanya biashara wote wamegoma kwenda kununua korosho kwa hiyo bei basi ni wazi kwamba wamegundua watakula hasara mbona mwaka jana hawakulazimishwa na wakanunua.
Naona rungu limewaangukia waziri wa biashara na waziri wa kilimo.
Ninahisi tunatumia nguvu sana kutatua mambo ambayo yanahitaji kutatuliwa kitaalamu, na kuwafungia kwa kutonunua korosho kwa bei itakayowatia hasara lazima itakuwa na affect maana action and reaction are equal but opposite in direction.
Uchumi ni hesabu na hesabu haidanganyi majibu yataonekana kwente long run na uchumi haujengwi kwa ubabe bali kwa maarifa.
Ukitaka kujua kuwa hili jambo serikali inahaha kuwa prove wakina zitto wrong wakati wanapinga serikali kuchukua ela ya korosho kutaua zao, ndiyo maana huioni ikihangaika na bei ya mahindi iliyoanguka mpaka sehemu nyingine gunia la mahindi 15,000. Mbona serikali hujasikia inasema itawasaidia kutafuta soko au kuwashawishi wafanya biashara wanunue mahindi kwa bei nzuri.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom