mfianchi
Platinum Member
- Jul 1, 2009
- 11,867
- 8,280
Hivyo ni muhimu vinatumika kama kengele za kanisani. Mimi nakaa karibu na kanisa moja kubwa lina mikengele mikubwa basi ikianza kupigwa hiyo inabidi uweke pamba masikoni lakini silalamiki kwakuwa vyote hivyo vinatumika kwaajili ya kuwaita waumini kwenda kumwabudu Mungu. Tena mimi hivyo vipaza sauti vya msikini huwa navipenda sana kwani vinanisaidia pia kujua majira au muda katika siku. Mfano asubuhi huwa vinanisaidia sana kukujulisha kuwa kumekucha amka ukasali kisha uelekee kwenya kutafuata/kuhangaika. Ameni!
Kengele hazipigwi usiku,pia makanisa yameacha kutumia kengele,na hizo kengele tayari zimekuwa chuma chakavu,hebu na mtu aseme ni kanisa lipi linatumia kengele kuwaita /kuwajulisha waumini wake kuwa sala inaanza/inaisha.Hayo mambo ya kengele ilikuwa zamani ,siku hizi hakuna.Pia mlalamikaji nae ana haki na si msikiti tu ndio wana haki,ni wakati wa kubadilika waumini wako wote hapo hapo hiyo misipika na mikelele saa 10 usiku ni ya nini?