Kuna ukweli wowote kuwa uzuri wa jengo siyo uhakika wa furaha na amani?

Sky Eclat

JF-Expert Member
Oct 17, 2012
57,720
215,773
8cfcca9a9188dad38ac6302c24f36093.jpeg
 
Hakuna uhusiano wa moja kwa moja kati ya pesa na furaha katika ndoa..
 
kuna watu wamejenga nyumba nzuri.. ila wanalala vyumba tofauti hawana furaha, wanasubiri siku za kuishi ziishe tu.
 
kuna watu wamejenga nyumba nzuri.. ila wanalala vyumba tofauti hawana furaha, wanasubiri siku za kuishi ziishe tu.

Unakuta hamna maelewano na kila mtu anasema alichangia, ukifiria kuuza mjengo roho inauma, inabidi mkae siku ziende.
 
Yeah ni kweli kabisa. Furaha na amani inapotezwa na mambo mengi.

1. Watu ikiwemo wanafamilia au ndugu waishio humo, huweza tengeneza migogoro kwa namna nyingi ikakufanya hata ukakosa raha na furaha ya kuwa humo ndani.

2. Ndugu, majirani wanao wazunguka huweza kuwa chanzo au kikwazo cha raha ya kuwepo hapo. Wivu na mengineyo huwezo kuwa sababisho ya hayo wanaowazunguka kuwa nyima raha.

3. Roho na vinavyo fanana navyo.
Hapa inaweza letwa na namna mambo yalifanyika zaman, mikataba ya inayowahusu, historia ya ardhi husika au koooo. Hapa unaweza kuwa haunted hata ukaon nyumba kama jelaa
 
Nilikutana na mwana physophy aliniambia ukitaka uwe na raha na amani duniani uwe mtu wa kati, yaani usiwe masikini sana wala usiwe tajiri kupindukia. Matajiri hawalali usingizi wa amani, kuna mambo mengi wanafikiria. Masikini sana pia unawaza kesho utakula nini.
 
Huo ni usemi motivated na chuki za masikini kwa matajiri...wametunga sentensi za kujifariji,"kaolewa na tajiri,nyumba nzuri sio ndoa nzuri",hii purely sentensi ya wivu wa wazi..

Matatizo ya ndoa wanapata masikini na matajiri kwa viwango vile vile,hamna formula...tusihusishe mali za mtu na upendo wa ndoa wa wawili hao,umasikini unachangia magomvi katika ndoa the same way utajiri,tena walao hata utajiri una afadhali...

Masikini tuache wivu,kaolewa kwenye nyumba nzuri tusianze kuhukumu wakati na sisi huku umasikinini kunawaka moto the same way..

Stupid poverty mentality!
 
Inategemea pia nyinyi wawili mlikutana vipi, ni watu wa aina gani? Mkipishana sana madaraja hata la kuongea ndani mnakuwa hamna.
 
Nina uhakika watu kama mzee Mengi, Bill Gate na wachache wanafuraha sababu wana kanuni ya kurudisha walikotoa, usipofanya hivyo, utajiri wako ni kama mzigo. Hulali ukitembea unaangalia kisigino chako, inakugharimu pesa nyingi kuwa na walinzi na ulinzi kwenye nyumba. Hata nyumba nzuri kama hiuyo uliyoweka huiinjoy sababu huaminik mtu yeyote.
 
Inategemea pia nyinyi wawili mlikutana vipi, ni watu wa aina gani? Mkipishana sana madaraja hata la kuongea ndani mnakuwa hamna.

Utasema hivyo hivyo kwenye elimu,umri,status ya familia zenu,uzuri binafsi,race,/skin color,urefu,ufupi,etc,etc..shit never ends....hicho ulichokitoa cha mali tena moja tu ya nyumba,ni myopic at best!

Mwisho wa siku ni mtu tu alivyo na malezi yake,mtu mstaarabu ni mstaarabu tu,ataishi vizuri na mwenza wake regardless,mshenzi mshenzi tu...hizi mnazotoa hapa ni sentensi za wivu kwa wenye nacho as if masikini hampati matatizo kwenye ndoa zetu...hii mada ni meaningless kwakweli
 
ni maskini anayetamani kuwa na nyumba ndo anawaza kuwa those people must be very happy because they have a big house.

kama kuna kitu ulikuwa unakitaka, furaha yako inaweza kutokana na kukipata.

lakini overall sio kila ulichokuwa unataka kitakupa furaha.

watu wajiangalie wenyewe furaha yao inatoka wapi....mambo wengine naona yajibiwe umri ukishaenda. manake kuna watu wamejenga, wana mke na watoto, wana kazi, but hawana furaha. ndo hapo Mtu anawaza maisha yana maana tu kama kuna maisha mengine badala ya haya.

I think that's a very sad thought. just make the most of the life you know of.
 
Back
Top Bottom