Kuna wakati Dunia yote itakaa kwa amani bila vita?

Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
269,634
697,916
Kwa wengi wasiofahamu vita ni biashara moja kubwa sana, biashara ya silaha na kuna baadhi ya mataifa uchumi wao unategemea silaha, kukiwa na amani silaha haziuziki kivile.

Kwa wasiojua, vita ni namna ya kupimana ubavu; nani ana silaha gani kali zaidi, nani ana mbinu bora zaidi nani ana jeshi mahiri zaidi.

Kwa wasiojua vita ni sehemu ya kufanyia makaribio ya silaha mpya; uwezo wa kuharibu na kuangamiza kwa haraka na kasi zaidi, uwezo wa mwendokasi, uwezo wa kukwepa mitego na vizuizi vya adui na uwezo wa kutoonekana kwenye rada za adui.

Kwa wasiojua vita ni njia ya kupenyeza agenda za siri, uporaji, kujenga mahusiano, kafarakanisha kwa malengo maalum nk. Vita ni kamari na kwa baadhi michezo ya kufurahisha kwa baadhi.

Vita ni ajira na maokoto, vita ni biashara nje ya silaha, vita ni mtandao wa kufanikisha mengi ambayo hayawezi kufanikiwa bila vita.

Kwa sehemu kubwa huwa kinachoripotiwa kwenye uwanja wa vita ukweli na uhalisia huwa chini ya asilimia 60! Kuna uongo na propaganda za kila aina.

Vyombo vinavyoripoti vita husika huripoti kulingana na mapenzi binafsi, nani mmiliki, nani mfadhili nk.

Wanadamu wanachonganishwa kwa maslahi ya wengine, wanafarakanishwa kwa agenda za siri za wengine, wanatumika kama kipimo cha kuhimili sumu kupitia madhara ya sumu za silaha vitani!

Kwa haya machache na mengine ambayo sijayaandika hapa ni wazi vita haitakaa ikome duniani.

Tujiandae kwakuwa hatujui watagombanishwa kina nani tena!
 
haiwezekani kwa maana vita= money, kuna documentary itafute kama ukipenda youtube inaitwa “all wars are bankers wars”, mara nyingi sababu wanazitoa za vita hazina uhusiano wowote na ukweli, jiulize nchi masikini wanapata wapi fedha za kununulia silaha? Hizo silaha wanazitoa wapi?
 
Pia chanzo Cha vita ni shetani ili kupata damu nyingi kwa wingi
4416c9c68074ead443718d70406de292.jpg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
2025 kitanukaaa believe me....
Watz wamechoka wanasubir mfadhiri tu kiwake mim nipo mstar wa mbele kuingia msistuniiiiiiiiiijiiiii..........
 
Kwa wengi wasiofahamu vita ni biashara moja kubwa sana, biashara ya silaha na kuna baadhi ya mataifa uchumi wao unategemea silaha, kukiwa na amani silaha haziuziki kivile.

Kwa wasiojua, vita ni namna ya kupimana ubavu; nani ana silaha gani kali zaidi, nani ana mbinu bora zaidi nani ana jeshi mahiri zaidi.

Kwa wasiojua vita ni sehemu ya kufanyia makaribio ya silaha mpya; uwezo wa kuharibu na kuangamiza kwa haraka na kasi zaidi, uwezo wa mwendokasi, uwezo wa kukwepa mitego na vizuizi vya adui na uwezo wa kutoonekana kwenye rada za adui.

Kwa wasiojua vita ni njia ya kupenyeza agenda za siri, uporaji, kujenga mahusiano, kafarakanisha kwa malengo maalum nk. Vita ni kamari na kwa baadhi michezo ya kufurahisha kwa baadhi.

Vita ni ajira na maokoto, vita ni biashara nje ya silaha, vita ni mtandao wa kufanikisha mengi ambayo hayawezi kufanikiwa bila vita.

Kwa sehemu kubwa huwa kinachoripotiwa kwenye uwanja wa vita ukweli na uhalisia huwa chini ya asilimia 60! Kuna uongo na propaganda za kila aina.

Vyombo vinavyoripoti vita husika huripoti kulingana na mapenzi binafsi, nani mmiliki, nani mfadhili nk.

Wanadamu wanachonganishwa kwa maslahi ya wengine, wanafarakanishwa kwa agenda za siri za wengine, wanatumika kama kipimo cha kuhimili sumu kupitia madhara ya sumu za silaha vitani!

Kwa haya machache na mengine ambayo sijayaandika hapa ni wazi vita haitakaa ikome duniani.

Tujiandae kwakuwa hatujui watagombanishwa kina nani tena!
Imani itapatikana pale tu kutakapokuwa hakuna dini inayoamini kumuuwa mwingine kunakufikisha kwa Mungu.
 
Back
Top Bottom