Kuna wanawake wanapenda ukweli; wabarikiwe sana

Kuna wanawake wanapenda ukweli; wabarikiwe sana

Innocent Kirumbuyo

JF-Expert Member
Joined
Jan 1, 2014
Posts
4,647
Reaction score
4,495
Kuna rafiki yangu mmoja ambae tulikutana kwa bahati na tukawa tunaishi mtaa mmoja Tabora,alikuwa ni mtu ambae aliishi kwa mateso sana katika mapenzi.Maana alikuwa na uhusiano na mschana mmoja aliyekuwa mwanafunzi katika chuo cha ualimu, si mnajua kwenye kutongozana huwa tunaulizana kuhusu kazi,sasa jamaa yangu alikuwa hana kazi ila akadanganya ni mwalimu wa secondary ili ampate binti kirahisi. Mapenzi yalianza vizuri kwenye simu,ikafikia hatua binti anataka kuja kumtembelea jamaa.jamaa akiangalia hana kazi ya maana bali alikuwa ana kibarua kwa wale jamaa wauzaji wa sabuni,dawa za meno,sijui vioo wale waongo kabisa ambao hudanganya kuwa sabuni ya kuongeza hamu ya kuoga.ndiko alikokuwa jamaa yangu.

Sasa shida ikazidi pale binti alipokuja kumtembelea jamaa,kiukweli kwa muonekano wa jamaa na mavazi yake hata kama ni mimi ndio ningekuwa binti ilikuwa vigumu sana kugundua kuwa jamaa hana kazi.Basi jamaa alipopigiwa simu na binti kuwa yupo njiani anakuja jamaa akafanya maandalizi akanunua box la chaki na akatafuta mavitabu ya uongo na kweli ili kuendeleza uongo wake.Binti akafika salama na maisha yakaanza,maana binti alidai atakaa wiki moja kisha arudi chuo.

Sasa shida ikawa kwa jamaa maana kazi yake ya uuzaji sabuni na mafuta haina Jumamosi wala jumapili,lakini kwa kuwa alidanganya ni mwalimu ilibidi Jumamosi na Jumapili apumzike nyumbani.lakini hizo siku nyingine alikuwa anaamka asubuhi anabeba mavitabu yake na chaki kisha anamuaga binti wa watu kuwa anaelekea shule,kumbe anaenda kufundisha watu jinsi ya kutumia sabuni za kuondoa chunusi.Mungu akamjalia ndani ya ile wiki hakujulikana kuwa ni muongo kwa binti yule,na binti akarudi chuoni salama.Lakini kumbe katika harakati zile binti alichukua ujauzito na hii ndio ikawa tabu kubwa kuliko.maana jamaa kwa zile siku 2 Jumamosi na Jumapili ambazo hakwenda kuuza sabuni Jumatatu alipokwenda alikuta kazi imepata mtu mwingine.hivyo akawa mtaani bila kazi,wakati binti anawaza jinsi watakavyoishi na mumewe wote wakiwa waalimu,

Jamaa anawaza siku akija kugundulika kuwa hana kazi ila mimi baada ya hapo nilitoka Tanzania na niliporudi nilikuta walikwisha kuoana na wana mtoto mmoja,mwanamke mwalimu,mwanaume kawa mkulima na nilipomuuliza jamaa kuwa siku alivyogundulika ilikuwaje,yeye alidai kuwa hatawahi kuona aibu tena kama aliyoiona siku hiyo.

Funzo kwa vijana sio mpaka utumie uongo kumpata mwanamke jaribu kuwa mkweli na kuweka wazi maisha yako kwa yule umpendae.

Funzo kwa waschana msipende kudanganywa maana kuna wanawake wengine hulazimisha wanaume wawadanganye.kuna mmoja nilikuwa nachat nae akaniuliza uko wapi? Nikamjibu nipo Rwanda, akauliza Rwanda unafanya? Nikamjibu nafanya kazi,akauliza kazi gani? Mimi sikumjibu ila nikamtumia picha nashona viatu akanibrock hadi leo.
 
Bila huo uongo inawezekana asingempata uyo dada. Sometimes uongo unalipa ila usiwe too much
 
Sasa mkuu huoni hapo pana faida kuwadanganya alafu ukweli waje kuujua mbeleni huko

Angemwambiaga hana kazi naamini asilimia 98% mwanamke angemkataaga
 
wanasema kuna uongo mzuri
hebu twende na huo uongo mzuri unatusaidia kuwapata hawa

nina kisa hicho cha uongo kwa hawa mademu dahh huwa nacheka sana
Mo ww una asili ya uongo tuu[emoji14][emoji14]
 
Akuna mwanaume anapenda kudanganywa ata siku moja
basi ni hivyo hivyo hakuna mwanadam anayependa kudanganywa kamwe..labda uwe ukimdanganya asijue akijua lolote laweza tokea kulingana na jinsi ulivyomtumia katika huo ulaghai
 
basi ni hivyo hivyo hakuna mwanadam anayependa kudanganywa kamwe..labda uwe ukimdanganya asijue akijua lolote laweza tokea kulingana na jinsi ulivyomtumia katika huo ulaghai
Mwanamke anapenda kudanganywa
 
Kati ya vitu ambavyo sivipendi kwenye masuala haya ya mahusiano ni "KUDANGANYA[UWONGO]" kwann usiwe mkweli tu tena ukiwa mkweli ni rahisi sana kumgundua mwenye mapenzi ya dhati na mwenye mapenzi ya kinafiki.
hakuna kitu kizuri kwenye mahusiano kama kuwa mkweli na muwazi kwani vitakuweka huru na kukufanya uishi kwa amani na furaha.
 
People like to be lied a bit, rarely do they like to hear the truth. They might say they do, but they don't really mean it!

Maisha ya mahusiano bila uongo wa hapa na pale, hayaendi.
 
Back
Top Bottom