Kuna uhusiano gani kati ya supu na pombe?

Kuna uhusiano gani kati ya supu na pombe?

Ukipiga supu yako na chapati mbili halafu unashushia na Pepsi, Coke au sprite ya bariiiiiiiiidi..........ukiona ka nafasi kanaruhusu unaenda kuzimua na chupa zako mbili mambo yanakaa level

Umeulizwa uhusiano gani? na siyo mambo yanakaaje?
 
Pombe ni moja ya kichwaji kinacho sababisha mnywaji kukojoa sana. Kitendo cha kukojoa sana hupunguza kiasi cha maji mwilini hivyo kufanya damu kuwa nzito na hivyo kupunguza kasi ya mzunguko wake wa kawaida mwilini. Mnywaji wa bia mathalani anaweza kunywa bia moja halafu akakojoa kiasi cha chupa mbili za mkojo. Hivyo kadiri unavyokunywa ndivyo utakavyo kojoa zaidi hivyo kupunguza kiasi cha maji mwilini. Ukienda sehemu za pombe hasa baa utakuta wanywaji wenakojoa zaidi kuliko wanavyojisaidia haja kubwa. Yaani kwa ufupi baa zinaweza hata zisiwe na vyoo zikawa na sehemu ya kukojolea tu na kukawa hakuna tatizo.

Hali hii ya kukojoa sana ambayo hupunguza kiasi cha maji mwilini ndiyo husababisha mnywaji kuamka asubuhi akiwa mchovu sana hali ambayo huwa tumezoea kuiita "Hang Over" ambapo wengine hujisikia kama kichwa kuuma au kuwa kizito. Hii ni kwasabu mzunguko wa damu kwenda kichwani huwa mdogo kutokana na mzunguko mdogo wa damu unaosababishwa na upungufu wa maji mwilini. Sasa ili kumfanya mtu achangamke na kurudisha nguvu ndio utagundua wanywaji wengi hukimbilia supu ya kongoro au mchemsho ili kurudisha haraka maji mwilini kwani supu ina mafuta na maji ambayo hukaa mwilini na kuongeza nguvu hivyo kufanya damu kuwa nyepesi na kurudi katika kasi ya mzunguko wake wa kawaida. Vile vile utakuta wengi wanakunywa maji sana au soda kama pepsi ili kupata nguvu sababu soda zina sukari hivyo ni kama wanatumia badala ya Gluecos. Na kwakuwa wengi hunywa bila kula na wakisha kunywa hopoteza hamu ya chakula, hivyo wanakuwa hawana nguvu kutokana na njaa ndio maana utaona wanapoichapa supu asubuhi lazima huishushia kwa chapati ambazo huwa ndio mbadala wa chakula ambacho hawakula jana yake.

SIRI NYINGINE KUHUSU WANYWAJI: Kama wewe ni mfuatiliaji sana wa mambo ya kinywaji utagundua kuwa wanywaji wengi huwa hawaugui magonjwa mengi yatokanayo na maambukizo katika damu kama malaria. Hii ni kwasasabu wanapiga deki sana miili yao kwa kukojoa sana. Hivyo mara wakipata maambukizo huwa wanaflash out virusi vya magonjwa hayo kupitia kukojoa sana. Ndio maana kuna kitu kinaitwa Water Therapy. Yaani wewe ukijenga tabia ya kunywa maji sana mathalani lita tatu hadi tano kwa siku, unaweza kukuta unazuia na kuondoa magonjwa mengi mwilini magonjwa na watu wakashanga kuwa wewe una kinga ya magonjwa kama malaria. Hivyo wanywaji wa pombe wao bila kujua huwa wanafanya Water therapy kwa njia ya pombe. Hii ipo hadi kwenye magonjwa ya zinaa kama kisonono na kaswende. Mtu aliyekunywa maji mengi au bia anaweza kutembea na mtu mwenye ugonjwa wa zinaa halafu asiambukizwe kwa sababu yeye baada ya mchezo huenda kukojoa sana hivyo kufash out wale wadudu wa ugonjwa. Ukiona ameambukizwa labda awe amepata mchubuko. Ndio maana unaweza kukuta mtu ametembea na mtu mwenye ukimwi na asiupate na mwingine akaupata na watu mtaani wakabaki kushangaa. ONYO: Maelezo yangu haya yasikufanye uanze kunywa pombe wakati ulikuwa hunywi. Ila nakushauri kunywa maji kwa wingi kadiri uwezavyo ni tiba tosha.

Cha kwanza wewe unaonekana ni mhehe kwa kabila
Cha pili waonekana elimu yako ni kubwa sana. Una PhD ya unywaji( PhD in Drinking).
Cha tatu namuulizia ndugu yako 'Tulibaha 'hajambo?.
Cha mwisho,nashukuru kwa ufafanuzi.
 
Duh respect mkuu.....ngoja niwahi supu na chapati fasta maana mning'inio unanizingua
 
Watu wengi wanaokunywa pombe huwa ni wapenzi wakubwa wa supu, mtu akilewa usiku lazima asubuhi ataamkia kunywa supu kabla hajanywa chai. Sasa kuna uhusiano gani kati ya supu na pombe? Tujuzane.
Wengi hudhani supu ni dawa ya kuondoa pombe.
waswahili husema....
Supu si DAWA dawa ki kuacha Pombe.
 
Ukifuatilia wote wanaompata Tulimumu big up wana hangover.
 
Last edited by a moderator:
Tulimumu for President - 2015
Ha ha haaaaa mkuu! Ngoja na mimi nikae nyumbani halafu wana JF muandamane kuja kuniomba nigombee. Msisahau kuja na hela ya kutosha ya fomu na kampeni
 
Back
Top Bottom