Kuna mwana JF amesoma ''The Urantia Book"?

Sawa.

1.Kuna vitu vipo, na vinathibitishika kuwa vipo. Hivi tunapata uhakika kwamba vipo, havina tabu.
2. Kuna vitu havipo, kimakosa vinathibitishika kuwa vipo. Hivi tunapata uhakika wa uongo kwamba vipo.
3. Kuna vitu vipo, na havithibitishiki kwamba vipo. Hivi tunataka kuvichunguza na kuvihakikisha kwamba vipo tupate uhakika kwamba vipo.
4.Kuna vitu havipo, na havithibitishiki kwamba vipo au havipo, kwa sababu havipo, na kama havipo, havithibitishiki kuwa vipo au havipo, kwa sababu falsafa ya kuthibitisha kiuhalisia (other than logical proofs such as proof by contradiction) ni kwa vilivyopo, visivyopo havithibitishiki, kwa sababu havipo.

Sasa, umetoa hoja nzuri, kwamba kushindwa kuthibitisha kitu hakumaanishi kitu hakipo. Inawezekana kitu kipo, lakini hakithibitishiki tu. Hili nalielewa na nimelielezea mara kadhaa hapa.

Lakini je, utajuaje kitu kipo, na hakithibitishiki tu, na si kwamba hakithibitishiki kuwa kipo kwa sababu hakipo?

Kabla ya uthibitisho, utajuaje tofauti?

Hatutakiwi kukubali tu kwamba kitu kipo ila hakithibitishiki tu, kwa msingi huo, mimi naweza kukuambia kwamba mimi ndiye Mungu, ila wewe kwa akili zako za kibinadamu huwezi kuthibitisha hilo, utakubali?

Zaidi ya hilo, pingamizi langu kuhusu uwepo wa Mungu si tu kwa sababu wewe huwezi kuthibitisha Mungu yupo.

Pingamizi langu kuhusu uwepo wa Mungu, hususan huyu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote ni kwamba, hoja ya uwepo wake ina internal contradiction. Uwepo wa Mungu huyu ni sawa na mtu akwambie katika Euclidean planes, kuna pembetatu ambayo hapohapo ni duara, wakati unajua pembetatu na duara ni vitu tofauti, na haiwezekani kuwapo pembetatu ambayo hapohapo ni duara.

Kwa hivyo, ninapokupa mtihani wa kuthibitisha uwepo wa Mungu, tayari najua huwezi kuthibitisha Mungu yupo.

Mungu huyu hayupo, si kwa sababu wewe huwezi kuthibitisha yupo (tushaona kuna vingine hatuwezi kuvithibitisha lakini vipo, inatuchukua miaka mingi kuvithibitisha), lakini, Mungu huyu hayupo kwa sababu dhana ya kuwepo kwake ina internal contradiction.

You can either have an omnipotent, omniscient and omni benevolent God, or have a universe in which evil is possible.You can't have both logically. The two are mutually exclusive.

And since we have a world in which evil is possible, by using the very definition of people who believe God exists, then that God does not exist.

1. Ni muhimu kuweza kuthibitisha kitu kipo, hata kama kutoweza kuthibitisha kitu kipo hakumaanishi kitu hakipo.

2. Namba 1 hapo juu ni muhimu ili tujue kwamba hatuamini kitu kipo wakati hakipo. Kwa sababu, tukisema tu kitu kipo ila hatuwezi kukithibitisha, inawezekana ikawa hatuwezi kukithibitisha kwa sababu hakipo, tukaamini kipo, wakati hakipo.

3.Muhimu zaidi, sitegemei wewe kushindwa kwako kuthibitisha kwamba Mungu yupo kama uthibitisho wangu kwamba Mungu hayupo. Uthibitisho wangu kwamba Mungu hayupo unatokana na problem of evil/ Epicurean Paradox.Wewe kushindwa kuthibitisha Mungu yupo nakuonesha umeshindwa kuthibitisha Mungu yupo kwa sababu hayupo, si kwa sababu nyingine.

Sijui kama umenielewa.
 
I will let Eli Walach talk for me.

"When you have to shoot, shoot. Don't talk."

 
Huyo Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote, kuumba ulimwengu ambao watu kumjua ni shida sana, wanabishana, wanapigana vita, wanauana, kwa sababu za dini na kushindwa kukubaliana kuhusu uwepo wake, huoni kwamba ni contradiction?

Huoni kwamba huyo Mungu angekuwepo, kwa jinsi alivyo mwema, alivyo mjuzi na muweza wa yote, angejiweka wazi kwa kila mtu, kila mtu amjue bila utata, tusihitaji mtume wala msahafu, kila mtu amjue tangu anazaliwa kwa kuwekewa habari zake zote kwenye DNA isiyoharibika, kiasi kwamba watu wote wa dunia wamjue Mungu wa kweli, atuepushe na mizozo isiyoisha kuhusu uwepo wa Mungu?

Hivi, huoni kuwa that is the logical thing kwa Mungu huyo kufanya, instead of kujificha asijulikane vizuri, watu wakauana mamilioni kwa mamilioni, kutokana na vita za kidini?

Huoni kwamba, logically tu, kuwapo kwa dini tofauti, migogoro ya kidini, sintofahamu nyingi, na hata hii mijadala ya kujadili uwepo wa Mungu, ni ushahidi kwamba huyo Mungu hayupo, kwa sababu angekuwepo, mjadala kuhusu uwepo wake usingewezekana kuwepo, kwa kuwa kila mtu angejua Mungu yupo bila utata?
 
Majibizano hayawezi kufika muafaka kama mnajadiliana kwa imani.

Kwa sababu imani haina kanuni, mtu anaamini anachoamini tu, halazimiki kufuata kanuni.

Lakini kama tunaamua kufuata logic na facts, tunaweza kufikia makubaliano kwamba Mungu- kwa kuanzia mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote- hayupo.

Kwa sababu tunaweza kuonesha logically, kwa proof by contradiction, kwamba Mungu huyo hawezi kuwepo, by using the problem of evil and the Epicurean Paradox.
 
Akina nicola tesla hawa
 
Za Biblia, Quran, vitabu vingi vya dini, zako wewe.

Ndiyo maana mpaka sasa hujathibitisha Mungu yupo.

Ukibisha, thibitisha Mungu yupo nje ya hizo stories.
Huwezi kuthibitisha uwepo wa Mungu kwa kutumia Logical Mind mkuu,since it is very LIMITED,maana utapaswa kutumia only five senses.

Je unajua kuwa kuna more than five senses? Then you have to go beyond the mind via yoga ama Meditation to explore the presence of God ama higher mystical spiritual consciousness which is UNLIMITED.
 
Ukikataa logic, umekubali chaos.

Yani, umekubali ulimwengu ambao:-
1. Mungu yupo.
2. Mungu hayupo.
3.Mungu yupo na hayupo kwa wakati huohuo.
4. Mungu yupo na hayupo kwa wakati huo huo, lakini hilo linamaanisha yupo.
5. Mungu yupo na hayupo kwa wakati huohuo, lakini hilo linamaanisha hayupo.
6. Hayupo ni yupo, Mungu hayupo, na hilo linamaanisha yupo.
7. Yupo ni hayupo, Mungu yupo, na hilo linamaanisha hayupo
8. Mungu yupo kama hayupo.
9.Mungu hayupo kama yupo.
10.Yote hayo ya juu kwa pamoja.
 
Kama unanipinga na kusema Mungu yupo, thibitisha Mungu yupo.

Mimi reference yangu ya kwanza kuhusu kutokuwepo kwa Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote ni Epicurean Paradox.
I gat you ngoja nikuitie sipana Leo hadi akili ikukae sawa naomba twende nukta after nukta sitaki urukeuruke, wewe mzee wa epicurus philosophy kumbe unatumia Epicurean paradox ntakupangulia moja baada ya nyingine na Leo ndio utakua mwisho wako kuwasumbua watu humu
 
Umeielewa kwanza?

"When you have to shoot, shoot. Don't talk"

 
Nishamtia za uso uko hadi kani-ignore,

Post in thread 'Maisha ya Hussein Jumbe ni ushuhuda tosha kwamba jamii zetu zina wachawi, watu wenye roho mbaya sana na makatili. Tuwe na Imani kwa Mungu' Maisha ya Hussein Jumbe ni ushuhuda tosha kwamba jamii zetu zina wachawi, watu wenye roho mbaya sana na makatili. Tuwe na Imani kwa Mungu
 
HIcho hapo
Asante sana mkuu.Japo kina page nyingi sana,na inaonekana ni kigumu sana,ni km kitabu kimoja kinaitwa Summa Theologica,kiliandikwa na Mt.Thoma wa Akwino,nacho ni kikubwa sana na ni kigumu balaa.
 
kuna pembetatu ambayo hapohapo ni duara, wakati unajua pembetatu na duara ni vitu tofauti, na haiwezekani kuwapo pembetatu ambayo hapohapo ni duara.
Wewe utawashinda wajinga wajinga tu kwa hizi hoja zako uchwara
 
Kuna hiki kingine. Kinaonesha fix zilizomo katika hicho kitabu cha Urantia.

Bahati mbaya the PDF is too large to upload here

Urantia: The Great Cult Mystery.

Author(s): Martin Gardner

Publisher: Prometheus, Year: 2008

ISBN: 1591026229,9781591026228



Description:
Well-known skeptic and acclaimed popular science writer Martin Gardner presents a complete history of the Urantia movement, from its beginnings in the early 20th century to the present day. In addition to providing an outline of the Urantia cult's worldview, Gardner presents strong evidence to establish the identity of the man whose trancelike orations formed the basis of the book. Gardner also analyzes the flaws in Urantian science and points out many instances of plagiarism in various sections of the book.In a new postscript to this paperback edition, Gardner details recent developments in the Urantia movement, corrects some errors in the original edition, and responds to critical reactions from Urantia believers to his skeptical perspective on the book and the movement.Although there are other histories of The Urantia Book, this is the only one written by a skeptic. Anyone interested in the New Age, cults, or the development of new religions will find much fascinating material in Gardner's thorough overview.
 
Mkuu wewe mbona kichwa chako nikigumu kuelewa Nimekuuliza tunatumia logic ipi kupata maana sahihi ya Neno Mungu ?

We unasema wa biblia na Qur'an Mimi sijauliza Mungu gani nataka maana ya Mungu
Mboka akili yako Ni nzito sana!!

Ukishindwa waombe msaada kina scar wakusaidie.
 
Nimekwambia Mungu ni hadithi tu, hayupo, kila utamaduni unatunga hadithi yao ya Mungu, sasa unataka maana gani?

Yani unataka nikwambie Mungu yupo anakaa mbinguni wakati hayupo?

Nimekwambia kama unabisha thibitisha Mungu yupo.

Umeshindwa.

Kwa sababu hayupo.
 
Haya thibitisha kuwa maana ua neno Mungu Ni hadithi bila kuacha shaka yoyote?

Kumbe Erick shigongo huwa anatunga Mungu nzuri sana za kusisimua sivyo
 
Asante sana mkuu.Japo kina page nyingi sana,na inaonekana ni kigumu sana,ni km kitabu kimoja kinaitwa Summa Theologica,kiliandikwa na Mt.Thoma wa Akwino,nacho ni kikubwa sana na ni kigumu balaa.
vitabu vikubwa ndio vina madini ,pg,8000 soma pg 80 daily siku 100 kimeisha
 
Mungu yupo...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…