Kuna shida ya uongozi kwenye nchi yetu

Megalodon

JF-Expert Member
Apr 9, 2021
1,910
3,311
Wanasiasa wa nchi hii wengi wanaonesha hawana MENTAL STRENGTH na MATURITY.

Alianza na yule wa TANESCO, badala ya kutuletea solution ya matatizo ya mgao wa umeme , alisikika akisema matatizo ya umeme ni kutokana na utawala ulipita kushindwa kuboresha vyema mifumo.

Hii ni lack of Maturity na huenda tukawa tunashangilia, lakini hawa watu ndio chelewesho la maendeleo na tafsiri sahihi ni kuwa hawana jipya na ni Blah Blah na majungu yasiyo na tija .

Akaja mwingine kusema TTCL was a failure kwa kulazimisha watumishi, hii ni cheap mind nyingine ambayo haina solution zaidi ya kuelezea matatizo.

Tuletee solution na mapendekezo ya kuboresha shirika otherwise ni failure nyingine ya awamu hii na nikuwapotezea muda wa Tanzania.

Tutaendelea kuwa ni watu wa kuelezea ambayo tunaamini ni makosa ya mwendazake hadi lini ? Tunatakiwa kuja na mapendekezo chanya au kuja kuuambia umma kuwa hiki kilikosewa na utawala uliopita?

Je, tutafanya hivyo for how long , Na je ipi ni tija kwa kufanya hivyo ? Ipi ni faida yake ...... hii ndiyo inaitwa lack of mental strength and maturity.

Kwa muktadha huo , njia pekee ambayo inaweza kuwa ni solution ya kuleta maendeleo TZ ni kufanya complete remission ya hiki chama kwenye UTAWALA.

CCM haina muendelezo wa nchi na maendeleo; Kila kiongozi anaekuja madarakani anakuja na philosophy yake inayodumaza yote yaliyofanyika nyuma.

Lack of Continuity kwenye nchi yetu ni tatizo sugu linalotuchelewesha sana.
Kwa mfano, Miradi ya barabara haina proper Supervision from the top dog mpaka sasa.

Nikianza na barabara ya mbagala , Chang’ombe , Karume, temeke etc etc zote ni hazipitiki zaidi ya mwaka huku maelezo yakinifu juu ya kwanini barabara hizo mpaka sasa hazijakamilika hayapo clear. How come kipande cha magomeni hadi karume kichukue mwaka? How come kipande cha Karume hadi Chang’ombe kichukue mwaka?

Huwezi kuwa Rais wa kusaini makaratasi, bila ya kwenda field na kuona changamoto za watendaji na kutizama kodi za wananchi zinatumika vipi ... ? Mfumo wa nchi yetu haupo AUTOMATED, hivyo RAIS ni lazima afanye meddling kwenye mambo mengi ya maendeleo yanayotafuna kodi zetu.

Nashauri utoe mapendekezo yatakayokwenda kuufanya mfumo wa vyama vingi kuwa THABITI na namna bora ya kupata KATIBA MPYA itakayokwenda kufanya nchi yetu kupata viongozi wa machaguo yetu.

Hakuna namna tutakayoacha au kusahaulishwa kutamka KATIBA MPYA.

Muda sahihi wa KATIBA MPYA ndiyo huu.

Katiba mpya itakwenda kufanya mfumo wa vyama vingi kuwa THABITI na kutuletea maendeleo ya kizazi chetu .

Chaguo ni letu na Tanzania ni yetu!
 
Mwanzoni,
Umeanza vizuri Sana kuuchambua uzi wako,

Katikati
ukaingiwa mihemko ukaingiza uchama, na upuuzi mwingine nje ya mada yako.

Mwishoni,
Ukaharibu kabisa kuingiza maswala ya usimba na uyanga kwenye maswala muhimu ya kitaifa.

Kwa mantiki hiyo,
Ushaur na mapendekezo yako vimekosa sifa ya kupokelewa na kushughulikiwa na wahusika
 
Kati ya kosa kubwa ambapo wenye wamewahi fanya ni kuacha ccm itawale KWA miaka lukuki Hadi leo!!!wangeandaa chama mbadala ccm kingejifunza mengi na mitandao ya kifisadi isingekuwepo!
 
Nikianza na barabara ya mbagala , Chang’ombe , Karume, temeke etc etc zote ni hazipitiki zaidi ya mwaka huku maelezo yakinifu juu ya kwanini barabara hizo mpaka sasa hazijakamilika hayapo clear. How come kipande cha magomeni hadi karume kichukue mwaka? How come kipande cha Karume hadi Chang’ombe kichukue mwaka?
Ungeweka mkataba wa ujenzi Ili tuone kama ilitarajiwa zikamalike kwa kipindi gani, hapo tungekuelewa. Je, ulikuwepo wakati wa ujenzi wa awamu ya kwanza ya mwendokasi?
 
Katiba mpya hiihii ambayo wanaoipigania wakialikwa chai ikulu wanaachana nayo?
 

Similar Discussions

15 Reactions
Reply
Back
Top Bottom