Kuna ukweli kwenye bei za hizo machine

Kuna ukweli kwenye bei za hizo machine

OgaBoy

JF-Expert Member
Joined
Aug 22, 2022
Posts
3,183
Reaction score
4,518




Ni pikipiki mbalimbali je bei zake zina sadifu uhalisia nani anihakikishie hawa jama wapo hapa dar
 
Mkuu jamaa hawa hawako DSM kwa maelezo yao wako Z,bar chake chake
Kwa maana hii utasikia tuma tuna fanya delivery ujue imeisha hiyoo.
Aiseh mkuu acha kabisa kama itakuwa kweli yaani mtz KUKOSA usafiri ni juu yake sababu 400k Kuna bike nzuri za umeme
 
Tatizo ni moja tu kwa wafanya biashara wa kibongo.
Wanaweza kuleta bikes kutoka China, lakini hakuna duka utapata spares zake.

Hata bumper likivunjika lazima uchonge mbao, na unaweza kurudi kwenye duka wakasema zilikuja Mara moja tu kama Shati la mtumba

Unaharibu battery halafu hakuna la badili yake.

Hapo ndio huwa nachoka biashara hizo za nyumbani

Ukitaka kununua hakikisha ni Soko la kudumu kama Bajaj na Sanlg, tena ukahakikishe mwenyewe kama ni soko la kudumu

La sivyo achana nayo kabisa la sivyo utashona mpaka plastic kwa spoku ya moto
 
Back
Top Bottom