Kuna umuhimu gani wa kuulizana makabila wakati wa kupatiwa huduma za Umma?

Ni muhimu sana kwa kutunza takwimu. Kwa mfano uhalifu...
Kabila gani linafanya zaidi uhalifu A na si B
Je uhalifu X unafanywa na watu wa rika lipi..

Je, kwa nini wahalifu wa dini X wenye age Y wanafanya sana uhalifu wa ubakaji, wizi wa kuvunja nk

Hii inasaidia kwa watunga sera za ulinzi na usalama kujua pa kuanzia...hata Police pia kujua wajipange vipi

Ndiyo maana mtoa hoja tuna kanda maalum ya rorya..... Ni hizo takwimu.
 
Mimi lazima mwanamke nimuulize kabila kabĺa hajanipa huduma. Unaweza kuparamia jianamke la kikuria au mchawi wa Sumbawanga aondoke na mbegu zako.
 
Hii imenikuta juzi uhamiaji, yule dada asee nilitamani kumjibu vibaya, baada ya salamu na kueleza shida zangu swali alilouliza mimi ni kabila gani daaah, kwakuwa nilikuwa na shida nikamjibu bado alihoji maswali mengi mnooo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kingsmann,
Jibu lako halina uhusiano na swali. Ukiamini kuna umuhimu wa kujua DINI ya mteja, kwa nini ajue kabila lake. Vipi kama mtu hajui kabila (au: hataki kuionyesha)?
 
Jibu lako halina uhusiano na swali. Ukiamini kuna umuhimu wa kujua DINI ya mteja, kwa nini ajue kabila lake. Vipi kama mtu hajui kabila (au: hataki kuionyesha)?
Ndio maana nimeanza na neno mfano.

Ngoja nikupe mfano halisi sasa unaohusiana na kabila.

"Head nodding" kwa watu wa bara la Asia ni kitu cha kawaida kwenye maongezi. Sote tunajua kwamba head nodding ina maanisha kukubaliana, lakini kwa hao wenzetu haimaanishi hivyo bali kama mazoea tuu.

Kwa hiyo unapoongea naye akitikisa kichwa usije kudhani ndio anakubaliana na wewe, hapana.

Vivyo hivyo kwenye kwa hapa kwetu ukishajua kabila la mteja ni hili, inakusaidia ku-integrate huduma yako na mila zao ili kupata matokeo mazuri zaidi.

Mfano kaja mteja kakuambia kabila lake ni mhaya, sote tunajua hulka yao ya grandiosity, kwa hiyo kwenye kumpa huduma utamruhusu ajieleze lakini ili uweze kupata kila unachokitafuta utamuuliza vijiswali speicific vitakavyokuwezesha kupata data za muhimu huku ukiacha zile mbwembwe zake.


Unforgetable[/i]
 
Mfano kaja mteja kakuambia kabila lake ni mhaya, sote tunajua hulka yao ya grandiosity, kwa hiyo kwenye kumpa huduma utamruhusu ajieleze lakini ili uweze kupata kila unachokitafuta utamuuliza vijiswali speicific vitakavyokuwezesha kupata data za muhimu huku ukiacha zile mbwembwe zake.
Hapana, mimi sijui "hulka yao ya grandiosity" (hujui kujieleza kwa Kiswahili??). Kumbe vipi akimpata Mhaya asiyeonyesha "grandiosity"?

Sijui kama mganga mwenyeji pale Tanga atajua tabia za pekee za Mnyiha au Msafwa. Ningehofia zaidi kama amesikia chochote kuhusu watu hao inaweza kumzuia kutoa huduma bora.

Kama a) mwuuguzu yupo kazini (badala ya kutembea nje), b) anafuata hatua za kitaalamu za kumkagua mgonjwa na c) anafuatilia yale ambayo inatakiwa kutekelezwa, basi nitaridhika kabisa.
 
Huyo hakimu lazima atakuwa mwehu tu. Hukumu inatolewa kulingana na ushahidi na sio hisia za hakimu kuhusu mtuhumiwa husika
digba sowey,
Kuna Makabila mengine yanakataa aina fulani ya Dawa kutokana na Mizimu yao, lakini pia kuna Makabila mengine yakiwa na Kesi Mahakamani yakupasa uwe makini nayo vinginevyo unaweza ukawa unamrahisishia Kazi ya Kuhukumu Hakimu kutokana na Historia mbaya ya hayo Makabila.
 
Kabila la baba yako na lako ndilo kabila la watoto wako..ingawa ni upuuzi kuulizana makabila.

Sent using Jamii Forums mobile app
Bado siyo kweli, siyo lazima kabila la baba liwe langu, na siyo lazima kabila langu liwe ndilo la wanangu. Kabila ni nini kwanza? Ni lugha? Ni utamaduni? Ni nasaba (genetic)? Ni nini?
  • Kuhusu lugha, nafahamu lugha za makabila mawili na katik hayo ya wazazi wangu hayamo
  • Kuhusu utamaduni wa kikabila sijawahi kufuata utamaduni wowote wa kabila linaloweza kuitwa la kwangu: nimeishi miji kadhaa utotoni, nimesafiri kwingi Tanzania kwa sababu ya kazi na kote niliishi na kufuata yale ninayokubaliana nayo ya mahali husika.
  • Kwenye nasaba ndiko nina kila mchanganyiko.
Ukabila ni upumbavu tu.
 
Hata kama uko safarini,ukuenda Lodge ukiletewa kitabu cha wageni lazima ujaze na kabila lako.
 
Lakini kIbila ni muhimu kwa ajili ya UTAMBUZI maana kama unaumwa unawezakukutwa na mauti, je, watujua aliyefariki ni mtu wa wapi? Hata polisi kuna mambo mengi yanawezakutokea wakati ukiwa hapo, magereza au mahakamani. Tatizo ni pale tunapoulizana dini hata kazini wakati serikali inasema haina dini wakati huo inalazimisha watu kuwa na dini, mfano, vyeti vya ndoa
Kabila siyo utambulisho wa anakotokea mtu. Kama lengo ni kutaka kujua huyu ni mtu wa wapi basi swali liwe hilohilo, wewe ni mtu wa wapi au makazi yako ya kudumu ni wapi nitakujibu natokea Kondoa nitakutajia tarafa, kata, kijiji na hata kitongoji, lakini hiyo bado haimaanishi kabila. Kwani data zinazoonesha hadi kijiji au mtaa ninakoishi hazitoshi tu?

Ukabila ni ubaguzi tu. Mtu ameishi Kondoa kwa generations nne, hadi babu wa baba yake, lakini bado unataka ajitambulishe kwa kabila la yule babu aliyehamia kutoka Musoma zaidi ya miaka 100 iliyopita, lengo ni kumbagua tu hakuna zaidi. Kwanini tusiseme sisi watu wa Kondoa kwa ujumla wetu, makabila yabaki kwenye mazungumzo na mambo ya utani na majina, basi.
 
Hata kama uko safarini,ukuenda Lodge ukiletewa kitabu cha wageni lazima ujaze na kabila lako.
Ni mazoea yaleyale ya kibaguzi. Njia sahihi ya kupata utambulisho wa mtu katika mazingira kama hayo ya lodge ni kumuuliza kitambulisho chake cha NIDA au cha kura, nakili hizo taarifa zinatosha, ni nzuri na ni reliable. Hii ya makabila haisaidii utambulisho.

Bora hata ukiuliza wilaya na kijiji anachotoka mtu, hiyo inaweza kusaidia kwenye dharura kama amezimika huko lodge polisi watajua wafuatilie taarifa zake kijiji fulani. Ukiandika kabila lako ni msukuma haisaidii maana hao wako karibu nchi nzima.

Ukirekodi makabila unakusanya data isiyokuwa na faida yoyote, ndiyo sababu hata kwenye sensa haipo.
 
Siyo kwamba hawana ,,kabila” bali wameyafuta na kujenga Taifa, watu wanaotumia. ,,kabila“ ni primitive, Dunia nzima washatoka huko isipokuwa Afrika na misitu ya Amazon ndo bado kuna ,, tribes“, kwanza tribe ni neno la dharau kama nigger tu na ni kwa ajili ya Waafrika tu.
Kuna maeneo us vichaa wengi Kama Ikungi kwa Tundu Lisu.
Pia kuna maeneo yana wakoma wengi kujua kabila kunasaidia daktari ajue atoe dawa gani ambayo hutumiwa kwenye maeneo husika
 
Back
Top Bottom