Kuna mtu anakaribia kuingia 18 za Serikali, Magufuli hatanii....

Kuna mtu anakaribia kuingia 18 za Serikali, Magufuli hatanii....

Tume ya Katiba

JF-Expert Member
Joined
Apr 6, 2012
Posts
4,896
Reaction score
1,866
Wadau,

Kwa mujibu wa maneno ya JPM ya leo inaonekana kabisa, kwa sasa kansa kuu ni huu upotoshaji wa takwimu, na kwa muktadha huu ni kwamba kuna mtu muda wowote kuanzia sasa ataingia kwenye 18 za JPM, walio karibu nae mtu huyu wamfikishie salamu kuwa atakapo pewa data zozote toka kwa watu "wasiojulikana" kama siri za serikali atafute vyanzo vingine kuthibitisha kabla hajarusha kwenye hadhira.......

Katika wakosoaji wanaoogopwa na serikali nyingi duniani ni wale wenye taaluma za sheria au wale ambao wanasoma na kufuatilia ripoti, takwimu, vitabu au makala mbali mbali. Lissu, Zitto,Slaa, Lipumba(Enzi zake), Lamwai (Enzi zake) na wengineo wengi ni mifano ya aina hiyo... kwa wanasheria sababu ipo very clear wapo makini sana kwenye yale wanayozungumza na wanajua kuwa ni ngumu kuwashida Mahakamani, kwa watu aina ya Zitto, slaa et al. pamoja na kuwa sio wanasheria ni watu ambao wanasoma sana vitabu, makala na machapisho na matokeao ya takwimu mbali mbali, watu hawa huwa ni wabaya sana kwa kuwa wakosoapo hutumia takwimu na rejea mbali mbali....Hakuna serikali makini duniani kote itakuacha salama ikiwa ukosoaji wako "hata kama ni kweli " lakini unalenga kuzua taharuki katika jamii...Hakuna..Hakuna...


Kitakachomkuta asije kusema hatukumkumbusha. Ni wajibu wangu kama Mzalendo wa nchi hii kumkumbusha mtu yoyote ninayeona anaelekea kuingia kwenye hatari itakayosababisha taharuki kwenye jamii.

Tumpe muda JPM atimize azma yake kwa watanzania, na kama hatatimiza ahadi zake msema kweli ni Box la kura 2020.

Wenu

Tume ya Katiba
Mtakwimu Mwandamizi
 
Aisee! Wacha movie iendelee. Ngoja wengine tuwe watazamaji.
 
Sio mara ya kwanza kwa Mh Rais kusema kuwa kuna watu walichukua fedha ili kusaidia upande wa wezi wa rasilimali zetu...leo hii tena ameonya juu ya wanaopiga kelele ili kuwaridhisha waliomhonga anawafahamu.
 
Huyo JPM kwani yeye hana ndugu? Na yupo tayari kwao hata panya asiguse? Huyu alishasema yeyote atakayehusika na kifo chake hata panya hawatabaki kwao. Ni kufa ukoo mzima. Kama anajiamini JPM amfanyizie mtu huyo.
 
mmm sijakupata Mkuu au ni VITISHO vinavyoletwa kutokana na ukosefu wa haki na wajibu ?sasa mkuu hapa unamtahatharisha nani?serikali inaogopa nini kama wanaongoza nchi kwa kufuata utawala bora?na hawa W/blowers ni muhimu mno katika jamii.
 
Back
Top Bottom