SoC03 Kuna Machozi ya Mamba kwenye kupambana na uharibifu wa Mazingira

Stories of Change - 2023 Competition

BLACK MOVEMENT

JF-Expert Member
Mar 11, 2020
2,712
6,507
Mamba anajulikana kwa kuwa na machozi ya kinafiki sana, unaweza muona analia machozi yanatoka kumbe ana zuga.

Sasa na sisi kwenye Kupambana na uharibifu wa Mazingira ni bora tukaacha unafiki kama wa Mamba.

Mabadiliko ya Tabia nchi ni kweli yapo na yanaendelea kutuletea matatizo makunwa sana na hii ni Dunia nzima, Africa kama Africa hatujaachwa nyuma na mabadiliko ya tabia nchi na ukiangalia kwa nchi zetu kama Africa sababu kubwa ni kwa sababu ya shughuri za kibinadamu ambazo ndio zinapelekea kuwe na majanga hasa ukame au mafuriko makubwa sana.


Tanzania kuna kiwango cha juu sana cha kuharibi mazingira hasa ukataji miti, make hii ndio kiini hasa cha matatizo yote, miti inakatwa sana kwa mikaa na kuni, kuanzia mijini na vijijini kote huko ni mikaa na kuni, hali ni mbaya sana. Kaskazini kote huko hali ni mbaya sana kwenye swala la uharibifu wa mazingira.

Kuna taasisi mbali mbali zinazo pambana na hili swala la kutunza mazingira na wengine ni watu binafisi na kuna ambao hata huenda kumuomba Mungu aachilie mvua. Ila kwenye hizi taasisi zote ziwe binafisi na za Serikali kuna kitu huwa hatuulizani nacho ni kwamba JE MAJUMBANI KWETU TUNATUMIA NINI?


Majumbani kwetu tunatumia nini? Hili ni Swali muhimu sana kwa wale wote wanao pambana na mazingira, Majumbani kwetu tunatumia nini kupikia? Kama nyumbani kwetu stoo imejaa kuni na mikaa basi ni bora muda wa kwenda kuombea mvua ukaenda kufanya kazi zingine kwa sababu hata Mungu sio fala kiasi hicho kwamba unaharibu vitu alivyo umba na unarudi tena kumuomba mvua.

Ifike wakati Jamii kama tunataka kweli kupambana na mabadiliko ya Tabia nchi basi tuache unafiki.

Taasisi zinazo Pambana na Mazingira; Je hawa wafanya kazi wa hizi taasisi majumbani mwao wanatumia nini kama nishati? Hawa kama wanatumia kuni na mikaa basi wana kiwango kikubwa sana machozi ya mamba na malengo yao sio kupambana na uharibifu wa mazingira bali ni kujipatia pesa kutoka kwa wafadhili, ,make huwezi kuwa wakili wa kutetea mazingira ilihali nyumbani kwako umejaza magunia ya mikaa.

Mikutano ya injii Kuombea Mvua; Kabla Sara haijaanza kutolewa swali kuu liwe ni je wale tulio kusanyika je majumbani kwetu hatutumii kuni na mikaa? Mashambani kule hatukati miti hovyo? Wale wachungaju na mashehe wanao ongoza maombi je kweli wana chukia uharibifu wa mazingira hasa ukataji wa miti hovyo?

Je Wale Maaskari wanao linda misitu wanatumia nishati gani majumbani mwao? Hili ni swali pia ninalo kuwa najiuliza kwamba wale askari majumbani kwao wanatumia nini hasa?wana stock za mitungi ya gesi au ni hizi hizi kuni na mikaa? Kama ni kuni na mikaa basi hawana nguvu ya kupambana na uharibifu wa mazigira ilihali wao majumbani mwao wanatumia mikaa na kuni.

Serikali na Magari yake; Hakuna ubishi kwamba magari ya Serikali na taasisi zake ndio wanaongoza kwa kubeba mikaa tena wanafanya hivyo makusudi kwa sababu wanajua hawakaguliwa na mtu, sasa kama Serikali inahubiri mazingira na huku Magari yake yakiwa ndio bingwa wa kubeba mikaa hii sio sawa kabisa, huwezi hubiri maji huku unakunywa wine? Hatuwezi hubori kuokoa misiyu huku magari yetu yakiwa ndio wabeba mikaa wakuu, hapa tuna zuga na ni kiwango cha juu cha unafiki mubwa sana.Na sijawahi sikia waziri hata wa Mazingira analitolea maelezo hili la Gari za umma kuwa zina ongozakubeba mikaa tena yamagendo.

Nini kifanyike sasa angalau kuokoa mazingira na kuwa kweli tuko Serious na kuokoa mazingira yetu?

  1. Wale tunao enda kuombea mvua tuhaikishe sisi majumbani kwetu ni kweli tunachukia mkaa na kuni na sio kwenda kuombea mvua ilihali stoo imejaa kuni na mikaa, Mungua sio mnafiki hawezi sikiliza sara za aina hii kamwe. Tuhakikishe ni mawakili kweli wa kutetea mazingira na sio kuwa wanafiki wakuu na kuwa kujivika ngozi za kondoo kumbe ndani ni Mbwa mwitu.
  2. Wale Maaskari wana pambana na kulinda misitu wapewe gesi za hata bure za kupikia majumbani kwao,ili basi wawe na nguvu kidogo ya kulinda misitu make kuna wakatu hata wao wenyewe huchoma mikaa yak wenda kutumia majumbani mwao.
  3. Magari ya Serikali yasibebe mikaa, wafanye kama zilivyo NGOs ambazi yingi haziruhsu magari ayo kubeba mikaa na ni kosa kabisa. Ni wakati sasa Serikli itembee kwa kile inacho hubiri kiuhusu mazingira.
  4. Wewe Mkulima kama wewe ndio bingwa wa kukata miti shambani kwako basi acha na la sivyo unapo kuwa huoni mvua uslalamike kwa sababu sababu ni wewe na mchawi mkuu ni wewe na si mwingine, wakulima ni moja ya watu wanao haribu sana mazingira hivyo tuache kukata miti la sivyo tukae kimya tunapo ona hakuna mvua.
Tutaweza pambana na mazingira endapo tutaacha unafiki tofauti na hapo tutaangamia kwa sababu kuu moja unafiki mkubwa sana wa sisi kujifanya tunauchungu na mazingira kumbe ni kilio cha machozu ya Mamba.
Uharibifu wa mazingira ni tatizo kubwa sana na ni tatizo ambalo wale tunaombana nalo tjmejawa.na machozi ya mamba, ifike wakati sasa tuwe serious na hili tatizo tuachane na kudanganya.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom