Kuna Viboko kumfanya mtoto aelewe na Kuna Viboko kumpa mtoto Nidhamu!

Adhabu ya viboko kwa watoto ni barbaric na mojawapo ya adhabu za hovyo sana katika karne ya 21.
Ww mtoto wako huwa akikosea huwa unampa hadhabu gani akosea nje ya viboko au bado hujazaa?
 

Kama ulishawahi kupendwa katika maisha yako na Wazazi/Mlezi huwezi kuthubutu kumfanyia ukatili mtoto wako mwenyewe damu yako, ni sawa na Mwanamke ambaye ameolewa anapigwa kila na Mume wake lkn bado anarudi na kumtetea mtesi wake, hiyo ni psychological problem, kama ulipendwa na kukulia maisha ya amani na furaha utajua upendo ni nini lkn kama ulikosa upendo ni ngumu kujua na ndio maana kwako unaona ni kawaida kutesa mtoto wako damu yako mwenyewe!
 
Mi naona mwalimu ashughulikie taaluma ya mtoto, maswala ya nidhamu amwachie mzazi.

Kama mikono inawasha akachape watoto wake
 
Matokeo ya viboko ni tumepata taifa la hovyo. Taifa la watu waoga ambao hawawajibiki mpaka kuwe na adhabu. Watu ambao kwao hakuna jambo baya, ila ubaya ni kukamatwa na kuadhibiwa.
 
Viboko Ni muhimu Sana kwa wanafunzi jitu zima liko lasaba halijui horoza hata Kwanza Hadi ya hata tano

Bila fimbo huu Ni mwanafunzi kweli

Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
 
Umeonges Busara Sanaa

Inawezekana yeye watoto wake, wakikosa anawafanyia sherehe
 
Laiti watunga Sera na Viongozi wote (Serikali +Dini zote + Wanasiasa) wangezingatia hayo uliyoshauri hapa, tungefanikiwa pakubwa sana. Ubarikiwe sana kwa andiko hili.
 
Kwa hiyo ww ukikosea serikali ikakufunga inakuwa imekufanyia ukatiri na sio kulipia makosa uliyo yafanya?

Adhabu na ukatiri vina husiana nn? Ukatiri kwa mtoto utafisirika pale utakapo mpa adhabu kubwa na isiyo endana na umri wake na kosa lake.
Kwani mtoto akikosea ukachukua kafimbo kadogo ukamcharaza tuviboko tutatu huyo mtoto atapungukiwa na nn?


Huwezi kusema una upendo kwa mtoto alafu awe anafanya mambo ya kumpoteza alafu unamuacha kwa kigezo cha eti kupiga mtoto ni ukatiri.

Nimekuuliza swali hujanijibu ww mtoto wako huwa akikosea huwa unamuita na kumpongeza na kufanyia sherehe?
 
Hii nimeipenda na ndio ukweli. "Hao hao walio sema kuwa kupiga mtoto ni ukatiri ndo hao hao walio sema kufanya ushoga na kutoa mimba ni halali."
Na wapo wanaotumia msemo wa vijiweni........"Hapendwi mtu hapa........"
 

Kwa nini umpe mtoto adhabu? Hiyo ni psychopathy, hilo la Serikali kutoa adhabu ni kwa criminals sidhani kama unataka kumfananisha mtoto wako damu yako na criminals ambao wanafungwa na Serikali ili kuprotect jamii.

Kama umelelewa kwa upendo na amani huwezi mpa adhabu mtoto damu yako, hiyo wording peke yake kwamba adhabu inaonyesho ukosekano wa upendo!
 
Sidhani uko sahihi sana mkuu. Mwanao unamleaje?Unamlea peke yako? Mtoto unayempenda kwa kawaida mzazi huwa unatamani kwamba hapo baadaye ajekuwa ni mtu wa namna fulani ndani ya Jamii. Upendo ni pamoja na kumrudi (kumpa adhabu) ili ajitambue kwamba alichofanya sio kitu chema au kizuri. Zipo njia nyingi za kumfundisha atambue mambo mema na mabaya. Wewe kama mzazi utatamani aache na kuepuka yale mabaya na azingatie kutenda yale mema siku zote na mwishowe hiyo ijijenge kwake na iwe ndio tabia yake.
Je, labda mwanao anaanza mazoea ambayo baadaye inaweza kuja kuwa ni tabia kwa kuanza kidogo-kidogo kuiba sukari nyumbani au kwenda kwa majirani na kujichukulia bila kuomba e.g. maembe au chochote anachokitamani. Kweli ww utambembeleza? Ukimkataza hasikii anarudia na wakati mwingine ukimwita ili kumuonya anakimbia. Utamchekea tuu?
Kwa kufanya hivyo ww ndo utakuwa unaonesha una tatizo la Psychopathy kwani hata jamii unamoishi hawatakuelewa yaani huendani na mfumo uliopo wa kijamii (ww uko kinyume) ambapo watoto wanalelewa kwa kila aina ya mbinu inayokubalika. Kumbuka mtoto ni wako kwa kuzaa lakini kijamii ni mtoto atakayelelewa na Jamii nzima ili hatimaye aweze kukubalika ndani ya jamii mahalia. Mtoto mtukutu, mtundu, mwizi, mjeuri na asiye na adabu huwa ni aibu na fedheha kwa wazazi wake na huwa ni chukizo/kero ndani ya jamii na lawama huenda kwa wazazi kwamba wazazi wameshindwa kumlea. Je, utauficha wapi uso wako ikiwa Jamii nzima inakunyoshea kidole? Usidhani kwamba utadumu daima na mwanao huyo unayempeti-peti.
 
Hoja zako ni nzuri,,but bado fimbo haiwezi kuwa solution kwa karne hii.
Ni kweli fimbo haiwezi kuwa solution kwa karne hii bali ni mojawapo kati ya mbinu nyingi zinazoweza kutumika ili kufikia lengo.
 
Hoja hii "Adhabu na ukatiri vina husiana nn? Ukatiri kwa mtoto utafisirika pale utakapo mpa adhabu kubwa na isiyo endana na umri wake na kosa lake.
Kwani mtoto akikosea ukachukua kafimbo kadogo ukamcharaza tuviboko tutatu huyo mtoto atapungukiwa na nn?"
Ni hoja yenye mashiko
Hiyo ndo Hekima na Busara ya Mzazi anayempenda mwanaye. Hongera mkuu.
 
Mi naona mwalimu ashughulikie taaluma ya mtoto, maswala ya nidhamu amwachie mzazi.

Kama mikono inawasha akachape watoto wake
Hapo hapo kwenye kushughulikia Taaluma, Kuna wanafunzi bila kutumia Viboko, hawaelewi kabisa .

Wangapi Leo hii tunawakumbuka wale Walimu walikua wakali enzi zetu tunasoma naleo tunawakumbuka Kwa kutufanya tuwe Bora na wenye Thaman?.
 
Alafu Ukatili na Utoaji adhabu ni vitu viwili tofauti.


Mwanadam anapokosea nilazima ajutishwe kupitia Adhabu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…