UKAWA imeingiza mambo ya vyama vyao Bungeni kwa kuamini kuwa ndio mahala pekee pa kushawishi viongozi wa kitaifa. Ni nidhamu mbaya sana kumzomea mtu aliye kuzidi umri, achilia mbali mtu huyo kuwa kiongozi wa taifa ama lah. Hivyo kitu ambacho UKAWA walikifanya jama akisameheki, akivumiliki na wote wenye akili tumekilaani kile kitendo cha kuzomea Bungeni.
Mkuu HAMY-D;
Mbona unaufuata ule msemo wa kwetu; Nyani haoni kundule?? Katika maono yako, ni nani kati ya UKAWA na CCM wanaleta mambo yao mle bungeni?
Nakuomba uwe mkweli tu mkuu:
Unaunga mkono Dr Shein na mwenzake Kificho kuingia mle bungeni kwa nyadhifa walizo ingia nazo?? Naomba tu uwe mkweli. Hata mtoto wa darasa la nne anajua wazi kuwa Zanziba kuna mgogoro wa kisiasa. Mh. rais amekiri kuwa kuna "Majaribu ya kisiasa kule zenj"
Jiulize swali; Kumuingiza Dr na Kificho bungeni, kwenye bunge la JMT ndio kuyamaliza hayo majaribu ya kisiasa au kuyakuza?
Nadhani, endapo utayajibu kiufasaha hayo maswali, utaunga mkono UKAWA kutoka nje. Hawana njia nyingine kuelezea hisia zao baada ya weye kuunga mkono Spika aikanyage katiba