Uchaguzi 2020 Kuna uwezekano wa nchi hizi zikatumika katika kudukua Mfumo wa Uchaguzi. Intel za Serikali kuweni macho

Kejuu

JF-Expert Member
May 20, 2020
645
906
Ndugu zangu,

Napenda kumshukuru Mungu kwa kutupa uhai na kutufanya tuione siku ya leo.

Kuna jambo moja hapa nalileta kwenu wadau ili tulifanyie analysis kwa pamoja, ambalo linamhusu huyu dogo, I think you understand whom I'm referring to. Dogo kasema kazunguka sana katika nchi za Ulaya na Marekani, naamini nia ni moja tu kupambana ili ajaribu kuingia Ikulu kwa nguzu za haya mataifa niliyoyataja. Na hiki ndo kinachompa jeuri na kiburi cha kuongea kwa kulipuka lipuka na inampelekea kupoteza hata focus.

Hakuna mtu asiyejua kazi kubwa na adhimu ambayo Mhe. Rais amelifanyia taifa hili kwa kipindi cha miaka hii mitano katika kulinda rasilimali zake, kusimamia miradi mikubwa ya nchi mpaka Afrika na ulimwengu mzima umebaki kuduwaa, na amekuwa role mode kwa nchi nyingi za Africa.

Kwa namna ninavyozijua hizi nchi, misimamo ya Mh. Rais, ni mwiba mkubwa sana kwa jamaa hawa, kwasababu huwa hawataki kuona nchi za Kiafrika zinakuwa na viongozi imara, mfano Libya as our case study.

Kuna uwezekano dogo akatumia nchi zifuatazo:
  1. Baadhi ya nchi za EU
  2. Marekani
  3. Kenya
Hakuna mtu asiyejua aliyekuwa kaimu balozi wa Marekani alivyokuwa na chuki na nchi yetu. Kama ukijaribu kukonect dots, tayari Marekani imetambulisha balozi mpya hivi karibuni katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi mkuu, nani ajuaye kama huyu ndugu ana maelekezo kutoka juu, na tayari yuko na mission fulani ambayo dogo atakuwa anaijua.

Kwanini Kenya? Wenye kumbukumbu mtakumbuka, serikali ya Kenyata walikuwa marafiki na Chadema, hata Lowasa aliwahi kwenda kuipigia kampeni kule Kenya, Mh. Magufuli alikuwa pro Odinga. Nikukumbushe tena, kwa kasi hii ambayo Tanzania inakua kiuchumi chini ya uongozi IMARA NA MADHUBIUTI wa Mh. Raisi mpaka nchi imeingia kwenye uchumi wa kati, usidhani hii inawapendeza wakenya walivyo na wivu vile kwa nchi yetu.

Kwa kusema hivyo, kunauwezekano wa Kenya kutumika kwa ajili ya kuingilia mfumo kuhesabu kura ili kujaribu kumsaidia dogo kuingia Ikulu, japo hili litakuwa ni ndoto ya mchana kwake. Kuna possibilities hili linaweza kuwa linajulikana na intel za Tz, just my speculations.

Accordingly, ukijaribu kukonect dots tena, ile issue ya ndege ya delegations wa Kenya kushindwa kuja kupay tributes kwa msiba wa Mh. hayati Ben, huku kukawa na two contradiction reasons kwa nchi hizi mbili: hali mbaya ya hewa (Tz) vs technical problem (Ke), there might be something at odds for these two superpower in EA region, which could be attributed to my argument.

Namalizia na kusema, dogo ashakuwa kibaraka PERIOD. Watanzania wazalendo popote pale mlipo, tuiombeeni sana nchi yetu isije kibaraka huyu akatumika kuivuruga nchi yetu.

Asante,
Nawasilisha
Kejuu
 
Kejuu,

Ungejitahidi ukaandika kingereza kilichonyooka au kiswahili pekeyake kilichonyooka mkuu

Hata hivyo uchaguzi wa mwaka huu pamoja na kwamba utakua na mazonge mengi bado sijaona mwenye ubavu wa kupimana na JPM

Hata TL, BM wangepata msaada wa kutoka NATO yote JPM ni lazima amalizie muhula wake

Tutarudi hapa November kukumbushana(Sio utabiri) ni hali halisi
 
Unaweza ukawa umeonambali, tahadhari ni kwamba hoja hizi zisitumike kuthibitisha wizi wa kura.Lakini pia kiongozi mkuu pamoja na mema yote aliyoyafanya kashindwa kutengeneza umoja wa kitaifa na ndio maana itawawia rahisi vibaraka kutuingilia
 
Hata mimi nimesikia hilo kupitia rafiki yangu anae inshi miongoni wa nchi za jumuiya ya Ulaya
 
Kweli waliosema mara mia mtu mjinga kuliko mpumbavu hawakukosea,nchi zetu za afrika mifumo yote tunayoitumia imetengenezwa na hao USA pamoja na nchi za ulaya sasa hizo intel inazozisema zimetengenezwa na Mtanzania?

Huyo USA akitaka hata ww ndio uwe rais hata kabla ya kesho kutwa inawezekana kwa 100%.
Acha utahira siku nyingine andika vitu vya maana.tafakari kabla hujaandika.
 
Kejuu,

Tanzania chini ya CCM ndo kinara wa ukombozi wa nchi za Afrika dhidi ya mabeberu! TL na vibaraka wake subiri tar 28 tutawaonyesha, walai wakipata kura zaidi ya asilimia 10 wakatambikie! Tunawachinja kwenye sanduku mapema kabisa!
 
Kejuu,

Ukishaumwa na nyoka, ukisikia sauti ya unyasi tu unashtuka. Hoja hujibiwa kwa hoja, haitajiki siasa rahisi rahisi, bali jukwaa sawa la kuendesha siasa za kistaarabu.
 
Kejuu,

Mkuu binadam tumeumbwa kuwaza na wenda umewaza vizuri ila pamoja na mawazo yako mkuu dawa ni moja tu ccm wajipange tu kwamba kwenye vituo kura zihesabike kwa uwazi then si watakua na hard copy amabazo watazijumlisha kwa nchi nzima na ambazo kila wakala wa chama atakua amesaini.

So ikitokea mfumo ukaingiliwa basi hard copy zitatumika na hapa kwa kweli hatutaki chama chochote kuonewa iwe ccm au vyama pinzani tunataka alieshindwa au kushinda basi iwe halali, basi cha msingi huko kwenye vituo kura ziehesabike kwa uwazi na hizo ndo zitumwe kwenye mfumo na namheshim sana JPM ni matumaiin yangu na kwa sababu ni mcha mungu na kwa kua kushinda au kushindwa hakumpunguzii chochote au kumuongezea chochote.

Nafikili atayapokea matokeo yoyote yatakyo patikana ali hali bado ana baki kama mzee wetu wa kitaifa na watanzania tutaendelea kumtunza na kuitunza hadhi yake kama rais au kama rais mstahafu, yaliyopita yamepita. Mzee Magu hatakiwi kuwa na wasiwasi kwa sasa hapaitajiki visasi tena
 
Ungejitahidi ukaandika kingereza kilichonyooka au kiswahili pekeyake kilichonyooka mkuu

Hata hivyo uchaguzi wa mwaka huu pamoja na kwamba utakua na mazonge mengi bado sijaona mwenye ubavu wa kupimana na JPM

Hata TL, BM wangepata msaada wa kutoka NATO yote JPM ni lazima amalizie muhula wake

Tutarudi hapa November kukumbushana(Sio utabiri) ni hali halisi
Mkuu ukweli kama huu haupendezi masikioni mwa vijana wa bavicha.
 
Yan mm na akili zangu niende kwenye kituo cha kupiga kura nmepe mlopokaji (lissu) kura yangu? Never never.. ...ni jambo jema taadhari muhimu
 
Si vizuri kutuhumu nchi bila kuwa Na uhakika. Hayo mawazo yako yanaweza chukuliwa kuwa ndiyo mawazo ya serikali iliyopo madarakani. Huu Ni uchonganishi. Mnatafita nini? Kuna siku mtashitakiwa!
 
Kejuu,

Yawezekana wewe utakuwa unaamimi una uwezo mkubwa wa kuona na kuchambua mambo. Lakini naamini unakosa vitu vingi sana. Sijui ni kukosa uelewa au huna taarifa au ni mvivu wa kujielimisha kiasi kwamba huna uwezo wa kutambua kama unayolishwa ni kweli au uwongo.

Kuna mafanikio madogo sana ya kiuchumi katika awamu hii kuliko mbili zilizotangulia. Tafuta vigezo vya ukuaji wa uchumi, ndiyo utaelewa.

Hata kwa indicators za ndani, tupo kwenye nafasi duni kuliko ukuaji wa awamu nilizozitaja.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom