Kuna nini kati ya Mheshimiwa Rais Magufuli na Ludovick Mwananzila?

Freed Freed

JF-Expert Member
Jun 27, 2017
6,230
6,471
Halo JF.

Rais Magufuli ktk moja ya vikao vya ndani ya chama cha CCM, amemlaumu Naibu waziri wa zamani wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, na aliyewahi kuwa pia RC Tabora ndugu Ludovick Mwananzila kwa kumwita mwenye tamaa nyingi sana.

Mwananzilia alishika nafasi ya unaibu waziri ktk awamu ya kwanza ya Kikwete na mkuu wa Mkoa ktk awamu ya pili baada ya kukosa ubunge mwaka 2010.

Rais Magufuli anamlaumu Mwananzila kwa kuwa baada ya kukosa ubunge 2010 aliteuliwa mkuu wa Mkoa lakini 2015 kwa tamaa zake alirudi tena jimboni kwake kuomba ubunge ilihali ana cheo kikubwa serikalini. Alifika mbali kwa kusema Mwananzila hafai hata kuwa Katibu Tarafa na ndiyo maana kampoteza kabisa. Aliwaambia wajumbe wakafanye kazi bila woga.

Je ni kwamba hivi sasa RC, DC, DAS, RAS, Makatibu na Manaibu katibu mkuu wizara na wakuu wa idara wakigombea ubunge watapoteza nafasi zao na kuonekana wenye tamaa? Je wakishindwa ubunge wajiandae kutafuta kazi nyingine?

Vp kuhusu Katibu mkuu wa wizara anayenyemelea Ubunge jimbo la Iramba Magharibi ataonekana ana tamaa akijitosa kugombea na atapoteza ukatibu ikiwa ameshindwa?

Je kuna kuhitilafiana kwingwine kati ya Rais na Ludovic Mwananzila au ni kugombea tu ubunge 2010 na 2015 na kushindwa kote na kuonekana mwenye tamaa sana?

 
Back
Top Bottom