Kuna umuhimu gani wa kuulizana makabila wakati wa kupatiwa huduma za Umma?

Hata Guest house lazima ujaze kwenye daftali lao wanaboa Sana... Huwa naandika mchagga tu
Tatizo ukifa hospital au guest house uliandika jina peter Paul kabila ukashindwa kuweka au ukaandika la uongo. polisi wakitangaza hakuna ndugu atakuja kuchukua maiti yako utazikwa nA city

Mfano umepata ajali wasamaria wakakuokota kujiandikisha unatakiwa uandika majina, Kabila nk kurahisha kutambuliwa na marafiki, ndugu, majirani nk
 
Mkuu nani alikuambia kuwa kabila ndio utambulisho halisi wa mtu,Mimi nadhani kioengele cha kabila na dini kiondolewe katika masuala ya huduma kwa umma ,mtu hawezi kutambulika kwa kabila Bali majina na eneo analotoka
Tatizo ukifa hospital au guest house uliandika jina peter Paul kabila ukashindwa kuweka au ukaandika la uongo. polisi wakitangaza hakuna ndugu atakuja kuchukua maiti yako utazikwa nA city

Mfano umepata ajali wasamaria wakakuokota kujiandikisha unatakiwa uandika majina, Kabila nk kurahisha kutambuliwa na marafiki, ndugu, majirani nk

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Asee na mm umenitoa tongotongo, kuna hizi survey za online mfano premise Unaweza kuulizwa kabisa lako wakati wa Kujiandikisha lakini ukifanya kwa site za nje utaulizwa asili yako kama ni uerope, Spanish African n.k sa hapa ndio nimejua maana yake.

Kumbe basi huenda baadhi ya maswali utakayoulizwa yakatokana na jamii unayotokea. Big up sana
Wazungu hawana makabila, ukienda watakuuliza ethnicity yako, either African, Hispanic, American, African-American n.k.

Unforgetable

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Muhimu kwa baadhi ya mambo, mfano ukisema wewe Mkurya, mulaaa unatokea mara kwenye recruitment za jeshi walau unafikiriwa.

Ukisema mzaramo ktk ajira tutakupangia sanaa na utamaduni

Mchaga,basi zile sehemu za fedha unawezafanya vizuri ama tusikupe kwa kuhofia kutupiga.

N.k n.k

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna jamaa yangu alipata msala tukiwa chuo..
Siku anapewa dhamana akaulizwa kabila na hakimu akajibu sina kabila, hakimu alimind sana akamuuliza kwann anakosa kabila, jamaa akakomaa kuwa yeye hana kabila.. Ilibaki kidogo arudishwe mahabusu.. Sema ndugu zake waliingilia kati kumtetea.

Sasa sijui kwanini wanalazimisha kila mtu awe na kabila?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom