Habari wadau,
Kama kichwa kinavohoji, nimekuwa nikijiuliza kinyesi cha mwanadamu kina nini? Mazingira ya vijijini ambapo watu hujisaidia maporini ni kawaida kukuta mbwa au nguruwe wakisaka vinyesi vya binadamu. Binafsi nimeshuhudia Mara nyingi kwa wanyama tajwa yaani kitimoto na mbwa wakifurahia kinyesi. Wataalam wa mifugo Wanasema nguruwe akila kinyesi cha binadamu ni rahisi kupata minyoo aina ya Taenia solium. "Cyst" au mayai ya minyoo hiyo husafiri kwenye mfumo na kutengeneza vipele vyeupe kwenye nyama. Nguruwe ni carrier wa vijidudu hivyo kwa sababu kiafya havimdhuru ila hiyo nyama ni hatari kwa binadamu. Madhara mojawapo ni ugonjwa hatari wa kifafa ambapo katika stage za juu hautibiki.
Baada ya ufafanuzi huo naomba wataalamu waniambie kwa nini hawa wanyama tajwa hula kinyesi cha binadamu na c ya wanyama wengine? Huwezi kumkuta mbwa au nguruwe akila kinyesi cha ng'ombe, mbuzi, mbwa na wanyama wengineo. Kuna madini lishe gani katika kinyesi cha binadamu?
Nawasilisha
Sent using
Jamii Forums mobile app