Kuna uhusiano gani kati ubahili na Umaskini?

CHAKATI MKATO

Member
Dec 4, 2018
29
53
Habari wana jukwaa,

Kwa muda mrefu sana nilikuwa najiuliza hivi watu wanaotoaga ofa bar kwanini huwa hawaishiwi, au wanaotoaga misaada mikubwa pia kwa nini wanaendelea tu na maisha yao afu mimi ambaye sifanyi hivyo maisha yangu hayajabadilika kitu yapo vilevile.

Kwa muda mrefu sana nilikuwa mtu ambaye anatumia kipato chake kwa umakini mkubwa mno, kuna watu nalingana nao kipato ila wana matumizi makubwa sana sikuwahi kunua kwa nini hawaishiwi. Yaani kifupi nilikuwa sihongi, sinywi pombe sitoi misaada n.k

Sasa hivi karibuni nmeingiwa na mkono wa utoaji yaani nakuta na hela nayo inakuja hivyo hivyo yaani ni hela ambayo siitarajii ila inatokea tu hadi nashangaa. Sasa najiuliza kwavnini sikua napata kipindi cha ubahili vwangu ila sasa naipata nini kinafanya niipate hii hela? Je, kuna mtu humu hali kama hii imewahi kumtokea?
 
Pesa inavuta pesa, huwezi kupata pesa kama hutumii pesa, kama mbahili hata kuweza hutoweza uataogopa kupoteza pesa kwahiyo tumia pesa upate pesa, na kutoa kwa watu ni kama sadaka sababu unarahisisha maisha ya walu mungu nae anazidi kukuwezesha(hila usipitilize) kwani wepesi wa mwanadamu unakuja kupitia mwanadamu mwenzie, Mungu anakuwezesha zaidi kama unanyanyua wenzako maana wengi watanyanyuka kupitia wewe
 
Kuwa bahili kunaweza kuleta utajiri lakini sio ubahili bila akili.Unakuta unakuwa bahili kwenye pombe, kuhonga, na hata kuvaa lakini unapenda sifa mbele za watu kila mtu akilia shida kidogo unatoa hela, au unakuwa bahili kwenye hivyo vyote ila ukiona misosi uvumulivu unakushida,ukiamua kuwa bahili kuwa bahili kwenye kila kitu halafu hiyo hela unayoibana iingize kwenye kuzalisha ili izidi kuongezeka.
 
Kuwa bahili kunaweza kuleta utajiri lakini sio ubahili bila akili.Unakuta unakuwa bahili kwenye pombe,kuhonga,na hata kuvaa lakini unapenda sifa mbele za watu kila mtu akilia shida kidogo unatoa hela,au unakuwa bahili kwenye hivyo vyote ila ukiona misosi uvumulivu unakushida,ukiamua kuwa bahili kuwa bahili kwenye kila kitu halafu hiyo hela unayoibana iingize kwenye kuzalisha ili izidi kuongezeka...
Ubahili ni kitendo cha kutoa lakini uwezo wa kutoa upo ambapo umesikini huna kitu igawa unaweza kuwa na nia ya kutoa lakini huna! Hakuna uhusiano maana kutoa au kutotoa ni hurka na tabia.
 
TUMIA PESA IKUZOEEE

TUMIA PESA KUPATA PESA/TOA PESA UAPATE PESA

MBINU ZA UTAJIRI NI UBAHILI

:cool::cool::cool::cool::cool:
 
Habari wana jukwaa, kwa muda mrefu sana nilikuwa najiuliza hivi watu wanaotoaga ofa bar kwa nini huwa hawaishiwi, au wanaotoaga misaada mikubwa pia kwa nini wanaendelea tu na maisha yao afu mimi ambaye sifanyi hivyo maisha yangu hayajabadirika kitu yapo vilevile.

Kwa muda mrefu sana nilikuwa mtu ambaye anatumia kipato chake kwa umakini mkubwa mno, kuna watu nalingana nao kipato ila wana matumizi makubwa sana sikuwahi kunua kwa nini hawaishiwi. Yaani kifupi nilikuwa sihongi, sinywi pombe sitoi misaada n.k

Sasa hivi karibuni nmeingiwa na mkono wa utoaji yaani nakuta na hela nayo inakuja hivyo hivyo yaani ni hela ambayo siitarajii ila inatokea tu hadi nashangaa. Sasa najiuliza kwavnini sikua napata kipindi cha ubahili vwangu ila sasa naipata nini kinafanya niipate hii hela? Je, kuna mtu humu hali kama hii imewahi kumtokea?
Ee bwana umegusa mada ya msingi mno ambayo laiti tu watu waijue na waifuate. Kuna sheria ya utoaji na upokeaji huweza amini inafanya kazi kama 2+2=4,ukiweza kuifuata utakuwa tajiri mpaka uchoke.
 
Ukisoma uchumi, mbinu mojawapo ya kuwa tajiri ni kuwa mbahiri.
Naam ila ujuzi wa ubahili unaofundishwa kwenye uchumi siyo ubahili wa uchoyo...." rational and wise use of available resources so as to ensure efficiency and effectiveness"...
Ubahili unaozingumziwa umejikita sana kwenye " propensity".
Ubahili mwingine tunaouona ni ubinafsi tu na uchoyo.
 
unaombwa laki na una buku mfukoni je unacho?
Kuwa nacho ni tofauti kabisa na mfano uliotoa ndugu yangu. Mafanikio ni zao la matumizi sahihi ya vichache ulivyonavyo.Buku ndiyo inayokuja kuwa Trilion n.k.
"..The problem is how we use what we have and not the size"
 
Kwangu Mimi mtu Bahili naona kuwa anakipaji Cha pekee. Mimi huwa naamini kubania pesa Ni kudumaza mawazo kuwa hutapata nyingine. Hapa pesa ikipatikana inatumiwa bila ubahili.
 
Kuwa nacho ni tofauti kabisa na mfano uliotoa ndugu yangu. Mafanikio ni zao la matumizi sahihi ya vichache ulivyonavyo.Buku ndiyo inayokuja kuwa Trilion n.k.
"..The problem is how we use what we have and not the size"

Kabla haijawa trilion si bado buku mzee? swali lilikua tofauti ya ubahili na umaskini na umaskini Ni kutokua nacho au kuwa nacho kisichotosha
 
Back
Top Bottom