Kuna tofauti kati ya network ya kupiga simu na network ya internet?

Ziroseventytwo

JF-Expert Member
Mar 27, 2011
7,990
13,645
Simu infinix ina line ya tigo. Ikiwa kwenye 4G au 3G ukiipigia haipatikani. Hata kama umezima data. Ila ikiwa kwenye 2G simu ukiipigia inapatikana hata kama umezima data. Sasa nimeshindwa kuelewa hii kitu inakuwaje.

Naomba ufafanuzi kwenye hili.

Cc. reyzzap na Chief-Mkwawa
 
Kwa mim ninavyojua, simu ukiwa umeiset katka 4G only, ikipgiwa haipatikan, ila kwa 3G mawasiliano yanakuwepo kama kawaida!
 
Mkuu ina maana simu yako haina 3g/4G auto.

1. Simu ya kawaida Inatumia 2g kwa ajili ya kupiga
2. 3g sauti yake inaitwa HD voice lakini ili uipate kwa Tanzania inabidi muwe munatumia mtandao mmoja na wote muwe na simu za kisasa
3. 4g sauti yake inaitwa Volte na mitandao yetu mainstream hawana nafkiri smile walikua nayo.

Hivyo my guess simu yake inakaa 4g only ama 3g only mtu akikupigia inashindwa ku change kwenda 2g kupokea simu.

Possible solution
Bonyeza ##4636## Kisha ingia phone information Kuna box la network type utaona kuna option nyingi sana, Jaribu kuweka option ya

LTE/UMTS (auto PRL) kama picha inavyoonesha.
 
Mkuu,kwenye page ya pili katika comment yako umesahau kufuta IMEI..
 
mkuu, iset simu yako katika 2G, 3G and 4G auto detect! Vingnevyo utaendelea kutokupatikana kama simu yako unailazimisha kukaa kwenye 4G only!
 
Mkuu ahsante kwa ufafanuzi. Nimejaribu imekataa. Inaandika connection problem or invalid MMI code.
 
Mkuu ahsante kwa ufafanuzi. Nimejaribu imekataa. Inaandika connection problem or invalid MMI code.
Ina maana wameiblock hio code.

Ume Jaribu kwenda kawaida setting Kisha setting za network/connection Kisha kwenye mobile network ama cellular then network mode hakuna option ya lte/wcdma/GSM auto?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…