Serikali boresheni mfumo wa kidigitali kupokea maoni ya watu kuhusu masuala mbalimbali yanayoihusu nchi yao

budagala

Member
Jun 11, 2015
73
136
Ni jambo lisilopingika kwamba watu wote wenye maono kuhusu wapi tuipeleke Tanzania hawawezi kupewa dhamana ya uongozi au ufanya maamuzi.Hii ni kwa sababu nafasi za uteuzi au uwakilishi ni chache na wananchi tupo wengi.

Binafsi nimeitafuta muda mrefu fursa ya kuwa mwakilishi wa wananchi au mtumishi wa serikali ili niitumikie nchi yangu kwa uzalendo na wivu mkubwa.Sasa kwa kuwa mfumo wa kupata viongozi wa kuteuliwa au kupata wawakilishi kama wabunge umejaa figisu figisu na haueleweki,basi nawaomba Serikali mtutafutie special forum sie wazalendo tutoe maoni yetu ya siri kuhusu tunavyopenda nchi yetu kuendeshwa.

Mimi sio muumini sana wa uanaharakati wa kuhatarisha maisha yangu au kutumia lugha isiyofaa hadi nipotezwe au kuitesa familia yangu kwa kuanza kutunishiana msuli na serikali ambayo ina mkono mrefu.

Ombi langu ni moja tu,Mama Samia au wasaidizi wako kama mnanisikia,tutafutieni official digital platform,tuwashauri kwa staha mambo mbalimbali ambayo sie tulioko huku vijijini tunayaona na mkiyawekea mkazo,mama Tanzania itapiga hatua kubwa za kimaendeleo.Forum hiyo haitakuwa ya uchawa wa kusifia ili kupata uteuzi.Itakuwa forum ya kizalendo inayotaka kubadilisha status quo kwa nia njema wala sio kwa lugha chafu au kuikosea heshima serikali na mkuu wa nchi.Watu tunaoipenda nchi hii tupo wengi na wengine kwa kuwa tumekuwa tukinyimwa uteuzi,basi hamna shida na wala hatuna kinyongo.Tupeni basi nafasi tutoe maoni yetu yanayoweza kuwasaidia kuipeleka Tanzania kuwa taifa lenye nguvu kubwa za kiuchumi,kijeshi n.k.

Wengi tuna mawazo mazuri tu yatakayowanyoosha hata wenzetu jirani ambao wanakuja kasi kutaka kutu over take katika bandari na uchumi wetu wa utalii.Hatujawa hata na mwafaka wa kitaifa wa ku counter attack wenzetu wanaojitangaza huko duniani Kiswahili ni cha kwao na Mlima Kilimanjaro upo kwao.

Vision 2050 iendane na digital platform ya watu kutoa maoni yao kwa staha hata kama yatawakera wakubwa au kuwaudhi
 
Back
Top Bottom