Namshukuru aliyeleta uzi huu Mungu ambariki sana. Watu wako njia panda wanajua Yesu anaponya,ila hawajui wafanye nini. Watu wanapiga hela kwa jina la Yesu. Watu wana maradhi terminal cases za luekemia,hiv,diabetes,skin & colon ,pelvic cancers n.k wanataka kujua huyu anaeponya yupo. Lazima tujitofautishe ama sivyo watu watatuweka wote kwenye kapu moja.
Je umebanwa? Unaona giza mbele?hakuna msaada? Watu wanakutia moyo kiujanja ujanja huku wanasubiri ufe? Calm down.
Kabla hujaendelea kusoma chini rudi uzi #21 kuna bro amepangilia vizuri hii habari ya uponyaji inakujaje.
Ingia ndani ya moyo wako jisalimishe kwa Yesu kwa sala ya Toba,taratibu. Kuna uzi nyuma hapo una maandiko mazuri sana kuhusu uponyaji,ni vizuri kuupitia
Ukisha omba sala ya toba amini kwamba Mungu kwa Jina la Yesu amekusamehe. Usipoamini hilo utapata tatizo,shetani atakuyumbisha. Pia watu wengine wamepitia maisha ya kutisha hawaamini Mungu anasamehe kwa jinsi hiyo tu. Mungu anajua kama umezichukia dhambi au unataka upone urudi kule kule. Kifupi Amini kwamba umesamehewa. Baada ya hapo omba Bwana Yesu awe kiongozi wa maisha yako. Kwani katka mwili bado tamaa na mashindano ya mwili yapo na kero nyingine kwa nafsi yako huwezi.Ukiwa una omba amini Mungu anasikia hoja zako,huhitaji kulia na kulalama. Halafu omba Mungu akuponye shida yako. Ukiomba amini Mungu amesikia na uamini pia labda Marko 11:24 itakusaidia namaanisha nini. Baada ya hapo kaa katika imani Mungu anashulikia hilo tatizo. Na pia usianze kuwaza dr kasema hivi oh sijui mbona nieomba sijasikia kitu. Tafadhali usimpangie Mungu utapona vipi na kuanzia wapi,yeye ana spea zote,si ndio Muumbaji. Wengine wanapona ghafla wengine polepole. Cha msingi dhambi ikiwa ni pamoja na mawazo machafu yakatae. Kwa hali halisi utapata upinzani sana kimawazo na hii ni kawaid a kutokana na kukosa Mafundisho mpaka tunamwona shetani Mkubwa kuliko Mungu.
Nimeandika kwa watu waliokata tamaa. Wanaona mauti mbele na watu wanasubiri kugawana mali.
Ndg mpendwa haijalishi ugonjwa wa hospitali au majink au uchawi. Hapa tunafundishana na kutiana moyo. Labda nimalize kwa shuhuda ya tatizo lilonipata ambalo na amink lilikuwa ni nguvu za giza. Hivi visa vya watu kuanguka chooni kufa ghafla nilikuwa navisikia tu.
Ofisini siku moja nilikuwa nafanya kazi kwenye computer nikiwa na bosi wangu. Ilikuwa mida ya saa 10 hivi. Nilijisikia haja ndogo nikaenda choo cha nje cha shimo kama mita 20. Nilitegemea kupata choo hivyo nilisusha jeans langu, baada ya kutoa mkojo kidogo sana nikasimama nikapandisha jeans. Humo humo chooni nilivamiwa na kitu mwili mzima nikaona naishiwa nguvu na dalili za kufa nikaanza kuona giza,kupumua napata shida. Nilichanganyikiwa nikasema hii ndio stroke au,kumbe watu wanakufa hivi ? Nikiwa bado udhaifu unaendelea kunimaliza nguvu nikatoka njr ys choo. Hapo ndio nilishangaa nikaona dunia imebadilika muonekano wake, kuna watu nilikutana nao nje wakanisalimia na niliwatumbua lakini nilikuwa naangalia juu hivi niko wapi kwa hiyo siku mjibu mtu.Nilaamua kurudi kulekule chooni kuomba. Nikajua sasa nakufa ngoja nifanye maombi ya toba nisiangukia jehanum. Kwa hiyo niliacha kupanich nilitukiza moyo. Nikaanzs kuomba sala ya toba taratibu. Baada ya hapo nikaanza kukemea zile nguvu za giza. Nilijikuta naomba hivyo. Ghafla nikaona kibano kimeondoka na hali inakuwa shwari nikakemea tena na tena. Hsli ikawa shwari ingawa mtikisiko ulinidtua . Nikatoka chooni nikamkuta boss ananisubiri,sikumwambia lolote. Nikamaliza kazi nikapanda pikipiki yangu kubwa Yamaha toka ubungo maji mpaka Tabata Kimanga. Nimeandika haya ili wengine wasidhani hatukutani na vitu hivyo. Kwa mfano: Kama huna Yesu mganga/mchawi atatembea na mkeo nae anajua unamwogopa.
Mambo kama hayo
Tumepewa hazina ya ajabu. Wengine mleta uzi huu atafanikisha wao kupona,kutokana wachangiaji.
Mi nafunga ukurasa kwa leo poleni kwa kuwachosha
Jina la Bw. Libarikiwe