Kuna uhusiano wowote wa Waziri Jafo kuwa mwislamu na hasira kali aliyopata hadi kumsimamisha mtumishi mlevi kazi?

Mkuu kwa kitabu chao ni nini? Dini ni imani ya kikundi fulani cha watu juu ya kile wanachoaamini kuwa ni Mungu ama miungu yao. Kwa mtu ama kikundi kingine kichoamini katika imani hiyo sio kitabu wala wenye hiyo dini wenye maana kwao. Kwa maana nyingine hakuna anayelazimishwa kuamini dini isiyo yake. Haya ya jafo ni kama anataka kuelekeza watu kuamini wasichoamini wao. Mambo ya dini zaidi ya kuvumiliana hakuna kingine, sio sheria wala adhabu vinavyofaa. Waziri ameongozwa na imani yake zaidi kuliko busara na utaratibu wa nchi. Ukikomaa sana kusema mambo ya dini utakuwa mdini wa kwanza.

Sent using Jamii Forums mobile app
Unakosea, mfano kama mimi siamini katika Uislam haimaanishi niingie msikitin nianze fanya fujo na na kuharibu vitu nitakuwa ninakosea. Ebu fikiria Waislam waanze kuchana Biblia kisa hawaamini mafundisho ya dini ya Kristo? Haya mambo yasipokemewa yakakua itakuwa balaa.
Unakumbuka vurugu za mwembe chai? Unakumbuka enzi zile mihadhara ya kukashifu dini nyingine pata picha yasingekemewa leo hii tungekuwa wapi?

Jafo huenda hajalitazama kwa angle ya dini lakini kalitazama kwa angle ya usalama.

Mfano mimi nikisimama nikaanza kusema nina amini watu wote wanaotokea kanda ya ziwa na wapuuzi wana mila za kipuuzi. Ni imani yangu na sikulazimishi uamini hivyo lakini kuisema hadharani unahisi itakuwa sawa?
 
Je hao walioapa kuua mtu (kosa kisheria) wameshakamatwa na vyombo vya usalama?
Mwizi uwa akidundwa au akiiba wananchi wakamkimbiza polisi uwa wanamweka ndani kumuokoa kutoka mikoni mwa wananchi wenye hasirra kali. Kwani wananchi hao wenye hasira kali uwa wanawekwa ndani?

Serikali haina dini ila wananchi wana dini na dini ni kitu sensitive sana nadhani hakuna kitu kimeua watu wengi duniani kama "In the name of the Lord". Vita ya msalaba, Jihad, n.k
 
Wenzetu hawana uvumilivu.

Humu tu tunayavumilia mangapi?
Kila leo threads za maudhi mnaandika
Na bado tunajaribu kuwaambia acheni hizo
Nafikiri umefurahia sana pia tukio hilo

Sent from my iPhone using Tapatalk
 
Mimi sioni tatizo mtu kuchana kitabu tena kilichoandikwa na binadamu na ambacho kinanunulika madukani. Kama vipi si wamlipishe anunue kingine tu mambo yaishe. Sasa masuala ya kuwekana ndani kufukuza kazi na kutishiana kuuwana ni upuuzi gani?

Yani mtu atake kutoa uhai wa mwingine kisa kitabu tu? Huo ni upuuzi wa kiwango cha SGR.
 
Duuh aiseee hizo nyuzi za maudhi mbona huwa zinaandikwa na pande zote au ndo ile nyani haoni kundule?

Mie hicho kitabu hakiongezei kitu wala kunipunguzia hivyo sioni haja ya kufurahia kitu kisichonihusu
Humu tu tunayavumilia mangapi?
Kila leo threads za maudhi mnaandika
Na bado tunajaribu kuwaambia acheni hizo
Nafikiri umefurahia sana pia tukio hilo

Sent from my iPhone using Tapatalk
 
Aisee nimeshangaa sana eti yule aliyechana Quran kukamatwa kisa eti ameleta uchochezi wa kidini

Kwamba angeamsha hasira za Waislam na wangeweza kuchoma makanisa na kusababisha vurugu kubwa

Yaani hapa wanamaanisha Waislam ni watu wasioweza kupuuza jambo kama hilo, na ni watu wanaoongozwa na mihemko na hasira bila kufikiri, haya ni matusi makubwa sana

Yaani Waislam hawezi kumpuuza chizi mmoja aliyechana kitabu chao? Yaani wangeleta vurugu kwa watu wasiohusika kisa kitendo cha chizi mmoja?

Hii ina tofauti gani na kuhalisha hii dhana potofu kuwa Uislam ni dini ya vurugu na kuwa Waislam wanajilipua kutetea imani yao?

Waislam hawaetereki na kitu kama hiki, so kudhani wangeleta vurugu ni matusi kwao

Sent using Jamii Forums mobile app
Well said !
Kwani Biblia imefanyiwa hayo mara ngapi na watu wanapuuza tu ?
Muislam safi hawezi kuhangaika na kichaa mmoja kama huyo.
 
Huyo mchanaji kweli kakosea, anachouliza jamaa, maamuzi ya waziri, hayasababishwi na uislamu wake..?? Kama hajayatoa kwa sababu ya uislamu wake, basi tuonyeshe kifungu cha sheria kinachompa madaraka hayo..
Kitakuwepo kifungu cha sheria kinacho walazimu watumishi wa umma kuwaheshimu wenzao wamising ya imani kinaeza kisiwe direct lakini lazima kitakuwepo kikitafisiriwa kinaweza fit. Kama ambavyo hakuna kifungu cha moja kwa moja kinachosema ukitukana ni kosa kisheria lakini sheria ikitafsiriwa kutukana kunaweza kukuweka ndani
 
Mimi sioni tatizo mtu kuchana kitabu tena kilichoandikwa na binadamu na ambacho kinanunulika madukani. Kama vipi si wamlipishe anunue kingine tu mambo yaishe. Sasa masuala ya kuwekana ndani kufukuza kazi na kutishiana kuuwana ni upuuzi gani?

Yani mtu atake kutoa uhai wa mwingine kisa kitabu tu? Huo ni upuuzi wa kiwango cha SGR.
Wewe huoni tatizo ila wanaokiamini na kukiita kitabu chao wana tatizo juu ya hilo sasa kwanini ukichane kama huamini achana nacho.
Mfano kuna mtu akimfumania mke wake na njemba hatopigana wala kuua lakini mwingine ataaua kabisa. Kujiepusha na hilo usitembee na wake za watu maana kwanza siyo vizuri
 
Tatizo udini umeshika sana kasi hapa TZ na kuna upande mmoja huwa una 'play the victim' most of the time.

They are always blaming the other side for their misfortunes, problems e.t.c hawataki kabisa kuwa responsible hata kwa dawa. Wao ni kama wanaonewa kila siku.

Ndio maana wako sensitive na bullshit stuff kama vitabu kuchanwa lakini utashangaa wana retaliate kwa kuchoma kanisa au kupiga mabomu upande wa pili. Such victimhood is childish, ni inferiority complex.

Such a BS.
 
Kumbe alilewa saa za kazi. Amechana kitabu cha Mungu. Hasira ya Mungu imewaka juu yake.

Waziri hajakosea, vijana mheshimuni Mungu.

Vijana kama yeye wanatafuta ajira, yeye anafanya upuuzi huo.

Ngoja aje mtaani aone kulivyo kutamu.

Ameshindwa hata kumheshimu Mungu, shauri zake,

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wewe huoni tatizo ila wanaokiamini na kukiita kitabu chao wana tatizo juu ya hilo sasa kwanini ukichane kama huamini achana nacho.
Mfano kuna mtu akimfumania mke wake na njemba hatopigana wala kuua lakini mwingine ataaua kabisa. Kujiepusha na hilo usitembee na wake za watu maana kwanza siyo vizuri
Wallah nakuambia ni ujinga wa hali ya juu kutaka kuua mtu kisa kitabu kilichoandikwa na mwarabu.

Ina maana nyie mnaamini kitabu au mnamwamini Allah? It's only a mere book, simply paper and ink! What's the big deal!?
 
Kitakuwepo kifungu cha sheria kinacho walazimu watumishi wa umma kuwaheshimu wenzao wamising ya imani kinaeza kisiwe direct lakini lazima kitakuwepo kikitafisiriwa kinaweza fit. Kama ambavyo hakuna kifungu cha moja kwa moja kinachosema ukitukana ni kosa kisheria lakini sheria ikitafsiriwa kutukana kunaweza kukuweka ndani

Mkuu tabia unajifunza tangia utotoni
Ni malezi tu hayo kwani alielelewa kwa maadili mazuri hawezi kufanya huo ujinga hata siku moja

Sent from my iPhone using Tapatalk
 
Wallah nakuambia ni ujinga wa hali ya juu kutaka kuua mtu kisa kitabu kilichoandikwa na mwarabu.

Ina maana nyie mnaamini kitabu au mnamwamini Allah? It's only a mere book, simply paper and ink! What's the big deal!?
Mimi siyo Mwislam, haijalishi wanamwamini nani ila kama hawataki uchane kitabu chao kwanini ukichane? Usipokichanna hawatakudhuru sasa kama siyo kutafuta majanga kwanini ukichane?
Huko India kuna maeneo ukila nyama ya ng'ombe wanakuua maana wanamwabudu sasa wewe utoke hapa na kiherehere ukamchinje ng'ombe maeneo hayo kama siyo kutafuta kifo ni nini?
Imani ni kitu ambacho ukiifikiria hakina logic lakini ni sensitive sana hata wewe huenda ukiandika hapa unachokiamini kuna watu watacheka wakisema huna akili
 
Well said !
Kwani Biblia imefanyiwa hayo mara ngapi na watu wanapuuza tu ?
Muislam safi hawezi kuhangaika na kichaa mmoja kama huyo.
Naam Mkuu, Wakristo wanachomewa hadi makanisa ambyo ndani yake kunakuwa na Biblia na vingine vingi vya Dini yao na wanatulia, iweje Waislam tuonekane kuwa tutalete vurugu kwa ajili ya Quran moja?
 
Je hao walioapa kuua mtu (kosa kisheria) wameshakamatwa na vyombo vya usalama?

niliona comments kwenye mitandao tena wengi wao wanamjua jamaa vizuri, inasemekana pia hua ana tabia ya kupiga nyimbo za injili kwa sauti ya juu sana ofisini kwake

Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Vitu vingine ni ujinga tu mkuu, sio kwamba jamaa hajakosea lakini reaction ya watu ndio imenishangaza. Yani mpaka kutaka kumuua?

Kuhusu kupiga nyimbo za injili kwa sauti, kuna kosa gani kisheria hapo? Mbona misikiti inawekwa vipaza sauti na kupiga azana 24/7 huku uswahilini kwenye mchanganyiko wa imani zote.
 
Back
Top Bottom