Kuna shida ya uongozi kwenye nchi yetu

Awamu hii ipo kwenye kumdiscredit magufuli tu.

They have nothing tangiable to offer.

Wapo busy kutuonesha mwenda zake this mwenda zake that ..... hii inatusaidia nini. Yeye ameshakufa na fungu lake halipo. Ni ukosefu wa akili ... . Haina maana kwa Sababu there is no means kwamba atarudi na kujutia. Kila rais anamakosa yake , JK Anamakosa yke na aliharibu nchi, mkapa ana makosa yake , Nyerere ana makosa .... hivyo haina maaana. Na suala la kifo ni suala la Muda , kila mtu atakufa ... sio suala la kumcheka Mtu

Hawaviongozi ni wahuni they neeed to be serious
 
Uyo alikuwa nyonya damu alifuga vijana ambao ni majambazi waliokuwa wanaiba huku wamevaa suti

Na hii ndio shida kubwa . Nimewahi kusema hatujapata wapînzani Serious. Yaani wanatakiwa Lissu kama 10 walio Serious then CCM inatoka
 
Kati ya kosa kubwa ambapo wenye wamewahi fanya ni kuacha ccm itawale KWA miaka lukuki Hadi leo!!!wangeandaa chama mbadala ccm kingejifunza mengi na mitandao ya kifisadi isingekuwepo!

Nakubaliana na Wewe hili ni kosa kubwa sana na litatugharim. Yaani mpaka vizazi vya sasa vinaamini Rais lazima watoke CCM .

HIi Kitu
 
Wanasiasa wa nchi hii wengi wanaonesha hawana MENTAL STRENGTH na MATURITY.

Alianza na yule wa TANESCO, badala ya kutuletea solution ya matatizo ya mgao wa umeme , alisikika akisema matatizo ya umeme ni kutokana na utawala ulipita kushindwa kuboresha vyema mifumo.

Hii ni lack of Maturity na huenda tukawa tunashangilia, lakini hawa watu ndio chelewesho la maendeleo na tafsiri sahihi ni kuwa hawana jipya na ni Blah Blah na majungu yasiyo na tija .

Akaja mwingine kusema TTCL was a failure kwa kulazimisha watumishi, hii ni cheap mind nyingine ambayo haina solution zaidi ya kuelezea matatizo.

Tuletee solution na mapendekezo ya kuboresha shirika otherwise ni failure nyingine ya awamu hii na nikuwapotezea muda wa Tanzania.

Tutaendelea kuwa ni watu wa kuelezea ambayo tunaamini ni makosa ya mwendazake hadi lini ? Tunatakiwa kuja na mapendekezo chanya au kuja kuuambia umma kuwa hiki kilikosewa na utawala uliopita?

Je, tutafanya hivyo for how long , Na je ipi ni tija kwa kufanya hivyo ? Ipi ni faida yake ...... hii ndiyo inaitwa lack of mental strength and maturity.

Kwa muktadha huo , njia pekee ambayo inaweza kuwa ni solution ya kuleta maendeleo TZ ni kufanya complete remission ya hiki chama kwenye UTAWALA.

CCM haina muendelezo wa nchi na maendeleo; Kila kiongozi anaekuja madarakani anakuja na philosophy yake inayodumaza yote yaliyofanyika nyuma.

Lack of Continuity kwenye nchi yetu ni tatizo sugu linalotuchelewesha sana.
Kwa mfano, Miradi ya barabara haina proper Supervision from the top dog mpaka sasa.

Nikianza na barabara ya mbagala , Chang’ombe , Karume, temeke etc etc zote ni hazipitiki zaidi ya mwaka huku maelezo yakinifu juu ya kwanini barabara hizo mpaka sasa hazijakamilika hayapo clear. How come kipande cha magomeni hadi karume kichukue mwaka? How come kipande cha Karume hadi Chang’ombe kichukue mwaka?

Huwezi kuwa Rais wa kusaini makaratasi, bila ya kwenda field na kuona changamoto za watendaji na kutizama kodi za wananchi zinatumika vipi ... ? Mfumo wa nchi yetu haupo AUTOMATED, hivyo RAIS ni lazima afanye meddling kwenye mambo mengi ya maendeleo yanayotafuna kodi zetu.

Nashauri utoe mapendekezo yatakayokwenda kuufanya mfumo wa vyama vingi kuwa THABITI na namna bora ya kupata KATIBA MPYA itakayokwenda kufanya nchi yetu kupata viongozi wa machaguo yetu.

Hakuna namna tutakayoacha au kusahaulishwa kutamka KATIBA MPYA.

Muda sahihi wa KATIBA MPYA ndiyo huu.

Katiba mpya itakwenda kufanya mfumo wa vyama vingi kuwa THABITI na kutuletea maendeleo ya kizazi chetu .

Chaguo ni letu na Tanzania ni yetu!
Ni nani atafanya nini kupiga kelele na kuuamsha utawala uliopo kuhusu suala la Katiba Mpya kama viongozi wa Upinzani sasa wamebakia kujipendekeza kwa utawala uliopo?
 
Mwanzoni,
Umeanza vizuri Sana kuuchambua uzi wako,

Katikati
ukaingiwa mihemko ukaingiza uchama, na upuuzi mwingine nje ya mada yako.

Mwishoni,
Ukaharibu kabisa kuingiza maswala ya usimba na uyanga kwenye maswala muhimu ya kitaifa.

Kwa mantiki hiyo,
Ushaur na mapendekezo yako vimekosa sifa ya kupokelewa na kushughulikiwa na wahusika
Kwa kusoma comment yako tu umessumarize alichokisema na nimeelewa japo sijasoma maana uzi wakr n mrefu, anyway kazi iendeleee
 
Awamu hii ipo kwenye kumdiscredit magufuli tu.

They have nothing tangiable to offer.
Awamu hii ni ya CHADEMA, CUF, ACT na wapinzani kwa ujumla au ni ya CCM!!!????
Watanzania wenye uelewa mkubwa na wenye mapenzi mema na hili taifa tulipokuwa tukisema na kuandika kuwa tunahitaji katiba mpya, wewe na wenzako mlitutukana kwa vile mlikuwa jikoni.
Leo kwa kuwa aliyekuwa anakupa ugali hayupo na ananyang'anywa hata yale mazuri machache aliyoyafanya,unaona hii awamu haitendi haki.
Mwarobaini wa haya yote ni wale wote wenye mapenzi mema na nia thabiti ya kuona Tanzania ikipiga hatua kubwa kimaendeleo tukija pamoja na kuungana na kutengeneza mfumo (katiba mpya) ambao utaileta hiyo Tanzania mpya yenye neema ambayo kila mwananchi atafurahia kuwa sehemu ya jamii yake.
 
Ungeweka mkataba wa ujenzi Ili tuone kama ilitarajiwa zikamalike kwa kipindi gani, hapo tungekuelewa. Je, ulikuwepo wakati wa ujenzi wa awamu ya kwanza ya mwendokasi?
Mafanikio na matatizo yaliyopo nchini lazima yawahusu chama kilichopo madarakani.
Ndio ile mazuri yahusishwe na chama, lakini mapungufu na mabaya ndio ile kauli 'wapinzani walituchelewesha sana'
 
Hawa ilikuwa wavalishwe overall waingie field kabisa wakajionee tatizo la sivyo watakuwa wamekaa ofisini tu na kusubiri umbea

Huyo wa kwanza alikuwa kamiss kuzunguka na Chopper akatafuta sababu na kuja na zero solutions

Huyo mwingine nae akaona bora na yeye amkandie marehemu lakini ajue lile Jua lililompiga siku ile na vumbi kwenye viatu bado tunakumbuka
 
Siasa ni ahadi tu
Uongozi ni maono na utekelezaji.
Hivi tukae kutegemea wanasiasa wafanye Mambo ya uongozi .
Kwa uelewa wang mdogo kama wapo hawafiki 5%.
Deal makers wanaongoza nchi kila sekta. Mkuu angalia yako Mana ukiwaamsha waliolala R.I.P ww 😁😁
 
Mtoa mada anahoja sana kuhusu maendeleo yetu.
Ila nini kifanyike ndio hatuelewi,
Ni kweli hoja za serikali ni dhaifu kujitetea kwa wananchi na ni italeta madhara sana 2025.
Tukikumbuka tukio la tetemeko la ardhi kule bukoba, Marehemu JPM alijibu ''jukumu la serikali ni kujenga miundi mbinu ya kuwafanya wananchi waitumie kama fursa za kujiletea maendeleo na sio kuwaletea chakula''.Miundo mbinu hiyo ni vituo vya afya, shule, na barabara.
Tunashuhudia mambo mengi ni kama wananchi hatuonewi huruma na serikali mfano hiyo barabara, mkandarasi hana nia njema na watendaji wamejinyamazia tu kimya.
Yaani barabara inafumuliwa kipande kirefu halafu kinawekwa kifusi kinamomonyookaaa akipata hela tena anarudia kuweka kifusi pale pale tena na tena.na hawajali kuwa kuna sisi wenye gari ndogo yaani ni kifusi tu kwenda mbele.karume hadi magomeni ,
Nilisikia malengo ya mwenye nchi ni kujenga bara bara zenye hadhi ya changarawe kwenye hotuba za mwanzo mwanzo.nilikata tamaaa, tulishazoea kiwango cha lami au zege.(kama kule njombe).
Huyu mkandarasi wa karumevmagomeni na mbagala kurasini ameshindwa kujenga kipande kifupi fupi ili tusipate tabu ya kufumuliwa barabara?hapana nia njema hapa CCM wabaneni viongozi wenu.
Tukija mbezi hadi kibaha bado kukamilika?
Tukija kwenye pantoni ni kusubirishwa na mfoleni mrefu bila sababu,
Mwendo kasi kila leo wanatoka kwenye malengo yao, mara waende kibaha, mara waende makongo mbezi, mara magari mengine yanakuja kusaidia usafiri.ni shida tupu na taharuki kwa wateja wa kwenda posta.
Lakini mara serikali itawajengea nyumba wanaohama kwenye hifadhi ya ngorongori, KWELI hizo ni kazi za serikali?
Usalama wetu,
Wizi mitaani imezidi sana, watu wanatobolewa fremu zao za biashara na wengine wanachomewa moto, mateja wamerudi kwa kasi sana.
Elimu,
Majibu ya form four yametoka muda tu selection bado, naona linaandaliwa tatizo la selection kutoka karibu na kufungua shule ili wazazi wapanic,
Tarura na tanroad hawana muda wa kukagua barabara wao wameingia tenda za kuchora michoro na kuzibua mitaro, hapa wanalenga fedha kutumika na CCM wakija kustuka hawana hata km za KUSHAWISHI kuhusu ujenzi wa barabara nchini dhidi ya marehemu.
TRA waneacha kutangaza mapato ya kila mwezi na msigwa naona anapata tabu sana kuisemea serikali kwa yaliyotekelezwa ni afadhali apangiwe kazi nyengine asione aibu kutangaza vitu ambavyo wengine tunaona Abbas mungu alijivunia kipindi kile.
Nawaomba watendaji mfikilie kwa kina hizi PANIC zinazoandaliwa mapema kabla ya 2025.vyenginevyo mtabezwa mmefanya nini harafu mtabaki hamna majibu zaidi ya kutaka kumuonyesha marehemu ni mbaya kumbe nyie wenyewe mnapenda virahisi vigumu hamvishiki.
Fuatilieni malengo ya nchi, kwa kila ngazi,
CCM waambieni wenye viti wenu waendeshe mikutano ya kijiji na muone muhtasari ya malalamiko yao kwenye maeneo ya shule, afya, maji safi na barabara.
Mi binafsi ni mkazi wa mikoa mitatu nazunguka na najionea mikwamo iliopo.
 
Back
Top Bottom