Kuna tofauti yoyote ya tabia na hatima ya hawa wawili: Miguna Miguna wa Kenya na Tundu Lissu wa Tanzania?

Dr Akili

JF-Expert Member
Aug 21, 2011
4,953
4,326
1. Wote wawili ni manguli wa sheria.

2. Wote wawili ni wanaharakati nguli waliojikita kuzichafua nchi zao kimataifa huko ughaibuni.

3. Wote wawili wamedhamiria kuwa marais wa hizo nchi zao.

4. Wote wawili wana passport za kusafiria za nchi za ughaibuni. Miguna ni ya Canada na Lissu ni ya Ubelgiji.

5. Ili kupata passport hizo za ughaibuni lazima upate uraia wa nchi hizo. Kwa sheria za nchi yetu ukifanya hivyo unapoteza uraia wa Tanzania. Kwa sheria za Kenya unaendelea kuwa raia wa Kenya (dual citzenship).

6. Kwa tabia zao hizo (unpatriotic and unruly behavior) Miguna Miguna haruhusiwi kukanyaga nchi ya Kenya na warning alerts zilishatolewa na serikali ya Kenya kwa nchi zote za Afika zilizo kwenye AU kutomruhusu Miguna Miguna kuingia nchi zao.

Desemba 2019 Tundu Lissu alijaribu kuja Tanzania kuhudhuria mkutano mkuu wa Chadema, akakwamia Nairobi.

Je, kuna uwezekano kuwa Tundu Lissu naye anayapata yale anayoyapata mwenzake Miguna Miguna? Na kama ni hivyo ataifanyaje kazi yake ya umakamu mwenyekiti wa chadema aliyopewa hivi karibuni na chama hicho?
 
Miguna alipoteza sifa zote za kuwa raia wa Kenya pale alipochukua uraia wa Canada, na ndio hicho kinachomsumbua kurudi nyumbani hadi leo. Katiba ya Kenya hairuhusu dual citizenship.@Dr Akili

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Miguna alipoteza sifa zote za kuwa raia wa Kenya pale alipochukua uraia wa Canada, na ndio hicho kinachomsumbua kurudi nyumbani hadi leo. Katiba ya Kenya hairuhusu dual citizenship.@Dr Akili

Sent using Jamii Forums mobile app
Kabla ya kuandika uongo jiridhishe kwa angalau ku Google.

Kenya wameruhusu dual citizenship kwa miaka kadhaa sasa. Kuanzia 30th August 2011.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Miguna alipoteza sifa zote za kuwa raia wa Kenya pale alipochukua uraia wa Canada, na ndio hicho kinachomsumbua kurudi nyumbani hadi leo. Katiba ya Kenya hairuhusu dual citizenship.@Dr Akili

Sent using Jamii Forums mobile app
Katiba mpya ya Kenya inaruhusu dual citzenship. Hivyo Miguna alikuwa na dual citzenship. Inawezekana uraia wake wa Kenya amefutiwa baada ya kuleta za kuleta kama ambavyo Tanzania nayo inawezekana imemfutia Tundu Lissu uraia wake wa Tanzania baada ya kuleta za kuleta.

 
Miguna awe rais wa kenya

Ebu kuweni serius kidogo basi. kenya kama wewe sio kikuyu au kabila lile la moi sahau kuwa rais.
Na Tundu Lissu eti awe rais wa tanzania. Ninakubaliana na wewe kweli watu hawako serious hata kidogo!
 
Tueleza ni lini Tundu Lissu alipata uraia wa Ubelgiji?
Wewe unadhani huko Amerika alikokwenda kutuchafua alisafiri kwa passport ya Tanzania? Unadhani huko Ubelgiji anakoishi sasa anaishi kwa permit/ vissa ya passport ya Tanzania? Kwa taarifa yako passport yake ya Tanzania ilishachukuliwa na mwenyewe na huyo mwenyewe ni serikali ya JMT ambayo kila kukicha alikuwa akiitukana. Watu kama nyie mnashindwa kuelewa kuwa demokrasia au upinzani si kutukana na kugombana na serikali iliyowekwa madarakani na walio wengi kila kukicha.
 
Wewe unadhani huko Amerika alikokwenda kutuchafua alisafiri kwa passport ya Tanzania? Unadhani huko Ubelgiji anakoishi sasa anaishi kwa permit ya Tanzania? Kwa taarifa yako passport yake ya Tanzania ilishachukuliwa na mwenyewe na huyo mwenyewe ni serikali ya JMT ambayo kila kukicha alikuwa akiitukana. Watu kama nyie mnashindwa kuelewa kuwa demokrasia au upinzani si kutukana na kugombana na serikali iliyowekwa madarakani na walio wengi kila kukicha.
Kumbe ni mambo ya kudhani
 
Back
Top Bottom