The Tomorrow People
JF-Expert Member
- Jul 11, 2013
- 2,662
- 2,745
Ninapenda kuchukua fursa hii kuwakumbusha wabunge kuwa zama za kutaka kujikweza na kuitwa "WAHESHIMIWA" wakati wanafanya mambo ya kipumbavu mbele ya macho ya wananchi wa Tanzania zimepitwa na wakati.
Ninaandika makala hii ili Watanzania wenzangu na hata baadhi ya wabunge mtakaoipata makala hii "muifoward" hadi iwafikie walengwa. Sioni haya kusema bunge la 11 lina wabunge wa aina mbili, yaani wabunge wenye busara na Wabunge "Malofa na wapumbavu" na wasio na busara. Hii inatokana na sababu zifuatazo:-
Utamaduni uliojengeka wa kusimama na kuzomea, kupiga mayowe unadhalilisha hadhi ya bunge na hata kama unaofanywa Nchi nyingine sio wa kuigwa maana hauna tija kwa jamii. Juzi katika mchakato wa kupata Naibu Spika tulishuhudia wabunge wakisimama na kupiga mayowe, Kubweka na kubwabwaja Ovyo kuzuia usikivu na utulivu. Hali hiyo ilizuia usikivu na kutunyima uhondo wa kusikia majibu ya maswali mazito toka kwa Mh. Silinde kwenda kwa Dr. Tulia.
Lakini pia wakati ndg Nape Nnauye ana uliza swali kwa mgombea u Spika wa UKAWA ndg. Ole Medeye wabunge wengine bila sababu walianza kupayuka kama walevi na kubwatuka Ovyo kuzuia Ole Medeye asijibu maswali. Hizo ni tabia za kihuni, Kipuuzi na kijinga.
Jambo lilioonyesha kiwango cha juu cha upumbavu wa baadhi ya wabunge ni baada ya Jana kutoka Bungeni tena kwa kufanya fujo. Ninasema ni upumbavu bila kuona haya ili mjue kuwa hatuna sababu ya kuheshumu na kufumbia macho tabia za kihuni kama zile.
Ni wazi kuwa wananchi tumewachagua ili mtuwakilishe na kutetea maslahi Yetu na wala sio kuleta ushabiki wa vyama vyenu.Pia mkumbuke kuwa hatukuwachagua kwa kuwa nyinyi mpo peke yenu katika jamii.
Wananchi tusimame kidete kukemea mambo mawili. La kwanza tukemee utovu wa nidhamu wa kuzomea Ovyo na utaratibu mbovu wa "Ndiyo Mzee"...
Kwa Leo naishia hapa.