China anahitaji malighafi ambazo zimezagaa katika ardhi ya Tanganyika, wakati huo huo CCM ndio chama cha Mwalimu Nyerere.
Mnakumbuka historia ya urafiki wa China na Tanzania wakati huo wa Mwalimu?
China wameamua kuurudisha urafiki huo uliofifia baada ya kuona "viongozi" waliopo madarakani kuchoshwa na mabepari wa US na Ulaya kuingilia "mambo ya ndani"/ domokrasia na utawala bora,utawala wa sheria.
CCM pia wanahitaji kuonesha "maendeleo" kwa wananchi ili waweze kutangazwa tena kuwa ni washindi kwa ushindi wa kishindo utakapoitishwa "usanii wa" uchaguzi mkuu 2015. Kwa bahati China ana hela za kumwaga za miradi.
Hali hii inafanya, inapelekea China na CCM kuwa "ndugu wa damu".
Mtaani wanasema,"Nipe, nikupe/ au Kula,nikule".
Kwa ufupi,CCM anapata anayoyataka na China anapata anayoyataka. Mchezo unaendelea.
Lakini ukaribu huu wa CCM(Tanzania) na China unawachukiza wakoloni mabepari na mabeberu cowboy. Huenda hawa wanywa damu na wapenda dhahabu na wese wakatutengenezea bonge la "dhoruba", ni kawaida yao.
Wale wenye kumbukumbu za operations,"reconcur/recolonization" wataelewa nini tutarajie kutokea.