killo
JF-Expert Member
- Jul 13, 2008
- 401
- 94
Wakuu habarini na poleni na majukumu ya kila leo
Rejelea kichwa tajwa hapo juu naleta kwenu ili nijiweke sawa kati ya vifaa hvyo hasa kwenye matumizi.
Kwa upande wangu nahitaji sana kuvitumia ili kubadilisha madhari na kuboresha usikivu wa music kisasa zaidi. Moja ya ya changamoto ktk hili uimara wa kuweza kuhimili haya maisha yetu ya kibongobongo.
Ipi brand nzuri inayoweza kuhimili umeme wetu huu, naimani umeme mnaujua vema.
Nawasilisha
Asanteni
MKuu ngoja nijitahidi kukuelezea hizi vitu at the easiest way possible.
Sub-woofer: Ni speaker inayopiga sauti ya Bass peke yake. Toka zamani sub-woofer zilikuwepo ila tu zilikuwa zinachanganywa na spika nyingi kwenye Box moja. Kwa kadri teknolojia ya sauti ilivyozidi kukua, ikagundulika kwamba pia kuna uwezo wa kuitenga(kuiweka pekeyake) spika ya bass ilikuweza kupata mkito bora zaidi.
Home Theater: Ni system tegemezi ya kuendesha pia kutawanya sauti kutoka kwenye chombo kingine. Home theater pia ili iweze kuitwa hivyo lazima iwe na mkusanyiko wa sipika za aina mbali mbali kama Sub-woofer, spika za kati, na spika za tweeter.
Kwahiyo: Subwoofer ni sipika itowayo sauti ya Bass tuu na yenyewe kama yenyewe haichezi kitu mpaka iunganishwe na kitu kingine... Sijui Umeelewa?
Kuhusu uimara: Kwa kweli ni matumizi yako, Kwa umeme, ziku zote uwe na protection kwa vyombo vyako. Lakini pia katika hivi vyombo kuna swala zima la matumizi ya nyumbani na matumizi ya biashara... Sasa ukinunua chombo cha matumizi ya nyumbani ukakitumia kwenye matumizi ya biashara, hakitakaa sana kitaharibika tuu. Ndiyo maana kuna Kuna vyombo vya kupigia mziki wa biashaya na mziki wa majumbani.
Natumaini sijakukwaza na maneno yangu mengi kama mganga wa kienyeji..!!!