CAG amenyang'anywa "Udhibiti" amebaki na "Ukaguzi"

Jumanne Mwita

JF-Expert Member
Nov 18, 2014
424
1,044
KATIBA, ibara ya 143, ibara ndogo ya 2.

A. Inafafanua, CAG ndiye mwenye wajibu wa kuhakikisha kila thumuni inayotoka Hazina, inakuwa imeidhinishwa na Bunge. Na kujiridhisha matumizi yake.

B. CAG anapaswa kuhakikisha matumizi yote ya Serikali yanatokana na fedha zinazotoka Hazina.

C. CAG anapaswa kufanya ukaguzi angalau mara moja kwa mwaka na kuandaa ripoti.

Katiba, ibara ya 135, inaelekeza kila pesa inayokusanywa kwa ajili ya matumizi ya Serikali, lazima iingie Hazina.

Kisha, ibara ya 136 (3), inasisitiza kuwa fedha hazitatoka Hazina mpaka CAG aidhinishe.

SHIDA ILIPO

Ripoti za CAG kwa miaka sasa zimekuwa zikionesha kuwa majukumu mawili ya CAG ya kudhibiti utokaji wa fedha Hazina na kujiridhisha kama matumizi yapo kwa mujibu wa sheria, Wizara ya Fedha inayapora.

Majukumu hayo ndio yanajenga uhalali wa CAG kuitwa "Mdhibiti". Sasa, amebaki kuwa "Mkaguzi" tu.

Anakagua na kukabidhi ripoti kwa Bunge ambalo nalo linapitisha azimio la kumpongeza Rais, badala ya kuishughulikia Serikali.

Kipindi cha Magufuli, tulishuhudia fedha zinatoka Hazina bila taarifa. Sh1.5 trilioni. Kisha Sh970 bilioni. Mara Sh2.4 trilioni.

CAG 'akalalamika' kuwa fedha nyingine zilikuwa zinapokelewa na kutumika juu kwa juu bila kupita Hazina. Hivyo, kukosa udhibiti.

Wakati huu wa Samia, CAG anabaini Sh577 bilioni zilitoka Hazina bila maelezo. Sh1.46 zimetuka nje ya bajeti.

Yote hii ni kuonesha kuwa Serikali inapora mamlaka ya CAG ya kudhibiti fedha na matumizi Serikali kutoka Hazina.

Kutoa fedha Hazina bila idhini ya CAG, maana yake ni kuvunja Katiba. Ni kulidharau Bunge. Ni kuichukulia poa Sheria ya Bajeti iliyotungwa na Bunge.

Mwigulu Nchemba lazima atoe majibu, Sh577 bilioni zimetumikaje nje ya Bajeti. Na zilitokaje bila CAG kujua. Zilikwenda wapi na kufanya nini?

Kwako Rais Samia; umeitoa nchi gizani, umeirudisha mwangani. Tunahitaji uwajibikaji.

Mwaka 2012, Kikwete aliwaondoa kazini mawaziri, Mkulo (Fedha), Chami (Viwanda na Biashara), Nundu (Uchukuzi), Mponda (Afya), Ngeleja (Nishati na Madini), vilevile naibu mawaziri, Nkya (Afya) na Mfutakamba (Uchukuzi). Kupitia ripoti ya CAG. Bunge lilikuwa imara.

Luqman MALOTO
 
Sema mwanzo mgumu, ila kwa taswira iliyopo, tunaona kabisa Rais Samia ataturejesha katika mstari, nadhan, suala la udhibiti litalejeshwa mikononi mwa CAG very soon.

Sina wasiwasi na Rais, Mama Samia .
 
Umeelewa vibaya

Anayeidhinisha matumizi ya fedha za serikali ni Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania. (Ibara ya 136).

CAG anawajibu wa kuhakikisha fedha inayotoka hazina ni ile iliyoidhinishwa na Bunge. Ndipo anatoa idhini zitoke. (Yeye ni jicho la bunge kwenye mfuko wa hazina kuhakikisha kile kilichopitishwa ndicho kinatoka)

That's a very limited role, it might sound like a big thing but it's not. Matumizi mengi yanayolalamikiwa yapo kwenye bajeti na yameidhinishwa na Bunge, there is nothing CAG can do kuzuia fedha zisiende kwenye vyura kwa mfano, kwakua hiyo fedha ipo kwenye bajeti na ilipotishwa na bunge.

CAG ni jicho la bunge, sio mhimili unaojitegemea.
 
Back
Top Bottom