Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 34,175
- 43,935
Kwa vile serikali ya CCM imeamua mtindo wa kubinafsisha huduma muhimu tumeona hivi karibuni wakibinafsisha shughuli za usalama kwa Majembe Auction Mart na kwa muda mrefu wamebinafsisha hata shughuli za uokoaji na kupambana na moto. Hili limekuja baada ya kubinafsisha shughuli za ulinzi wa Polisi kwa kuruhusu uwepo wa vikampuni binafsi vya polisi (private police companies).
Tumeona upungufu wa mkakati huu kwenye majanga yanayoendelea ya mvua ya Krismasi (kama nilivyodokeza, tukiwa mtandao wa kwanza kuripoti juu ya mvua hiyo masaa 12 kabla ya vyombo vya habari vya Tanzania havijarukia).
Tumeonesha kwenye suala la hospitali ya Temeke na sasa najiuliza kwenye kupambana na majanga ya moto, je serikali ya CCM itaendelea mpaka lini kubinafsisha usalama wa maisha ya watu wetu? Mpaka wapi kuungue ndio tutajua kuwa huwezi kuwa na jiji la kisasa bila ya huduma ya kisasa ya kupambana na mojawapo ya majanga ya kawaida kabisa kutokea yaani moto?
- Ilipoungua Ikulu hatukujifunza?
- Ilipoungua Benki Kuu hatukujifunza
- Ilipoungua Nasaco hatukujifunza
Nadhani umeng'amua kuwa nia ya msingi ya kubinafsisha huduma zote za muhimu namna hiyo, ni kujinufaisha binafsi kwa wachache wenye dhamana za idara na wizara husika. Taifa zima linaangamizwa kutokana na kiu ya fedha chafu za kikundi fulani cha manyang'au wachache.
Hizo fedha wanazopata wala hazitawatosha. lakini kitakachowakumba mwishoni ni AIBU!
Wanatembelea nchi za wengine kushangaa, lakini hakuna wanalojifunza!
AIBU yao milele!
Nadhani viko viwili vya jiji. Kimoja kiko faya na kingine Temeke. Kuna vikosi vya zimamoto uwanja wa ndege na bandari.
Amandla......
hapa hoja sio VITUO VINGAPI VYA FIRE!.....hoja ni kwanin hivi vituo haviko active?....
imewahi tokea mikocheni hapo LIMOZIN inawaka moto ajabu,lilikuja gari la faya pale kwa mwendo mkali kweli kweli...!kufika pale HALINA MAJI!.......
WTF
hapa hoja sio VITUO VINGAPI VYA FIRE!.....hoja ni kwanin hivi vituo haviko active?....
imewahi tokea mikocheni hapo LIMOZIN inawaka moto ajabu,lilikuja gari la faya pale kwa mwendo mkali kweli kweli...!kufika pale HALINA MAJI!.......
WTF
hapa hoja sio VITUO VINGAPI VYA FIRE!.....hoja ni kwanin hivi vituo haviko active?....
imewahi tokea mikocheni hapo LIMOZIN inawaka moto ajabu,lilikuja gari la faya pale kwa mwendo mkali kweli kweli...!kufika pale HALINA MAJI!.......
WTF
Geoff hii hoja nilishaisikia mara nyingi tu mara magari yamekuja na hayana maji au maji hayatoshi hivi huwa ni kweli? Hivi dereva wa gari hilo anapolitoa spid toka kituoni kwenda eneo la tukio haangalii kama kuna maji au la? anakwenda kufanya nini sasa eneo la tukio amekuwa mwandishi wa habari ambaye hata yeye ana afadhali maana hukumbuka kamera yake au kalamu yake ya uandishi.
Mimi siamini kama serikali inashindwa kutatua tatizo hili nali tu ule utayari haupo. Kama tunaweza kuruhusu ujenzi wa nyumba za mabilioni, kesi za EPA e.tc. serikali inashindwa kweli kuturubuni kwa kiini macho cha fire??
On the same infrastructure tip...vipi zile sehemu ambako watu wamejenga kiholela holela? Maana kuna sehemu kama pale Tabata, Ubungo, au hata mitaa ya Tangi bovu ambako hakuna njia hata gari na hata baiskeli na pikipiki hazifiki. Kuna nyumba na sehemu za starehe (baa na migahawa) zinazofikika kwa miguu tu. Huko kukitokea moto itakuwaje?
Hata kama Dar ina watu milioni kadhaa (who knows idadi kamili) kwa nini iwe Dar tu? Lindi na Mafia kuna vituo vingapi vya zimamoto na EMS? Au huko hakuna watu wanaoweza kuungua na moto?