Kuna wadada wakija ghetto wanachukua kitu chochote cha kwenda kuturogea. Nimefunga camera wameanza kuumbuka vibaya kabla hawajaondoka najisanua

Wadiz

JF-Expert Member
Nov 10, 2022
5,411
11,061
Wasalaam,

Nawakumbusha tena camera ambazo ni ngumu mtu kujua zimejaa tele , kuondokana na hii vita ya wadada ama wanawake kuwa na mpango wa kuturogea kimapenzi. Mimi najisanua kila mara nawaumbua, mpaka sasa wengi wanashangaa maana hakuna dalili za kuona camera popote pale, kamanda nimefunga nimeunganisha kwenye simu yangu.

Nawashukuru sana wanasayansi wenzangu kwa hili. Camera ni mkombozi mbali na hilo nina machale mwili unasisimka nikiwa na demu mwenye hila, akiwa anawaza hila tu nywele husimama. Sasa na huyu mzungu camera ndio nimeua walakini.

Ukiwa kaksi shida ukiwa na roho nzuri wanakuona fala na bwege, sasa potelea mbali maisha ni roho mbaya na ukaksi basi.

Tumieni hizi camera kuwaepuka hawa wanawake wachawi.

Ni hayo tu

Shukrani 🙏🙏🙏

Wadiz
 
Kuna sehemu nilkuta kitunguu kama kina shida, nikapata udadisi. Kukiangalia vizuri, nikakuta kimekatwa katikati halafu kimechomekwa karatasi na kimeingiziwa sindano(hizi za kushonea kwa mkono).

Nikachomoa karatasi. Nikakuta imeandikwa jina la mtu(me).. nikachana ile karatasi na sindano nikatupa.

Bila shaka jamaa atakuwa ameponea chupuchupu.
 
Ukiona hivo wambie hata wasipate tabu wape condom yenye shahawa zako kabisa wakaroge vizuri uchawi hauendi kwa mentali
 
Yaani hili jambo ndo linanifanya nisiwe na demu from African countries ulozi mwingi sana mpaka kero hata hao ma church girl ni hivyo hivyo sijui shida ni nn.

Saivi ni kutafuta wazungu tu hamna namna.

Wabongo wamenishinda asee.
 
Mna shida sana watu ambao mnaamini habari za uchawi pole sana mtaishi maisha ya hofu mpaka siku mtakayokufa ndo hapohapo mtagundua kumbe hakunaga uchawi kila kitu kinaendeshwa na nature aliyo create Mungu na kwamba hakuna binadam anaweza kuingilia aka twist lolote kwa nguvu za giza....yaani kwa nguvu isiyonekana...
 
Back
Top Bottom