Kuna watu bado wanaamini kuna mabadiliko chini ya CCM?

Shukrani A. Ngonyani

JF-Expert Member
Joined
Feb 23, 2014
Posts
1,182
Reaction score
2,021
Niwe tu muwazi, uwezo wa kufikiri umetofautiana sana, na uwezo wa kuchambua mambo na kuyawasilisha mbele ya watu pia tumetofautiana.

Nimetazama sana hizi siku 60 na ushee za mh. Rais Magufuli nimejikuta naanza kuendelea kuamini hakuna mabadiliko ya dhati yanayoweza kuletwa chini ya uongozi wa CCM.

Ndani ya siku 60 tu tumeshuhudia akifanya makosa ambayo ni "grave mistakes". Hebu tuyatazame kwa uchache.

1. CCM imeingia ktk uchaguzi mkuu ikiwa na harufu mbaya ya ESCROW, bunge likapitisha maazimio mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuwawajibisha watendaji na viongozi waandamizi waliohusika ambao wameteuliwa na rais, hapo ndipo prof. Mwijarubi Muhongo na bwana Eliakimu Maswi walitakiwa wawekwe kando.

Cha ajabu teuzi za mh. Magufuli amewarudisha hawa waliobariki wizi ule, hii inanipa dhana tatu.
(a)Huenda madai ya wapinzani wakati wa kampeni kuwa pesa ya Escrow zimekwenda kugharamia kampeni za CCM?
(b)Bunge kama muhimili wa dola umepoteza sifa na heshima yake, kwani hiyo ni dharau dhidi ya taasisi ya bunge.
(c)Hakuna wizi ambao unatendeka pasi na CCM kufahamu hivyo wapinzani tu ndio wenye viherehere vya kukata mrija wa pesa kwa "miungu watu".

2. Bomoa bomoa inayoendelea sasa jijini Dar es Salaam huku kukiwa na malalamiko lukuki lakini taasisi kubwa kama ikulu imekaa kimya.

Mengi yatajadiliwa lakini serikali ni kama baba wa wananchi. Ilipaswa kuwahamisha kiustaarabu na kuwaonesha mahala pa kujihifadhi lakini pia kwa kutumia njia ya majadiliano na ikibidi kuwalipa fidia wananchi.

Mwananchi kajena nyumba yake kwa miaka 5, serikali inakuja inatoa notice ya miezi mitatu au isitoe kabisa, je serikali ilikuwa usingizini wakati wote huo?

3. Kudhalilisha na kuwatisha watumishi wa umma. Tumeshuhudia ndani ya siku 60 watumishi wa umma wakinyimwa likizo, wakikataliwa kusafiri, wakisimamishwa kazi pasi na kufuata taratibu za kiutumishi wengine wakidhalilishwa mahakamani kwa kesi ambazo kwa nje kuna baadhi unajua serikali itashindwa.

Nieleweke wazi hapa, kwa mwananchi wa kawaida tunaona kama faraja kwetu watumishi wa umma wanavyodhalilishwa kwani tunaamini maisha yetu magumu yameletwa na uzembe wao.

Lakini ukifikiri kwa mapana utagundua kuna haja ya kuchunguza badala ya kudhalilisha watumishi kwenye media ili kujiongezea umaarufu wa kisiasa.

4. Siku ya usafi yaani 9 desemba. Kwa kufuata agizo lake nchi nzima ikajikuta ikiingia ktk zoezi hili kwa kulazimishwa, kweli watu walishika fagio wakaingia kufagia barabarani(na sio maeneo ya makazi) na matokeo yake pia taka zote zikatolewa kwenye mitaro na kuwekwa barabarani pasi na kuzolewa.

Haya ni matokeo ya kutoa maagizo ya kibabe, wananchi walitenda usafi kwa "agizo" na sio kwa kupewa elimu ya usafi na wakafanya huku wakijua faida za usafi.

5. Kubebana kwa wateule, hivi kuna mtu alitarajia January Makamba, William Lukuvi, na msururu wa makatibu wakuu kama wanaweza wakarudi tena ktk utawala?

Sawa, ni "maamuzi ya rais" na hakuna anayeweza kuyazuia.

Kwa mawazo yangu huru, kwa siku 60 sijajutia kumpa kura yangu Edward Lowassa, labda huko mbele. Tungoje.

Shukrani A. Ngonyani,
januari 5, 2016.
Tanga,
00255784379799,
sirngonyani@gmail.com
 
10987412_1547754618847857_4693284863880757177_n.jpg
HAHAHAHA WATU WA MABONDENI WENGI NDO WALIKUWA WANAPANDA , MAKALANDINGA KUZURURA NAYO KUSAKA UBWABWA SASA NDO SASA KIUKWELI WAO NDO WANAOISOMA NAMBA
 
NGONYANI TAMBUA TU KWAMBA WAKATI WA KULEA MAOVU UMEKWISHA. SASA NI UTEKELEZAJI WA SHERIA NA KUPIGA KAZI TU. WEWE PIGA SIASA KUWATETEA WAVAMIZI WA MAENEO YA WAZI NA MABONDE LAKINI MUDA HUO HAKUNA TENA. ANAYOFANYA RAIS WETU MPENDWA MH JPM LAZIMA TUYAUNGE MKONO NDIO MAANA HATA WENYE AKILI KAMA BABU YAKO MTEI WANAMKUBALI. HUYO ULIYEMTAKA TUMEMKATAA ASUBIRI 2025!

lakini inapaswa wasaidiwe japo ndo wakati wao wa kuisoma namba.
 
12279164_807943905980853_3260613062629581131_n-jpg.307523

Kwa upande wa bomoa bomoa, wananchi inabidi tufuate sheria, sehemu ambayo serikali imetoa taarifa/tangazo kuwa sehemu hii watu hawatakiwi kujenga basi tusijenge, tusilaumu tu serikali, maana serikali imezuia, imetoa taarifa, na imetoa muda kwa wale waliokaidi na kujenga eneo lile wahame bado watu wako pale, kwanini tusijifunze kutii amri pasipo kusukumwa? Dar es salaam kwa sasa unapoingia toka mwanzao hadi mwisho umekaa ki ajabu ajabu kwa ajiri ya hawa watu kujenga pasipo mpangilio na ovyo ovyo, mji hauna feelings kwamba naingia jiji la dar, largest city of tanzania , mji umekaa ovyo pasipo ramani, kwa hili mimi nasupport serikali.
 
Chadema kila siku wanaponda viongozi Wa ccm kuwa ni wabovu lkn cha kushangaza ukifika uchaguzi chadema haohao wanaazima wagombea ccm.!?!!

Mgombea wao alitoka ccm

Wabunge Wa viti maalumu chadema wameteuliwa kutoka ccm
 
NGONYANI TAMBUA TU KWAMBA WAKATI WA KULEA MAOVU UMEKWISHA. SASA NI UTEKELEZAJI WA SHERIA NA KUPIGA KAZI TU. WEWE PIGA SIASA KUWATETEA WAVAMIZI WA MAENEO YA WAZI NA MABONDE LAKINI MUDA HUO HAKUNA TENA. ANAYOFANYA RAIS WETU MPENDWA MH JPM LAZIMA TUYAUNGE MKONO NDIO MAANA HATA WENYE AKILI KAMA BABU YAKO MTEI WANAMKUBALI. HUYO ULIYEMTAKA TUMEMKATAA ASUBIRI 2025!
kichwa kiko empty kabisa
 
  • Thanks
Reactions: PNC
Hata mimi najua mabadiliko yatapatikana ndani ya ccm hilo kaa ukijua.
 
Ni kweli kwamba CCM iko madarakani kwa muda mrefu sana wamefanya mengi ya hovyo kuliko mazuri CCM imeleta UDINI, UFISADI, UPENDELEO na mengine mengi ya hovyo hovyo kabisa, lakini nani badala yake

Hatuwezi kutafuta mabadiliko kwa kutafuta Nafuu ili kufanya kundi lingine linufaike, Hapana
 
duh! umeandika kama mtu aliyekata tamaa vile.
 
Niwe tu muwazi, uwezo wa kufikiri umetofautiana sana, na uwezo wa kuchambua mambo na kuyawasilisha mbele ya watu pia tumetofautiana.

Nimetazama sana hizi siku 60 na ushee za mh. Rais Magufuli nimejikuta naanza kuendelea kuamini hakuna mabadiliko ya dhati yanayoweza kuletwa chini ya uongozi wa CCM.

Ndani ya siku 60 tu tumeshuhudia akifanya makosa ambayo ni "grave mistakes". Hebu tuyatazame kwa uchache.

1. CCM imeingia ktk uchaguzi mkuu ikiwa na harufu mbaya ya ESCROW, bunge likapitisha maazimio mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuwawajibisha watendaji na viongozi waandamizi waliohusika ambao wameteuliwa na rais, hapo ndipo prof. Mwijarubi Muhongo na bwana Eliakimu Maswi walitakiwa wawekwe kando.

Cha ajabu teuzi za mh. Magufuli amewarudisha hawa waliobariki wizi ule, hii inanipa dhana tatu.
(a)Huenda madai ya wapinzani wakati wa kampeni kuwa pesa ya Escrow zimekwenda kugharamia kampeni za CCM?
(b)Bunge kama muhimili wa dola umepoteza sifa na heshima yake, kwani hiyo ni dharau dhidi ya taasisi ya bunge.
(c)Hakuna wizi ambao unatendeka pasi na CCM kufahamu hivyo wapinzani tu ndio wenye viherehere vya kukata mrija wa pesa kwa "miungu watu".

2. Bomoa bomoa inayoendelea sasa jijini Dar es Salaam huku kukiwa na malalamiko lukuki lakini taasisi kubwa kama ikulu imekaa kimya.

Mengi yatajadiliwa lakini serikali ni kama baba wa wananchi. Ilipaswa kuwahamisha kiustaarabu na kuwaonesha mahala pa kujihifadhi lakini pia kwa kutumia njia ya majadiliano na ikibidi kuwalipa fidia wananchi.

Mwananchi kajena nyumba yake kwa miaka 5, serikali inakuja inatoa notice ya miezi mitatu au isitoe kabisa, je serikali ilikuwa usingizini wakati wote huo?

3. Kudhalilisha na kuwatisha watumishi wa umma. Tumeshuhudia ndani ya siku 60 watumishi wa umma wakinyimwa likizo, wakikataliwa kusafiri, wakisimamishwa kazi pasi na kufuata taratibu za kiutumishi wengine wakidhalilishwa mahakamani kwa kesi ambazo kwa nje kuna baadhi unajua serikali itashindwa.

Nieleweke wazi hapa, kwa mwananchi wa kawaida tunaona kama faraja kwetu watumishi wa umma wanavyodhalilishwa kwani tunaamini maisha yetu magumu yameletwa na uzembe wao.

Lakini ukifikiri kwa mapana utagundua kuna haja ya kuchunguza badala ya kudhalilisha watumishi kwenye media ili kujiongezea umaarufu wa kisiasa.

4. Siku ya usafi yaani 9 desemba. Kwa kufuata agizo lake nchi nzima ikajikuta ikiingia ktk zoezi hili kwa kulazimishwa, kweli watu walishika fagio wakaingia kufagia barabarani(na sio maeneo ya makazi) na matokeo yake pia taka zote zikatolewa kwenye mitaro na kuwekwa barabarani pasi na kuzolewa.

Haya ni matokeo ya kutoa maagizo ya kibabe, wananchi walitenda usafi kwa "agizo" na sio kwa kupewa elimu ya usafi na wakafanya huku wakijua faida za usafi.

5. Kubebana kwa wateule, hivi kuna mtu alitarajia January Makamba, William Lukuvi, na msururu wa makatibu wakuu kama wanaweza wakarudi tena ktk utawala?

Sawa, ni "maamuzi ya rais" na hakuna anayeweza kuyazuia.

Kwa mawazo yangu huru, kwa siku 60 sijajutia kumpa kura yangu Edward Lowassa, labda huko mbele. Tungoje.

Shukrani A. Ngonyani,
januari 5, 2016.
Tanga,
00255784379799,
sirngonyani@gmail.com
 
Mabadiliko yanaanza na wewe mwenyewe na wala si mtu mwingine yoyote
 
Back
Top Bottom