Kuna tofauti gani kati ya ushuru na kodi?

Dnashon

Member
Feb 19, 2016
58
33
Jamani naombeni msaada wa maana halisi Kati ya kodi na ushuru, tumekuwa tukisumbulia sokoni na serikali ya kijiji wakidai ushuru wakati mwingine wakidai kodi..naombeni msaada wenu tofauti halisi.
 
Ushuru ni tozo zinazotozwa kwenye bidhaa au huduma. Mfano kuna tozo za mazao ya misitu, vinywaji n.k. Ila kodi ni tozo ambazo inatozwa taasisi husika. Mfano Corporate tax, capital gain tax. Hata Vat pia ni kodi japo hii inatozwa kwenye bidhaa kama kodi ya mauzo...
 
Tunaweza kusema, ushuru wa kuagiza gari ni aslimia 50% au ushuru wa kuingiza wine ni 10% kwa lita moja lakin tunasema, kodi ya faida ya kampuni ni asilimia 25... So kampuni inaweza kulipa ushuru tofauti tofauti kulingana na bidhaa lakini kampuni kama kampuni yenyewe mwisho wa mwaka ikitengeneza faida inalipa kodi moja ya faida...
 
hapa ni shule tu. wahi shuleni usipoteze muda humu JF maana utapotoshwa na kuishia huko ulikopotoshewa. Unatakiwa kupata dozi ya dhana/nadharia, masuala mahsusi, mifano halisi, na elimu kwa vitendo katika masomo ya public finance, corporate finance, taxation (theory/practice/law), na pengine DS. Kupata maarifa hakuhitaji short cut, vinginevyo utaishia kuwa kama akina Lugumi & Co.
 
zote hizo ni kodi ni maneno tofauti hutumkia kuzitofautisha kodi ni fedha yeyote ambayo serikali inakusanya au kuchukua kutoka kwetu( kisheria) kwa ajili ya kufanya shuguli yeyote iwe ya kiuchumi au kimaendeleo hiyo huitwa kodi kwa ujumla sasa kuna tofauti ya kulipa kodi

1 kutoka moja kwa moja katika mifuko yetu ambapo fedha huenda moja kwa moja katika mfuko wa serikali centro gov hii huitwa TAX (kodi)

2 nyingine ambapo fedha inatoka mfuko wako na kisha inakwenda mfuko mwingine local gov na kisha katika mfuko wa serikali hii huitwa LEVY (ushuru)

3 kuna kodi nyingine hutozwa mipakani huitwa DUTY hii ni kodi inayotozwa mipakani kodi hiii inayolipwa juu ya bidhaa au mambo ambayo unaweza kimwili kuyagusa
 
Nikweli Ila ukitaka kurudi shule kwa Kila kitu usichokijua utapoteza muda zaidi. Kumbuka kuuliza SI ujinga.. Humu jukuwani Kuna watu waelewa na wanamsaada mkubwa Sana so isibeze mchango wao. Tafasili Yao imenijenga zaidi ya ushauri Wako. Rudi shule ukaelimike vizuri
 
hapa ni shule tu. wahi shuleni usipoteze muda humu JF maana utapotoshwa na kuishia huko ulikopotoshewa. Unatakiwa kupata dozi ya dhana/nadharia, masuala mahsusi, mifano halisi, na elimu kwa vitendo katika masomo ya public finance, corporate finance, taxation (theory/practice/law), na pengine DS. Kupata maarifa hakuhitaji short cut, vinginevyo utaishia kuwa kama akina Lugumi & Co.
Jibu swali Au pita tu
Mbwembwe za nini Sasa?
Jamaa yuko sokoni anataka kujua tofauti ya
Kodi Na ushuru.Unataka akasome taxation?
WTF
 
hapa ni shule tu. wahi shuleni usipoteze muda humu JF maana utapotoshwa na kuishia huko ulikopotoshewa. Unatakiwa kupata dozi ya dhana/nadharia, masuala mahsusi, mifano halisi, na elimu kwa vitendo katika masomo ya public finance, corporate finance, taxation (theory/practice/law), na pengine DS. Kupata maarifa hakuhitaji short cut, vinginevyo utaishia kuwa kama akina Lugumi & Co.

Hizo mbwembwe zako za maandishi umemsaidia mleta uzi?

Msomi gani wewe ambaye umesomea hayo mambo, but still huna uwezo wa kumuelezea layman in a simple language akapata japo ABCs za mada husika?

Kilaza mkubwa we. Nyie products za 'Big Results Now' mna matatizo sana upstairs!
 
Maarifa ni gharama ndugu. Usitake kutumia maarifa na utaalam bila kulipia, isipokuwa kwa kusoma. Amua leo uende shule. Kutafuta na kutumia maarifa hakuna kuchelewa, ila ujinga utakuchelelwesha. Kwa asiyeweza kutafuta maarifa na kuyatumia kupitia njia za kawaida (kusoma) ninamshauri amwone mtaalam mshauri wa masuala ya kodi (sheria za kodi) amsaidie. Ila haitakuwa bure; kuna gharama za ushauri. Huo ndio mfumo wa ubeberu unavyotuhitaji kuishi. ...angalieni mnakojikwaa sio pahali mnakonagukia!
 
zote hizo ni kodi ni maneno tofauti hutumkia kuzitofautisha kodi ni fedha yeyote ambayo serikali inakusanya au kuchukua kutoka kwetu( kisheria) kwa ajili ya kufanya shuguli yeyote iwe ya kiuchumi au kimaendeleo hiyo huitwa kodi kwa ujumla sasa kuna tofauti ya kulipa kodi

1 kutoka moja kwa moja katika mifuko yetu ambapo fedha huenda moja kwa moja katika mfuko wa serikali centro gov hii huitwa TAX (kodi)

2 nyingine ambapo fedha inatoka mfuko wako na kisha inakwenda mfuko mwingine local gov na kisha katika mfuko wa serikali hii huitwa LEVY (ushuru)

3 kuna kodi nyingine hutozwa mipakani huitwa DUTY hii ni kodi inayotozwa mipakani kodi hiii inayolipwa juu ya bidhaa au mambo ambayo unaweza kimwili kuyagusa
Na stamp duty vipi mkuu?
 
Kodi huanzishwa kwa Muswaada unaopelekwa na kuridhiwa na Bunge ( Act) mf VAT Act
Ushuru ni ule unaopitishwa na Taasisi husika na kuridhiwa na Mamlaka ya eneo husika mf. Serikali za Mitaa.
Kodi hutumika Country wide, Ushuru ni wa eneo husika na huenda ikawa inatofautiana kati ya eneo na eneo.
 
Jamani naombeni msaada wa maana halisi Kati ya kodi na ushuru, tumekuwa tukisumbulia sokoni na serikali ya kijiji wakidai ushuru wakati mwingine wakidai kodi..naombeni msaada wenu tofauti halisi.
Kodi ni zaka/fungu la kumi=lazima utoe
Ushuru ni sadaka= kutoa ni hiari
 
Back
Top Bottom