Pigo tena kwa muziki wa Bongo Fleva baada ya ripoti kusema, M To The P aliyekuwa na Mangwea jijini Johannesburg naye amefariki dunia.
Taarifa kutoka Johannesburg zinaeleza M To The P amefariki dunia baada ya kulazwa katika hospitali ya St Helen Joseph ambayo mwili wa Mangwea umehifadhiwa.
Mangwea na M To The P walisafiri pamoja hadi Afrika Kusini kwa ajili ya kufanya onesho (show) na baadaye waliendelea na maisha, lakini jana Mangwea alikutwa amefariki dunia chumbani na M To The P akiwa taabani na kulimbizwa hospitalini.
"Kweli amefariki dunia, ni yule mwenzake na Mangwea, sasa tuko kwenye pilikapilika ya kuandaa mazishi," alisema Thomas, mmoja wa Watanzania wanaoshughulikia suala la mazishi.
Nadhani kwa wale ambao walikuwa hawamuelewi Lady Jay Dee nadhani jibu mmeanza kuliona. Hawa Jamaa wa Clouds wanaojifanya radio ya watu wana watu wao ambao wao wanapenda wawe wanasikika tuu . na kama mnabisha fanyeni research mtagundua wasanii wa THT wanapata kiasi gani cha airtime pamoja na wale ambao wana tow the line.
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.