Kuna mwana JF amesoma ''The Urantia Book"?

Hujajibu hapo kipengere cha 2

Mungu ni neno la hadithi za kutungwa????????? Are serious , dictionary gani imetafasiri hivyo au Ni mafikirio yako
Kama Mungu si hadithi ya kutungwa tu, unaweza kuthibitisha huyo Mungu yupo kweli nje ya hadithi za kutungwa tu?
 
Nimekuuliza kitu, hujajibu.

Kwenye faith unaweza kuamini chochote, unaweza kuamini mavi yako ni Mungu.

Je, ukiamini mavi yako ni Mungu, imani hiyo inafanya mavi yako yawe Mungu?
Ngoja waje wa kunya hapa watatujibu😋😋
 
Asante nitafanya hivyo,
Ni kampuni kubwa ya uchapishaji wa vitabu
 
Nimesoma nikasoma Kisha nikasoma tena nikaona mbona sifiki mwisho Hebu kwanza niangalie nakaribia kumaliza au? Nikaanza kuscroll nikascroll Kisha nikascroll tena na tena Kisha nikafika mwisho nikakuta BILGERT amekulima dislike nimecheka Sana.

Wabongo hatupendi kujichosha asee!! Huu mkeka mrefu bongo na marekani.
 
Hapa swali lako linajipinga moja kwa moja mkuu. Ukishaamini mavi yako kuwa Mungu maana yake umeshaamini mavi' ndiyo Mungu,swali la kweli au siyo kweli linakufa maana tayari umeamini mavi ndiyo Mungu.
Je, ukiamini mavi yako ni Mungu, imani hiyo inafanya mavi yako yawe Mungu?
Au kwako wewe Mungu ni nini?
 
Mkuu mimi sina njaa ya kupendwa na mtu JF.

Ndiyo maana naweza kutoa mawazo ambayo hayapendwi na watu wengi, kama kukataa uwepo wa Mungu, au kutetea haki za mashoga.

Mtu anayependa kupendwa hawezi kutoa mawazo kama yangu hapa JF.

Mimi napenda uhuru wa kujieleza ninavyofikiri kuliko ninavyotaka kupendwa na watu.

Kwa hivyo, mtu mjinga akinipa dislike, mimi nafurahi tu, kwa sababu najua ninawaza tofauti na mjinga.
 
Hapa swali lako linajipinga moja kwa moja mkuu. Ukishaamini mavi yako kuwa Mungu maana yake umeshaamini mavi' ndiyo Mungu,swali la kweli au siyo kweli linakufa maana tayari umeamini mavi ndiyo Mungu.

Au kwako wewe Mungu ni nini?
Tatizo unaishia kwa mtu mmoja wakati mimi swali langu liko universal.

Ukiamini wewe ni Samia Suluhu Hassan, rais wa Tanzania, mwanamke, wakati hilo si kweli, wewe ni Satoh Hirosh, mwanamme, hiyo imani yako inakufanya kweli uwe Samia Suluhu Hassan ?
 
Ok,

Turudi kwenye msingi wa swali lako ulilomuuliza jamaa hapo juu,kabla ya kutoa mfano ulipaswa uto tafsiri ya Mungu ni nini Kisha ndiyo uulize swali.

Mungu ni Nini?
 
Kama Mungu si hadithi ya kutungwa tu, unaweza kuthibitisha huyo Mungu yupo kweli nje ya hadithi za kutungwa tu?
Acha kuruka ruka jibu swali, nipe kwanza maana ya Mungu na Mimi nikuonyeshe Mungu isijekua unakomaa kupinga kitu usichokielewa.
 
Bravia.
 
Ok,

Turudi kwenye msingi wa swali lako ulilomuuliza jamaa hapo juu,kabla ya kutoa mfano ulipaswa uto tafsiri ya Mungu ni nini Kisha ndiyo uulize swali.

Mungu ni Nini?
Mungu ni hadithi wanayojipigia watu kama chaka la kufichia maswali magumu wasiyo na majibu yake, au kujipa matumaini kwamba kuna figure fulani ita wa protect, au kujiaminisha kuna siku watu watapewa hukumu baada ya kifo, waliotenda thawabu wapewe mbingi na waliotenda dhambi wapewe moto, au kukandamiza wengine kwa kufanya kama wanavyotaka wao kwa kupitia chaka hilo la Mungu. Au kujidunga ulevi wa mashairi yasiyo na mipaka kusema kila kitu ni Mungu na Mungu ni kila kitu.

Nje ya hizo hadithi za kujiaminisha wenyewe, hakuna Mungu.

Na mimi nilianza kulimulika hili hususan kwenye Mungu wa imani na falsafa zinazosema kuna Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote, aliyeumba ulimwengu.Kwa sababu huyo ndiye Mungu anayeeleweka na wengi na aliye rahisi kabisa kuonesha kimantiki kwamba hayupo.

Nimetoa muktadha huu kitambo tu, kama sehemu ya kuanzia. Ni wewe tu hujafuatilia mjadala.

Sasa wewe unammua na kumkubali Mungu gani ambaye unaweza kusema yupo kwa uthibitisho nje ya hadithi tu?
 
Sawa lete reference ya hicho ulichokiandika apo

Kabla sijakutwanga swali zaidi

Naona unaaandika mafikirio yako na sio jibu la swali!!!
 
Mungu ni hadithi wanayojipigia watu kama chaka
Unafanya kosa lile lile la awali,nililiona huko juu ukimjibu mtu hivi. Inakuwaje Mungu kuwa hadithi? Hii ndiyo tafsiri ya Mungu kwa mtu aliyekuuliza swali ili apate kufahamu Mungu ni nini?
Sawa,hii ni tafsiri ya wanaoamini katika Mungu,bado wewe hujatoa tafsiri yako ya Mungu ni nini.
Hapa unatembea katika mdundo wa watu fulani ambao mimi siwajui na mwishowe umehitimisha kutoa shutuma dhidi yao.
Nimetoa muktadha huu kitambo tu, kama sehemu ya kuanzia. Ni wewe tu hujafuatilia mjadala.
Nawezaje kuamini kitu ambacho sijapata tafsiri sahihi kutoka kwako Ila umetoa maelezo marefu yanayoshutumu watu fulani ambao hawapo katika mjadala?
Sasa wewe unammua na kumkubali Mungu gani ambaye unaweza kusema yupo kwa uthibitisho nje ya hadithi tu?
Bado hujatoa tafsiri ya Mungu ni nini ila umeongeza msamiati mwingine ambao unahitaji kufafamuliwa pia.

Hadithi ni nini kwa Mujibu wa maelezo yako ili nipate tafsiri sahihi ya Mungu?

Baada ya kunijibu,naomba unipe tafsiri ya Mungu ni nini mkuu.

Asante.
 
Sawa lete reference ya hicho ulichokiandika apo

Kabla sijakutwanga swali zaidi

Naona unaaandika mafikirio yako na sio jibu la swali!!!
Kama unanipinga na kusema Mungu yupo, thibitisha Mungu yupo.

Mimi reference yangu ya kwanza kuhusu kutokuwepo kwa Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote ni Epicurean Paradox.
 
Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…