A
Anonymous
Guest
Wagonjwa na ndugu zao wanaingizwa gharama za ziada zisizo na ulazima. Mgonjwa wangu ametoka kanda ya ziwa amefika Muhimbili wiki 2 zilizopita, hadi leo hakuna huduma yoyote ya kibingwa aliyopatiwa. Jumatatu ya wiki ya kwanza wakasema kuna vipimo atafanyiwa na pia madaktari watafanya kikao waone watampa huduma gani, wiki ikaisha.
Wiki iliyopita ambayo ni ya pili wakasema hawajaamua cha kufanya kwakua kuna Daktari hayupo hivyo asubiri Jumatatu ya leo ambayo inakua ni wiki ya 3, tumesubiri inafika leo wanasema inabidi akafanye X Ray kisha majibu yake yatajadiliwa wiki ijayo, yaani wiki ya 4.
Sasa hapa unajiuliza hizi wiki zote 3 hizi gharama ndugu tunaingia ni nini? Je ni kweli walishindwa kumuandikia X ray ile wiki ya kwanza? Na je hawawezi andika vipimo vyote mgonjwa akafanyiwa katika wiki ya kwanza? Au wanatengeneza mazingira ya rushwa?
Mbaya zaidi ni kuwa hakuna mifumo mizuri ya kutatu hizi shida pale.
Tunaomba tusaidiwe