Hivi karibuni kumetokea sintofahamu na kupishana kauli baina ya wajumbe wa TEC.
Mm nimeenda mbele zaidi je ni kweli hakuna mawasiliano baina Yao?!
Au ni mchezo wa kitaalamu na zoelefu wa hao magwiji wa Teolojia duniani?!
Nisaidie kung'amua ukweli.Maana hainiingii akilini eti wajumbe hao pamoja na umoja wa dhehebu lile hapa duniani itokee kutofautiana namna ile!
Huwa wanatofautiana kwa mambo mengi kama tu ilivyo kwa jumuiya yoyote na hatimaye hupiga kura na matokeo ya kura uwa ndio msimamo wa Baraza.
Minutes za mikutano yote ya Baraza huwasilishwa Holy See katika idara inaitwa Propaganda Fide ambayo husimamia shughuli zote za makanisa mahalia ya nchi za missioni! Nchi ya Missioni ni ile ambayo ukristu hauna umri za Zaidi ya miaka 500 kama nchi nyingi za Kiafrika. Pia nchi za missioni zi zile ambazo huendeshwaji wake unategemea ruzuku ya hiyo idara ya Propaganda Fide.
Tumezoea kuiita waraka lakini wenyewe wanaita Pastoral Letters.
Kuna waraka wa aina mbili: 1. Waraka wa kawaida mfano Waraka wa Kwaresima, Waraka wa Jumapili ya Msamaria Mwema, Waraka wa Jumapili ya Msamaria Mwema, Waraka wa Jumapili ya Misioni nk nyaraka hizi ni za kawaida hutolewa kila mwaka. 2. Nyaraka maalumu hizi hutolewa pale panapokuwa na shida maalum au dharula mahususi. Wakati wa awamu ya Rais Mwinyi Baraza lilitoa nyaraka maalum 3. Wakati wa awamu ya Mkapa Baraza halikutoa nyaraka maalum yoyote kwa muda wa miaka 10.
Hata huu waraka wa Juzi ni waraka wa kawaida sema tu mwandishi akaongeza ile sura inaongelea siasa. Nadhani hoja ya Pengo inalalia hapa, kwamba ule ulipaswa kuwa waraka wa kawaida wa kuwaelekeza waamini kuhusu mfungo wa Kwaresima.
Nyaraka hizi wala haziandikwi na Maaskofu wote. Na wala hazipelekwi kwa Maaskofu wote kwa proof reading kabla hazijatolewa.
Baraza limegawanywa katika idara mbalimbali kama vile mawasilaino, uchungaji, elimu, liturjia nk na kila idara husimamiwa na Askofu aliyechaguliwa na Rais wa Baraza. Kwa vile Maaskofu wana kazi nyingi na wengi wao hawaishi katika makao makuu ya Baraza, idara hizo husimamiwa na makatibu wakuu kwa utendaji wa siku kwa siku. Mapadre hawa ambao huchaguliwa na Maaskofu huwa ni wabobezi katika idara husika. Kwa mfano katibu wa idara ya liturjia lazima awe mtaalamu wa ngazi sio pungufu ya shahada ya uzamivu katika fani husika.
Hawa ndio huandaa hizi nyaraka kutegemea na muktadha wa nyaraka yenyewe. Katika kanisa Katoliki ni Maaskofu ndio wenye jukumu na mamlaka ya kufundisha na kusimamia waamini, wao ndio majina yao hujitokeza kama waandishi wa hizo nyaraka. Maaskofu huwa hawana mashaka na utendaji wa hao makatibu wakuu wa idara.
Nyaraka za Maaskofu zina nguvu ya Magisterium inayopita nguvu ya askofu wa jimbo.
Niwape mfano katika Jimbo la Dar es Salaam waamini hawaruhusiwi kupokea Ekaristi wakiwa wamepiga magoti. Ukienda Jimbo la Moshi kupiga magoti ndio utaratibu wa kawaida. Zuio hilo halina nguvu ktk Jimbo la Moshi kwa sbb limetolewa na Askofu Mkuu wa Dar es Salaam. Zuio hili lingekuwa limetolewa na Baraza majimbo yote yangelazima kufuata hata kama hawataki.
Ndio maana Pengo hata kama hapendi hawezi kuzuia hizo nyaraka zisitoke, na wala kutoka kwake hakuhitaji baraka zake.