Kuna tatizo gani kwenye hii picha?

Indume Yene

Platinum Member
Mar 17, 2008
2,950
711
Kuna tatizo kwenye hii picha, as msomaji jaribu kungalia ni kitu gani ambacho unaona kina kasoro.
Karibu.

03.JPG
 
Kwani caption yake ikoje? Au haieleweki ni nani mfadhili hapo kati ya Bridge of Hope and Stanbic bank? Au kasoro ni kuwa na mtu mwenye unene wa afya mbovu? Yawezekana kasoro unayo wewe mwenyewe kwenye kufanya photo interpretation!!
 
Kama Kikwete alikuwa anachekelea wakati alipokwenda kuangalia uharibifu wa Mabomu ya Gongo la Mboto, itakuwaje wanaopeleka msaada washindwe kupige vigelele!

Stupidity @ work!
 
Hao inaonyesha walikuwa wanatoa msaada kwa wenye shida/mahitaji kisw issue . Naona wanacheka labida ndo tatizo
 
Tatizo ninaloliona hapo ni furaha na matabasamu walionayo wahusika kanakwamba wanapokea tuzo au kombe baada ya kuibuka washindi kwenye mashindano fulani.Nadhani misaada ingekuwa inakabidhiwa direct kwa walengwa na sio wanasiasa ambao always they want photos and to make headlines kwenye media.
 
Kama hao wote ni watoa misaada, tatizo lipo kwenye hao wanaopokea maana wote kwa dhahiri sio waathirika bali ni kama vibosile fulani wanaouza sura kwa kutoa na kupokea hiyo misaada.

Pili hapo ni kuwa wanatangaza biashara za hao wazalishaji wa hizo bidhaa. Hii inatokana na kukosekana kwa standard za vifungashio bidhaa katika nji hii. Maana kwa kiroba kama hicho huwezi kutambua kama ni cha unga, mchele au chokaa bila ya kusoma hizo chapa; vile vile huwezi jua kama ni ndoo ya mafuta au rangi bila kusoma hayo mabandiko.

Ni maoni yangu binafsi.

Nawasilisha.
 
Tunaona makampuni yanapokwenda kutoa hiyo misaada, wanakwenda na mabango yenye nembo na majina ya makampuni yao. Je kwa wale waliotoa misaada yao personally waliwekewa mabango gani?
Je kuna ulazima wa kutangaza msaada wako kwa kuweka bango la kampuni yako? Mbona hatukuona bango la Shirika la Msalaba Mwekundu, Hospitali ya Muhimbili, na makanisa? Naombeni kufahamishwa kama kuna ulazima wa kutumia mabango kuwasadia wenzetu.
 
Back
Top Bottom