Kuna umuhimu wa kuwa na benchi la ufundi vituo vya polisi na jeshi

dmkali

JF-Expert Member
Nov 17, 2014
11,284
21,403
Hodi humu!

HISTORY FUPI YA KAZI YA KIPELELEZI

Naomba kushuhudia kazi moja iliyowahi fanywa na baba yangu aliyekuwa kitengo, Kuna mama mmoja aliwahi kutuhumiwa kwa kumwibia boss wake pesa nyingi zaidi ya mili 70, Mama huyo baada ya kupata zile pesa alihama alipokuwa anaishi, Baada ya kupeleleza ikasemekana alikwenda kijijini kwao Morogoro,Police waliamua kumfatilia hadi kijijini kwao, waliweza kwenda lakini bahati mbaya hawakumkuta,kwani walijibiwa kwani hamjakutana naye? Mbona katoka sasahivi kaenda Dar kwa shangazi yake? Wakamjibu hatuja kutana na mwanamke zaidi ya bibi momoja aliyebeba kuni, wakaambiwa kaaga anaenda dar kwa shangazi yake, waliweza kurudi dar walipofikadar kwenda kwa shangazi shake, walikutana na Bibi mmoja na na kuwaelekeza kwa Yule shangazi mtu, waliweza kuizingira ile nyumba.Bahati mbaya hawakukuta mtu ndani nyumba haikuwa na mtu, Ikabidi watulie kwa siku kadhaa, Baadae wakapata taarifa kuwa Yule mama yupo kijijini kwao ila wakitaka kumkamata waende mida ya usiku. Wakajipanga na kwenda tena kule kijijini, walifika usiku, kwa bahati mbaya kijiji kile kilikuwa na ulinzi wa sungusungu, na ikabidi waingie kwa style ya klabuni, ili wawe na wenyeji wawatangulie, vinginevyo wangeshitukiwa mapema maana vijijini mtu mgeni anapofika tu ni rahisi kila mtu kujua. Walifanya hivo, na walipokaribia kwa Yule mama, wakakutana na Babu mmoja akarudi nao hadi nyumbani akawaonyesha chumba alicholala binti yake kilichokuwa kinawaka taa, waliizimgila ile nyumba lakini walishangaa kile kibatari kilizimwa na chumba kizima kikawa kinaonekana kwa ndani kama kinawaka moto, walipofanikiwa kuingia hakukuwa na dalili za moto, na hakukuwa na mtu yeyote ndani, Yule mzee akawambia huenda kaenda uwani ila chumba chake ndo hicho,kwahiyo siku hiyo hawakufanikiwa,…STORY NI NDEFU SANA…ila mwisho wa picha mzee wangu akashauri wamshilikishe mtaalamu ( bench la ufundi/babu) Wakafanya hivo kwa siri ili kazi iishe, walipokwenda kwa babu, akawaambia huyo mtu msingemkamata, ana uwezo mkubwa sana, lakininitawasaidia kumkamata, Akawapa dawa, na akawambia nendeni, lakini mtakapokaribia kwake msiwashe tochi, Tumie mwaka wa vijiti au vibatari kwani mtakapowasha tochi tu mtamkosa tena, na yeyote mtakayekutana naye karibu na nyumba kwake kamateni, atakakuwa ndo huyohuyo, Wakafanya kama walivyoelekezwa na ni kweli wakafika na kukutana na kibabu kikongwe na mkongojo wakakidaka, na wakakiomba kiwamulikie kwa kijiti cha moto huku wengine wamezingira ile nyumba na baada walivyoingia ndani wakamkuta yule dada!..Hii ni summary tu ya story kama hizi. Hii ni ya kweli kabisa sio utani.

UJAMBAZI NA UGAIDI UNAOENDELEA KUUWA WATU

Kuna ujambazi unaendelea Tanzania,watu wanavamiwa hovyo hovyo majumbani mwao, hususani mkoa wa wa temeke maeneo ya mbagala-mikwambwe/kibada, usalama ni mdogo sana, hakuna ulinzi watu wanajirinda wenyewe, na inapotokea machafuko ya mauaji wakati mwingine inakuwa ni vigumu kuwatambua wahusika moja kwa moja hadi, kuna watu wanajeruhiwa ama kuuwawa, kuna watu wanataftwa na police na wana mauza uza kukamatika, inalichukua mda mlefu sana jeshi kuwakamata Kwani kuna waharifu wengine hutumia ushirikina kujificha.

JEE KUNA JESHI LOLOTE LILILOWAHI SHINDA VITA KWA NGUVU ZA BABU?

Yees! Kuna majeshi kadhaa yamewahi shinda vita kwa msaada wa waganga, siyo mbali, kuna mapigano yaliyowahi tokea CONGO mwaka mmoja katika misitu ya LUGUMBASHI, wanajeshi wa kongo walipoona wamezidiwa, walipata msaada wa waganga ili wasiweze kuonekana dhidi ya maadui na walifanikiwa kuwacharaza adui kwelikweli. Ipo mifano mingi kama hii ila huwa haisemwi.

USHAURI KWA JESHI LA POLICE/JESHI

Nina story za matukio kama haya ambayo ni kweli yapo na yamewahi kutokea,pamoja na hayo kuna kesi mbalimbali watu wanatumia ushirikina kupoteza ushahidi, kuna watu hutumia ushirikina ili kesi zao zisisikilizwe na hakimu kiila siku anaipiga karenda hadi kesi zinafutwa kabisa.nashauri jeshi la police/ jeshi liajili/kuwekwe kitengo cha Benchi la ufundi/Babu tena kama ikiwezekana wapewe magari maalum ya kipolice tena hata yaandikwe BENCH UFUNDI POLICE ili kuongeza ile HIGH VISIBILITY FORCE pamoja na kusaidia kazi za kipelelezi zenye changamoto ya kishirikina..pamoja na hilo nategemea ujio mpya wa OCD/OCS kwa mbagala ataongeza dolia tena ikiwezekana ulinzi shirikishi pia urejeshwe katika mkoa wa temeke kwani kuna ujambazi umekithili sana maeneo ya majimatitu,mikwambe,kibada watu wanavamiwa hovyohovyo kwakweli.

USHAURI KWA RAIA NA MALI ZAO

Naomba kutoa ushauri kwa wananchi angalau kama unauwezo jaribuni kufunga security systems and camera katika majumba yenu ili angalau kusaidia jeshi la police katika upelelezi, nashauri hivo kama mtaalam mwenye kampuni inayotoa ushauri na ufungaji wa security system and camera, ikiona inafaa waweza nicheki kwa namba 0789733825
(ushauri huu unaweza onekana wa ajabu sana kuwashauri wakuu laivu lakini hapa angalau usomeni)
 
Back
Top Bottom