Kuna mfano wa Mandela duniani?

Ushimen

JF-Expert Member
Oct 24, 2012
39,981
96,235
Nelson Mandela daima alitajwa kama 'kiongozi mkongwe wa dunia' ambaye alikuwa na ujuzi wa kutatua matatizo ya kidunia. Sifa yake ya madili mema ilimfanya kuonekama kama mrithi wa Mahatma Gandhi. Nani sasa anaweza kuchukua majuku ya Mandela?

Maswala ya Lockerbie, Burundi, DR Congo, Lesotho, Indonesia, Israel-Palestine, Kashmir, Mauaji ya Stephen Lawrence, uhamasisho wa Ukiwmi na kombe la dunia.

Orodha ya mambo aliyoyaweka karibu naye Mandela ni ndefu.

Katika baadhi ya mizozo kama mgogoro wa muda mrefu nchini Burundi alikuwa mpatanishi.

Maswala kama Ukimwi, alikuwa mwanaharakati na baba aliyepoteza mwanawe kwa maradhi hayo.

Mchango wake ulikubalika na ukakaribishwa sana.

Alipinga kuingiliwa kati mzozo wa Kosovo mwaka 1999 na kukosoa sera ya kigeni ya Marekani, wakati huo uhusiano wake na Kanali Gadaffi na aliyekuwa Rais Suharto haukuchukuliwa kwa wema.

Wengi walihisi kuwa alichelewa katika harakati zake dhidi ya ukimwi nchini Afrika Kusini.

Lakini wakosoaji wake wanakubali kuwa alikuwa kiongozi asiyekuwa na mfano wake duniani.

Alikuwa kiongozi ambaye watu walikuwa na matumaini naye, mtu ambaye alitoa mfano wa kuigwa duniani.

Mandela alionekana kama mtu aaliyweza kukabidhiwa majukumu na kuyafanya kwa kuzingatia ukweli kwani safari yake Jakarta ambako mwanasiasa wa Timor Mashariki alikuwa amezuiliwa mwaka 1997 ilipelekea kufanyika kwa kura ya maoni na kuachiliwa kwa mfungwa huyo Gusmao miaka miwili iliyofuata.

Alikuwa na maadili ya hali ya juu sana ambayo yanaweza kuwa funzo kwa wanasiasa wote duniani wasiokuwa na mwelekeo mwema na yote yalitokana na vita vyake dhidi ya utawala wa kibaguzi miaka ya themanini.

Kumekuwa na marais wengine wakongwe lakini wao walikuwa watu ambao siasa zao zilihusu maswala ya ndani ya nchi zao.

Mfano Jimmy Carter alitumwa Korea Kaskazini kuzungumzia maswala muhimu na pia amekuwa akijihusisha na maswala ya demokrasia barani Afrika lakini hana hisia alizokuwa nazo Mandela kuhusiana na maswala kadhaa kama Mandela alivyokuwa.

Tony Blair alijaribu kujihusisha na juhudi za upatanisho Mashariki ya kati lakini wengi waliona kama alikuwa anajaribu kujifutia historia mbaya aliyo nayo kuhusu vita vya Iraq.

Lakini jambo ambalo litasalia vichwani mwa wengi ni Mandela alipoamua kutangaza kuwa mwanawe amefariki kutokana na Ukimwi mwaka 2005. Hii ilikuwa mapema wakati ambapo Ukimwi ulikuwa umekuwa donda sugu Afrika Kusini. Mandela aliwataka wananchi wa taifa hilo kuweka wazi maswala ya Ukimwi.

Unaweza kwenda popote duniani na picha yake na hakuna asiyemfahamu . Hakuna mfano wa Mandela. Aung San Suu Kyi labda kidogo anaonekana kuwa kama Mandela lakini sio rahisi kwake kutambulika kama alivyotambulika Mandela.

Gandhi, Mandela na Suu Kyi walikuwa wafungwa wa kisiasa na kujitolea kwao kwa jamii ilikuwa sehemu kubwa ya maisha yao.

Wakati wa sherehe za kuzaliwa kwake alipokuwa na umri wa miaka 89, Mandela alibuni kikundi cha viongozi wakongwe aliowataka kuendeleza amani duniani.

Dunia inahitaji mtu mpole, mkarimu na wa kujitolea. Bila ya watu kama Mandela kuna uwezekano wa dunia kutumbukia katika migogoro ambayo haitapata wasuluhishi na kwa mtizamo wa wengi ni vigumu kupata mfano wa Mandela duniani.

1463637522668.jpg
 
SIna haja ya kusoma mengi san uliyaandika , kifup utkua umesmifia Nelson Mandela umejiona hakuna wa kumfananisha nae, ila nadhani ungeanza kusema nani anafana na Mwl Julius Kambarage Nyerere kwa Fact moja inayomcrtitisize Nelson Mandela .,, Kwa historia kuna watu wengi sana waliku nyuma ya Nelson Mandela katika kuiokumboa Africa Kusini na wenye impact kubwa kuliko sana kuliko yeyel, pia kumbuka ukombozi w S.A haukua ukombozi wa moja kwa moja bali ulikua ukombozi wa Mazungumzo ya kukubali waaburu kushika Uchumi huku Waafrika kusini weusi kushika siasa kitu ambacho hatukiwezi kukuiita ni Ukombozi .
 
Kwa wanaharakati wa ukombozi haa Stive Biko yupo juu hawa kuuawa kwao ndio kulileta chachu ya kutokomeza ubaguzi South Africa...Kaburu aliumiza sana kichwa kwa huyu mtu...Stive Biko na wengineo walikua wengi mkuu Mandela hakuzuka tuu.wapo waliokua na misimamo Tata Madiba anaachwa mbali..
 
Kuna hotoba moja ipo humu Jamii forum , ni hoyub aliyowahi kuihutubia Raisi Mzungu wa Africa Kusini ,kua Watu weusi tutabaki kua Raw Material za Watu weupe dunia , nguvu ya huyu mtu kusema maneno mabaya kiasi hicho yalitokana na hari ndogo na uwoga ulikua umewaajaa waaAfrica kusini wakti wa Ukombozi wa nchi yao , na ndio maana walikubali ukumbozi kw akipande kidogo cha mazungumzo .. chukueni siasa , tuchukue uchumi , sidhani kama kuna zaidi ya 20% ya mtu mweusi wa S.A wanaomiliki Investment ya maana , wote ni Makaburu.
 
Mkuu mandella mengine inawezekana upo sahihi ila swala la uwoga Wa south hawana kabisa tena kabisa kama unaangalia true story ya Stive biko au wengineo wakiadhibiwa Cape Town museum kisa kuavha kwa makusudi kipande ilihali ile Nchi yao wewe hapa unasema waoga...
 
Stive Biko ndie aliewaamsha wasauzi kuacha kutembea na kipande kama unakumbuka mauaji ya Soweto aliwaambia waache vitambulisho waende woote wakakamatwe police...waliuawa wengi na hiyo kesi ndio iliyomuua Stive biko 1977...
 
Stive Biko ndie aliewaamsha wasauzi kuacha kutembea na kipande kama unakumbuka mauaji ya Soweto aliwaambia waache vitambulisho waende woote wakakamatwe police...waliuawa wengi na hiyo kesi ndio iliyomuua Stive biko 1977...
Stive biko ni nan mkuu.? Na alikufaje..?
 
Stive Biko ndie aliewaamsha wasauzi kuacha kutembea na kipande kama unakumbuka mauaji ya Soweto aliwaambia waache vitambulisho waende woote wakakamatwe police...waliuawa wengi na hiyo kesi ndio iliyomuua Stive biko 1977...
Mkuu Isanga Family na wengine,
Harakati za kupinga ubaguzi wa rangi nchini Afrika Kusini, hususani, kwa kutumia mbinu ya kuacha kubeba "pass", zilianza hata kabla ya Steve Biko. Moja ya tukio kubwa la watu kukata "pass" ni lile la watu kuchoma "pass" zao na kujipeleka wenyewe katika vituo vya polisi ili wakamatwe na "kujaza jela zote".

Tukio hili liliratibiwa na kuendeshwa na Pan African Congress (PAC) chini ya Robert Sobukwe. Huu ndio ukawa mwanzo wa mauaji ya Sharpeville mwaka 1960, yaani zaidi ya miaka 15 kabla ya harakati za Steve Biko. Nitaileta mada hii siku za karibuni.
 
Dunia inahitaji mtu mpole, mkarimu na wa kujitolea. Bila ya watu kama Mandela kuna uwezekano wa dunia kutumbukia katika migogoro ambayo haitapata wasuluhishi na kwa mtizamo wa wengi ni vigumu kupata mfano wa Mandela duniani.
Ni kweli. nchi nyingi,hasa Afrika, tumekosa Viongozi wa namna hii........
 
Kwani Mandela alifanya nini la ajabu.
1.Kama ni issue ya kuwasamehe makaburu_hakuwa na option zaidi ya kuacha tu liende maake makaburu bado walikuwa na nguvu kubwa kiuchumi,kisiasa na hata kiutamaduni.
2.Alivyotoka tu alipewa support kubwa na mataifa mbalimbali hivyo kumfanya akubalike,atambulike na asikike dunian kirahisi sana...na hii ilitiwa chumvi na wazungu sababu ya interest za kulinda maslahi ya wazungu wenzao huko SA.
3.Zaidi ya yote..alifanya unafiki wa kuwanadi makaburu kwa nchi za Africa kwa kuwaambia eti ni watu wazuri na hivyo wapokewe popote waendapo kwa mgongo wa uwekezaji....na hili alilifanya maksudi sababu alijua raslimali za SA zitaanza kugombewa na waafrica vs makaburu na kuleta chaos nchini kwao.
..........better kama ungesema kina Nyerere,Nkhrumah,Lumumba,Biko,Mgabe,Ghaddafi etc...kuliko huyo Mandela.
 
ANC walimchagua Mandela kuwa nembo yao ya kupigania uhuru lakini akiwa jela kuna wakina Oliver Tambo ambao walikuwa strategist wa chama. Namkubali Mandela kwa kutokulipiza kisasi kwa makaburu na kukaa madarakani kwa miaka mitano tu kitu ambacho kwa viongozi waafrika hasa waliopigania uhuru ni adimu sana. Lakini ukija kwenye mambo ya ukombozi wa africa - nani kama Nyerere (kwa mawazo na matendo) na kwa hili Mandela haoni ndani (check na Mzee Kaunda au Brother Mugabe).
 
Back
Top Bottom