Kuna umuhimu wa kujisajili BRELA?

oxlade

JF-Expert Member
Jul 8, 2012
601
96
Mimi nina fremu nakodisha CD naomba mawazo yenu, je kama nataka kusajili kampuni yangu BRELA nitaisajili vipi, Na je ni faida zipi ofisi yangu itapata kwa kuisajili kampuni yangu BRELA?

Asanteni na ninaomba michango yenu.
 
Yapo maelezo mengi, ila kwa biashara ndogo kama yako haina haja ya kufungua kampuni....kampuni ni kitu kikubwa chenye taratibu nyingi kuanzia kufungua na kumanage .... ila kusajili jina LA biashara yako brela ni vema zaidi, biashara nawewe mtambulike....faida zipo nyingi...
Kwa ushauri zaidi nitembelee kwa ofc kama uko dar, kama uko mbali, inawezekana watu kama Mimi wapo huko, watafute au endelea kuwasiliana nami pia tembelea; www.kimiconsultancy.blogspot.com
 
Yapo maelezo mengi, ila kwa biashara ndogo kama yako haina haja ya kufungua kampuni....kampuni ni kitu kikubwa chenye taratibu nyingi kuanzia kufungua na kumanage .... ila kusajili jina LA biashara yako brela ni vema zaidi, biashara nawewe mtambulike....faida zipo nyingi...
Kwa ushauri zaidi nitembelee kwa ofc kama uko dar, kama uko mbali, inawezekana watu kama Mimi wapo huko, watafute au endelea kuwasiliana nami pia tembelea; www.kimiconsultancy.blogspot.com
Naomba kujua ofisi zako zilipo mkuu
 
Faida Tano(5) Za Kurasimisha Biashara Yako Na Kuiendesha Kitaalamu.
By Napenda Biashara August 24, 2015 KUANZA BIASHARA, MBINU ZA BIASHARA No Comments

Sehemu kubwa sana ya watu kwa sasa wanajihusisha na biashara. Na kwenye biashara hizi kuna wafanyabiashara wadogo, wafanyabiashara wa kati na hata wafanyabiashara wakubwa.

Makundi haya matatu ni muhimu sana kwa ukuaji wa uchumi wa nchi yoyote. Sio kwamba biashara kubwa ni bora kuliko ndogo, bali zote zina umuhimu mkubwa.

Lakini wafanyabiashara wengi wadogo wamekuwa hawaelewi hili. Wamekuwa wakiona kama biashara zao ni ndogo na hivyo hazina umuhimu mkubwa ukiacha kwao binafsi. Kwa mtazamo huu wamekuwa wakiendesha biashara hizo kienyeji na hivyo kukosa nafasi nzuri za kuweza kukuza zaidi biashara hizo.

Wafanyabiashara wengi wadogo hawajarasimisha biashara zao na hii imekuwa inawanyima vitu vingi sana ambavyo vingewasaidia kukuza biashara hizo. Kama wewe ni mfanyabiashara mdogo au unapanga kuingia kwenye biashara, basi leo utajifunza faida tano za kurasimisha biashara yako kupitia mtandao huu wa NAPENDA BIASHARA.

Karibu sasa uzijue faida hizi tano;

  1. Unafanya biashara kwa amani na bila ya usumbufu.
Wafanyabiashara wengi wadogo wamekuwa wakisumbuliwa sana na vyombo vya kiserikali kama halmashauri na mamlaka ya kodi. Mara nyingi wafanyabiashara wamejikuta wakifunga biashara zao ili kukwepa kukamatwa kwa kuendesha biashara bila ya kusajiliwa na mamlaka hizi. Japo wengi huona ni rahisi kufanya hivyo, lakini ukweli ni kwamba wanapoteza muda mwingi na wateja pia kwa kufunga funga biashara zao kuogopa kukamatwa.

SOMA; Kitu Kimoja Kitakachokutofautisha Wewe Na Wafanyabiashara Wengine, Na Kukuongezea Wateja Pia.

  1. Kupata huduma kutoka taasisi za kifedha.
Kama unataka kuongeza zaidi mtaji wa biashara yako, basi moja ya njia za kufanya hivyo ni kuchukua mkopo. Na ili uweze kupata mkopo kutoka kwenye taasisi yoyote ya kifedha ni lazima uwe na biashara iliyosajiliwa. Watu wengi huhangaika kusajili biashara zao pale wanapohitaji mkopo na hili limekuwa linawalazimu kutumia hata rushwa ili usajili uende haraka. Lakini kama wewe utachukua hatua na kusajili biashara yako leo, utakapofika wakati wa kuhitaji mkopo utapeleka tu vielelezo kwamba tayari biashara yako ilishasajiliwa.

  1. Kuiendesha biashara kitaalamu zaidi.
Unaposajili biashara yako, unaleta picha kwamba tayari unahitaji kuifanya kitaalamu. Utahitaji kuijua biashara yako vizuri zaidi na hata kuifuatilia kiundani. Utakaposajiliwa utakuwa unakadiriwa kodi kila baada ya muda fulani. Makadirio haya ya kodi yatakufanya wewe uijue biashara yako na hata ikibidi upate msaada wa wataalamu wa kodi ili wakutengenezee vizuri mahesabu yako ya kodi.

  1. Kuimarisha ushirikiano na wafanyabiashara wengine.
Ni rahisi sana kushirikiana na wafanyabiashara wengine kama unaendesha biashara iliyosajiliwa. Ila kama biashara yako haijasajiliwa utashindwa kufanya hivyo. Watu wanaamini zaidi biashara zinazoendeshwa kwa utaratibu wa sheria kwa sababu wanajua chochote kitakachotokea wapo upande salama. Ila kufanya biashara na wewe kama mtu binafsi inaweza kuwa hatari kwa biashara nyingine inayofanya hivyo.

  1. Unachangia ukuaji wa uchumi wa nchi.
Ndio hii ni faida nyingine kwako na kwa jamii inayokuzunguka. Japo unaweza usione hilo kwa haraka, lakini wanafunzi mashuleni, wagonjwa mahospitalini, na maendeleo mengine mengi yanayofanyika, wewe na biashara yako mnakuwa mmechangia kwa kiasi kikubwa kwa kodo mnayolipa. Ni jambo zuri kwako kuwa sehemu ya maendeleo ya nchi yako na jamii inayokuzunguka pia.

Anza leo utaratibu wa kurasimisha biashara yako kama bado hujafanya hivyo. Utafaidi mengi kuliko sasa unavyoiendesha kwa viwango vya chini.

Kwa ushauri wa biashara Faida Tano(5) Za Kurasimisha Biashara Yako Na Kuiendesha Kitaalamu.
 
Back
Top Bottom