Kuna Watu Ni Bure Kabisa! ππ
1. Unapewa lift unamwambia mwenye gari apunguze sauti ya redio na wakati kuna ngoma yake anasikiliza! Wewe ni bure kabisaπ!
2. Unaingia kwenye ofisi ya mtu, simu inaita unapokea na kuanza kuongea tena kwa sauti ya juu, wanakukata jicho huelewi maana! Wewe ni bure kabisaπ!
3. Unakwenda kwa watu unalazimisha ulale pale na wakati wenzako sebule ndiyo chumba, usiku wanatandika vya kulalia, unawasababishia kero. Wewe ni bure kabisa!
4. Unamuomba mtu hela, amekwambia siko vizuri, lakini unaendelea kulazimisha akupe utadhani ulimuwekeza. Wewe ni bure kabisaπ!
5. Unaenda sehemu, unakuta watu wana mazungumzo yao, unakaa na kuanza kuongea mambo yako bila kujua ajenda yao. Wewe ni bure kabisaπ!
6. Unaazima gari la watu lina mafuta, unatumia unarudisha taa inawaka, unashindwa kuongeza. Wewe ni bure kabisaπ!
7. Unamkuta mtu yupo bize na laptop anafanya kazi halafu unaanza kumuongelesha. Wewe ni bure kabisaπ!
8. Unataka kumpigia mtu simu wakati wa kazi ili tu mpige stori za hapa na pale, akisema ntakucheki unasema anaring. Wewe ni bure kabisaπ!
9. Unawahi nyumbani unakuta familia inaangalia vipindi vyao kwenye TV unaondoa channel yao unaweka mpira. Wewe ni Bure kabisa!
10. Unapiga simu ya kwanza haipokelewi, simu ya pili haipokelewi, unapiga mpaka mara 20 haipokelewi. Wewe ni bure kabisaπ!
11. Unakuta missed calls kwenye simu yako, huwatafuti waliokupigia na meseji zao hujibu. Wewe ni bure kabisaπ!
12. Chakula kimekuja, bakuli lina minofu mitano ya kuku na mko watano lakini wewe unapakua minofu miwili. Wewe ni bure kabisaπ!
13. Unaamka asubuhi na kuzunguka kwa majirani zako na mswaki mdomoni! Wewe ni bure kabisa!
14. Kila unayekutana naye unaanza kumpa stori za mpira ukidhani kila mtu ni shabiki wa mpira.
Wewe ni bure kabisa!
15. Unataka watu wote wakubaliane na mawazo yako, wakikupinga unazila
UNASUSA..
. Wewe ni bure kabisaπ!
*