Unapofika Stendi ya Mbezi na kuhitaji huduma ya choo kwenye ghorofa ya kwanza, unatozwa Sh300 bila kupewa risiti. Hata hivyo, ukienda ghorofani kwenye waiting lounge, unatozwa Sh200 na unapewa risiti.
Hali hii inazua maswali kuhusu uhalali wa tozo ya Sh300 na matumizi ya mapato hayo. Ikiwa tozo hiyo haijaidhinishwa, kuna viashiria vya ukiukwaji wa taratibu na upotevu wa mapato ya Serikali. Wahusika wanapaswa kuchunguza tofauti hiyo na kuhakikisha wananchi wanatozwa kiwango rasmi na kupewa risiti kwa kila malipo.
Hivi sisi kama taifa tunaweza nini? Hiki hakikuwa kipindi cha kujadili mambo ya namna hii, vyoo, matumizi yake, risiti yaani tunachoweza hasa nini, kila mtu kwa nafasi yake anataka tu ale, kuanzia wanaoiba kura hadi wanaoibiwa kura.