Kuna tofauti gani kati ya ushuru na kodi?

Kuna tofauti gani kati ya ushuru na kodi?

hapa ni shule tu. wahi shuleni usipoteze muda humu JF maana utapotoshwa na kuishia huko ulikopotoshewa. Unatakiwa kupata dozi ya dhana/nadharia, masuala mahsusi, mifano halisi, na elimu kwa vitendo katika masomo ya public finance, corporate finance, taxation (theory/practice/law), na pengine DS. Kupata maarifa hakuhitaji short cut, vinginevyo utaishia kuwa kama akina Lugumi & Co.[/QUOTE

Kwa hiyo kila kitu unaachotaka kujua hapa duniani lazima ukasome? Umeme ukasome? Madawa ukasome? Magari ukasome? Kilimoukasome? Kufua ukasome? Kutumia simu nako ukasome baada ya hapo hakuna wa kumuuliza mwenzie.
 
Kusoma ni njia ya kujifunza. Ndiyo ukitaka kuelewa jambo lolote sharti ujifunze. hakuna njia ya mkato.
 
Sijaomba
English translation nataka maana
Kodi ni kiasi kinacholipwa kwa Mamlaka bila kuwa na kiasi cha thamani unachopewa/unachopata toka aliyelipwa hiyo kodi(non exchange transanction) hata hivyo hiyo mamlaka inaweza kutoa huduma kadhaa ambazo zinaweza kuwa pungufu ya kiasi ulicholipa au kikazidi kiasi ulicholipa,ushuru,ada mamlaka hutoa huduma ambayo anayeitumia hupaswa kuilipia kama anayetumia huduma stendi ya mabasi hupaswa kulipia ada fulani,anayetumia soko hupaswa kulipa ushuru,anayeyumia nyumba ya mtu mwingine kwa shughuli yoyote hupaswa kulipa pango(rent),anayetumia chombo cha usafiri cha mtu mwingine hulipa nauli na kadhalika,
 
Jamani naombeni msaada wa maana halisi Kati ya kodi na ushuru, tumekuwa tukisumbulia sokoni na serikali ya kijiji wakidai ushuru wakati mwingine wakidai kodi..naombeni msaada wenu tofauti halisi.
Na jaribu na kukimbia: KODI ni malipo ya maalum yanayotokana na mapato ya mtu. USHURU ni malipo yanayotokana na bidhaa.
 
Hapa Hakuna hata bavicha mmoja atakayeleta majibu sahihi.

Ila ukiwaambia watukane sasa watakushushia mvua ya matusi.

Kodi ; Hukusanywa na Serikali kuu kupitia wakala wake TRA.

ushuru; Ni zao la sheria ndogo ndogo zinazopitishwa na halmashauri husika.

Anayekusanya ni halmashauri za miji husika.
 
Hapa Hakuna hata bavicha mmoja atakayeleta majibu sahihi.

Ila ukiwaambia watukane sasa watakushushia mvua ya matusi.

Kodi ; Hukusanywa na Serikali kuu kupitia wakala wake TRA.

ushuru; Ni zao la sheria ndogo ndogo zinazopitishwa na halmashauri husika.

Anayekusanya ni halmashauri za miji husika.
Ok ushuru wa forodha unakusanywa na Halmashauri?
 
Back
Top Bottom