PRODA LTD
JF-Expert Member
- Oct 20, 2016
- 1,005
- 1,333
Wanabodi,
Kuna vurugu kubwa maeneo ya stend ndogo Arusha Jiji la Arusha, vurugu hizi zimesababishwa na hatua ya Mkurugenzi wa Jiji la Arusha kutoa barua za kuwapa vibanda madalali ambao hawafanyi biashara. Mgogoro huu ambao umchukua sura mpya ikiwa ni pamoja na tuhuma za hao madalali kutoa rushwa kubwa kwa RC na Mkurugenzi ili wapendelewe.
Awali ilikubaliwa na baraza la madiwani kuwa utaratibu wa zabuni tena zabuni ya wazi ili kuondoa upendeleo. Zabuni hiyo imetolewa kwenye maeneo mengine yote kasoro stend ndogo tu. Kwanini RC na Mkurugenzi hawataki tena zabuni ambayo wao ndio walipendekeza? Nini hatima ya walionunua hiyo tenda kila mtu alilipa 50,000, tenda haijafika mwisho Mkurugenzi anatoa barua kwa watu wachache.
Tayari maduka yote yamefungwa kufuatia hofu ya vurugu!
Viongozi wa juu ingilieni huu mzozo,
Ni mimi mfanyiabishara
==============UPDATES
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo ameliagiza Jeshi la Polisi kufika eneo la stand ambapo muda magari zaidi ya matatu yakiwa yamejaa polisi yamefika maeneo stand ndogo