Kuna uhusiano wowote wa Waziri Jafo kuwa mwislamu na hasira kali aliyopata hadi kumsimamisha mtumishi mlevi kazi?

mbere

JF-Expert Member
Mar 5, 2015
6,969
6,460
Ni swali, naomba kueleweshwa. Huyu mchana Kurani, mlevi, akiwa nje ya kazi, akiwa amelewa, amebishana kijiweni, akachana, huku akiwa anayumba yumba kwa ulevi, na baada ya kuchana hakuna madhara hatarishi ya kiusalama yaliyotokea.

Ghafla kasimamishwa kazi kwa kuchana Kurani. Waziri amefanya sawa kumsimamisha kazi kweli?

Kwanini hakutizama na kusisitiza walio juu yake waangalie hatua za kinidhamu, zilizopo kisheria zichukue hatua kama zipo? Au kwasababu Waziri naye ni Muisilam?

Naona amekuwa fasta sana.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ukimwangalia vzuri wala haiumizi kichwa kugundua kua alikua amelewa hivyo huyu alipaswa kupuuzwa japo kakosea sana.

Naamini angechana Biblia wala hakuna hata ambae angeipost maana wangempuuza na hakuna ambaye angepata hacra kwa hilo, sasa kwakua kachokoza mwenyewe nnafikiri apate kinacho mstahili japo kwenye hadithi Mtume alipitia masuti na aliwasamehe.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
mbere,

Mimi siyo Mwislam ila jamaa kakosea we unajua kuwa watu wako so sensitive na kitabu chao halafu unakichana kama siyo chokochoko ni nini?

Unajua machafuko mara nyingi husababishwa na vitu vidogo.
Tujifunze kuheshimiana na kuvumiliana heshimu imani na hisia za wenzako.
 
Ukimwangalia vzuri wala haiumizi kichwa kugundua kua alikua amelewa hivyo huyu alipaswa kupuuzwa japo kakosea sana. Naamini angechana Biblia wala hakuna hata ambae angeipost maana wangempuuza na hakuna ambae angepata hacra kwa hilo,sasa kwakua kachokoza mwenyewe nnafikiri apate kinacho mstahili japo kwenye hadithi mtume alipitia masuti na aliwasamehe

Sent using Jamii Forums mobile app
Vip mbona nabii tito hamkumpotezea?
 
mbere,

Alichofanya Waziri sio sahihi,kwa kuwa kuchana Qur'an hakuna uhusiano wowote na kazi ya mhusika.Alichofanya Waziri ni purely hisia binafsi ambazo zimekuwa ignited na uislam wake, kitu ambacho si sahihi.

Sio siri kwamba Waislam wanapata hasira za kupindukia dini au mtume wao anapokashfiwa kwa njia yeyote ile. Zipo nguvu "hasi" nyuma ya hasira hizo.Hata hivyo maamuzi yake yalipaswa kuzingatia "standing orders."
 
Alichofanya Waziri sio sahihi,kwa kuwa kuchana Qur'an hakuna uhusiano wowote na kazi ya mhusika.Alichofanya Waziri ni purely hisia binafsi ambazo zimekuwa ignited na uislam wake,kitu ambacho si sahihi.Sio siri kwamba waislam wanapata hasira za kupindukia dini au mtume wao anapokashfiwa kwa njia yeyote ile.Zipo nguvu "hasi" nyuma ya hasira hizo.
Kwa hiyo alicho fanya huyo jamaa ni sahihi?
 
Kwa kuzingatia Uhuru wa kuabudu nafikiri waziri yupo sahihi,Ni lazima tuwe na heshima kile anachokiamini mwengine na kukiabudu.. kufutwa kazi naona ni sehemu ya adhabu kwanza ni utovu wa nidhamu,pili inashusha hadhi na kuleta kero,dharau na ni upuuzi ambao hatuhitaji kuuchekea maana mambo ya dini ni moja ya kitu makini sana kwani kidogo tu amani na utulivu vinapeperuka!! Ni bora kuwa na tahadhari kabla ya hatari yenyewe.. kuharibu ni vyepesi kuliko kujenga.
 
Kuna watu humu wanavichwa vya hovyo sana! Hawaoni mifano ktk nchi nyengine namna dini zinavyowaumiza haswa pande mbili zisipo elewana!

Kupitia tukio hili kuna watu humu wameshaanza kutoleana maneno,hivyo hi ni moja ya athari ya tukio lile!

Mambo huanza kama tone lkn hujaza bahari.. mambo kama haya huwa yanahitaji hekima na si kujitapa ama kudhihaki!! Ni bora ukahoji kuliko kudhihaki!

Kama mtu unajiona wewe kwenye mambo ya dini huwezi mijadala na huwezi kuzizuia hisia zako ni bora ukapita ukaenda kwenye udaku! Dini sio sehemu ya mashindano hakuna kitu kama hicho!

Huyo jamaa anastahiri hiyo adhabu,Ni vyema tufahamu athari ya vitu tulivyonavyo na vyengine kama huviwezi ni bora kufungilia mbali upuuzi, nashauri wengine mpite kwa kusoma tu mambo ya dini yanahitaji hekima kubwa na haswa ya utambuzi ktk pande hizi mbili zote, saikolojia na ubongo unaowaza sahihi.
 
Back
Top Bottom