DOKEZO Kuna ufisadi wa kutisha MAMCU LTD

DOKEZO Kuna ufisadi wa kutisha MAMCU LTD

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
A

Anonymous

Guest
Ufisadi wa kutisha unaendelea kwenye Ushirika wa Korosho,Mtwara Masasi Union Co operative(Mamcu).

Kulipana Posho na Safari za nje

Viongozi wamekuwa walipwa posho bila kufanya kazi(Hewa] na Kutengeneza safari za nje ambazo hazina tija kwa ushirika Mfano Mwaka jana na mwaka huu wamefanya safari nakulipana Posho za kufuru wakati tangu wameanza kusafiri hakuna input yoyote zaidi ya chama kudidimia.

Ofisi ya Msimamizi [TCDC] imegeuza kichaka kwa maafisa wake kutengeneza mifumo ya kwenda kula pesa.

Kuna ushirika mkubwa kati viongozi wa chama na maafisa wa usimamizi Tume ya maendeleo ya ushirika. Kwahiyo wanakula wote hivyo ukiuliza Tcdc watakwambia kila kitu kipo sawa kumbe kuna uozo mkubwa wakulima wanaibiwa.

Mikopo iliyokidhiri

Chama kilichukua Mkopo benki Mil 600 kwenda kulima shamba la Ufuta wilayani nanyumbu kichekesho cha dunia.

Pesa karibu zote zililiwa na viongozi na kiasi kidogo kilienda kulima baadae matokeo wakapata Tani 10 sawa na Mil 15 wakati gharama tu za kuvuna huo uvuta ni Mil 10.

Sasa wamekuja na Mkopo mwengi wa Malori ya kusafirisha korosho kutoka benki hapo kuna upigaji Mkubwa.

Hoja kukopa sio shida lakini unatumiaje mapato yako?.Mfano mwaka wa fedha 2024/2025 Mapato yalikuwa Bil 6 unashindwaje kutengeneza mradi?.Matokeo yake Pesa zinaliwa baadae unaenda kukopa Mil 800.

Matumizi mabaya/Wizi wa Fedha za Mapato

Chama kina mianya mingi ya upotevu wa makusanyo kuanzia kwenye maghala mpaka mapato ya Ushuru.

Kumetengenezwa mifumo ya kupiga fedha za mmakusanyo. Mfano ukichukua tu kiasi cha makusanyo ukazidisha na Tozo hizo pesa hazijakusanywa na chama.

Madeni
Chama kimeendelea kutengeneza madeni yasiyo lipika ya muda mrefu wakati kila mwaka wanakusanya Mabilioni ya fedha.

Ushauri
1. Tunaomba ukaguzi maalumu tena kutoka CAG maana COASCO, TCDC wana mtandao wao hivyo ukiwatumia hauwezi kupata ukweli

2. Ofisi ya Mkuu wa Mkoa na Wizara ya kilimo kufuatilia kwa karibu Uovu huu maana Pamegeuzwa shamba la bibi.
 
ndugu yangu yaan vyama vya ushirika ndio chaka la kutobolea kimaisha we pambana upate nafas hapo na wewe upige mipesa

MAMCU ndio chama tajiri kwa sasa tanzania kwa vyama vya ishirika hata KNCU hakioni ndan
 
Back
Top Bottom