Kuna uwezekano mkubwa mwakani wakazuiliwa kuandaa mabango ya kudai nyongeza ya mshahara

Equipment

Senior Member
Feb 14, 2017
187
168
Serikali imesema watumishi wa umma hawapaswi kuomba nyongeza ya mwaka ya mshahara, bali Serikali ndiyo yenye uamuzi wa kutoa au kutotoa nyongeza.

Hayo yamesemwa bungeni leo Mei 14, na Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Utumishi na utawala bora) Dk. Mary Mwanjelwa wakati akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum, Tunza Issa Malapo (Chadema).

Mbunge huyo alitaka kujua serikali inatumia sheria ipi kutowapa wafanyakazi stahiki zao zinazohusu kupandishwa madaraja, na ongezeko la mwaka.

Katika majibu yake, Dk. Mwanjelwa amesema kwa mujibu wa kanuni E.9 (1) ya kanuni ya kudumu katika utumishi wa umma za mwaka 2009, toleo la tatu, nyongeza ya mwaka ya mishahara haipaswi kuombwa.
 
Yaani hapo serikali imejibu kwamba sio lazima
Halafu ikifika Mei Mosi -wafanya kazi wa serikali ndio wakwanza kuimba nyimbo za mapambio
Hiyo ni dharau kubwa sana wakijua hawawezi kufanywa jambo lolote.Inaonekana kujibu kwa lugha yenye staha haiwezekani siku hizi.
 
Utabiri wangu ni kuwa siku ya Mei mosi 2020, jiwe hatahudhuria, atamtuma waziri amwakilishe!! Ile Ahadi inampa tabu jiwe
 
Wakikamilisha miradi na mengineyo wanataka wasifiwe wao tu wakati watimizaji ni haohao wanaowakatisha tamaa.Watumishi wana wakati mbaya sana awamu hii.
Kwa kweli hii ni awali mbaya sana - kama unaishi tz then ukisema kuwa haujawahi kumuona shetani ' itakuwa unaongopa
 
Kuna mawazo hua yana niijia kwamba Kama miaka mitano ya kwanza Mambo yako hivi je mitano ya mwisho Nini kita happen
 
Kuna mawazo hua yana niijia kwamba Kama miaka mitano ya kwanza Mambo yako hivi je mitano ya mwisho Nini kita happen
Ukizingatia kuwa awamu ya pili Marais huwa hawajibembelezi kwa wananchi! Watumishi watakiona cha mtema kuni!!
 
Serikali imesema watumishi wa umma hawapaswi kuomba nyongeza ya mwaka ya mshahara, bali Serikali ndiyo yenye uamuzi wa kutoa au kutotoa nyongeza.

Hayo yamesemwa bungeni leo Mei 14, na Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Utumishi na utawala bora) Dk. Mary Mwanjelwa wakati akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum, Tunza Issa Malapo (Chadema).

Mbunge huyo alitaka kujua serikali inatumia sheria ipi kutowapa wafanyakazi stahiki zao zinazohusu kupandishwa madaraja, na ongezeko la mwaka.

Katika majibu yake, Dk. Mwanjelwa amesema kwa mujibu wa kanuni E.9 (1) ya kanuni ya kudumu katika utumishi wa umma za mwaka 2009, toleo la tatu, nyongeza ya mwaka ya mishahara haipaswi kuombwa.
Hawa wafanyakazi ni wakupuuzwa tu, Kwan hata mwakani wakiongezwa kidogo tu watasahau yote ya nyuma na kuanza kusifia kua ni raisi Bora hajawahi kutokea anatujal Sana, achana nao hao wafanya kazi,

Ila pole Sana Kama na ww ni mfanyakazi wa uma , endelea kupigania haki yako.
 
Back
Top Bottom