Kuna mtu hafikiri vizuri na italigharimu taifa

kibaravumba

JF-Expert Member
Dec 21, 2012
6,634
7,010
Unaweza Ku imagine mtu kajeruhiwa damu inatoka puani na mdomoni,halafu wewe unakuja kuzuia damu isiendelee kutoka kwa vile itaisha.Wazo lako ni zuri.Ila unapoziba pua na mdomo ili kufanikisha lengo lako,Huyo mtu akifa kwa kukosa pumzi,utarudi kutuomba msamaha licha ya nia yako njema?Utashangiliwa na watanzania wasiofikiri vizuri na wengine wangefurahia hata Huyo mtu anayetoka damu afe tu tukose wote!Lakini kumbuka waliomtoa damu mtu wetu ni watu wako wa karibu na unapaswa pia kuwashughulikia.
Kuna mtu hapa hafikiri vizuri,na iko siku watanzania watajuta zaidi kuliko wanavyojuta sasa.Ukipewa nguvu tumia na akili kupiga mpira.Usilenge goli la adui ukiwa golini kwako,maana ukikosea kidogo mpira unakufunga wewe.Cheza Mpira kwanza usitazame goli.Kuna watu watafanya kazi ya kufunga.Sasa hivi beki wewe,kipa wewe,kiungo wewe, mshambuliaji wewe!Utafumga kweli goli?
 
Kama ungepanga kwa paragraphs, basi paragraph ya mwisho noma sana!
 
ameshasema yeye ndo rais, tumuachie kila kitu nawala hapangiwi au haingiliwi katika maamuzi, we unaumiza kichwa bure
 
Unapoamua kuleta thread acha kutumia lugha ngumu kama hii kwanini usiwe kama Ney bhana!!!!
 
Haya mambo bwana mh! Hivi ukiruhusu wimbo wa Ney wakiibuka mamia wakapsaza sauti ile ile utarudi kumats Ney ili uwakamate na hao wengine au utawaachia kusema hizo ni kelele za mlango?
 
Mleta uzi mbona unajificha nyuma ya keyboard yako, huku kiwiliwili kipo nje?
 
Duh cjui ndo huyu
 

Attachments

  • 20170328_200034png.png
    20170328_200034png.png
    183.7 KB · Views: 18
Mada inaelea hii...ni kama sehemu ya mjadala mrefu ambao hauko hapa. isijekuwa mtoa mada umepotea njia toka whatsap
 
Back
Top Bottom